Saturday, July 26, 2014

OKWI, KIIZA WAMPASUA KICHWA MAXIMO

 Kocha wa Yanga, Marcio Maximo amesema mchezaji yeyote mwenye ubinafsi hana nafasi kwenye kikosi chake, huku akishindwa kujua yupi wa kumuacha kati ya wachezaji wawili wa kimataifa.
Akizungumza jana mara baada ya mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Loyola, Maximo alisema hadi sasa hajaamua wa kumuacha kati ya Emmanuel Okwi na Hamis Kiiza.
“Kwa sasa siwezi kusema ninayemuacha hadi Septemba 17, nitatangaza nitakayemuacha, ila wachezaji wabinafsi hawatakuwa na nafasi katika kikosi changu.
“Nataka mchezaji anayejituma kwa moyo, anayepigania maslahi ya timu kwanza na si kukimbilia maslahi yake peke yake, tukiwa na umoja tunashinda pamoja, na kama tunapoteza tunaumia pamoja,” alisema Maximo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Alisema wachezaji anaowahitaji kwenye kikosi chake ni wale ambao wanajituma, wanajua wajibu wao uwanjani, anataka wachezaji kucheza kitimu badala ya kumtegemea mtu mmoja.
Mbrazil huyo alisema anataka kuijenga timu hiyo icheze kitimu zaidi kuliko kucheza kwa kumtegemea mchezaji fulani, kitu ambacho kinaathari pindi mchezaji husika anapokosekana.
“Nimejifunza mengi hasa kupitia Kombe la Dunia na kuona jinsi gani timu zilizokuwa zikiwategemea baadhi ya wachezaji zilivyoathirika tofauti na zile, ambazo zilicheza kitimu,” alisema Maximo na kuitolea mfano Ujerumani, mabingwa wa dunia.
Aidha, Maximo ambaye anakinoa kikosi cha timu hiyo akisaidiwa na wasaidizi wake watatu, Mbrazil mwenzake Leonaldo Leiva na Watanzania Salvatory Edward pamoja Juma Pondamali, ambaye ni wa makipa, alisema kwa sasa anaingiza mfumo wa timu hiyo kucheza kitimu muda wote kama ilivyo kwa Wajerumani.
Katika mazoezi ya jana, Maximo aliwapa mazoezi ya kuwajengea pumzi wachezaji wake ikiwa ni kukimbia kwa spidi na mpira na kumkabidhi mchezaji mwingine, ikiwa ni pamoja na kufanya ‘pushapu’, kabla ya kuwapa mbinu za kufunga na kukaba.
Yanga inajiandaa kwa mashindano ya Kombe la Kagame na Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septema, baada ya tarehe ya awali kubadilishwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...