Wednesday, August 13, 2014

UKAWA WAANZA VITA UPYAAA...!!!



Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe  akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.  Wanaomfuatia ni wenyeviti wenza wa umoja huo James Mbatia (katikati) na Profesa Ibrahimu Lipumba.


Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umemtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma na iwapo hatafanya hivyo utaongoza maandamano nchi nzima.

Umoja huo pia umeeleza kuwa kuendelea kwa Bunge hilo ni sawa na kuvuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya, kuiweka nchi rehani, kufuja fedha za walipakodi, kuwahadaa Watanzania kwa kupitisha Katiba isiyotokana na maoni yao, huku kanuni zikibadilishwa na kuingizwa mambo ya Tanganyika katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kadhalika, umemtaka Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalumu wa matumizi ya fedha za Bunge hilo kwa maelezo kuwa zinatumika bila maelezo sahihi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 13, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


..
.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RONALDO AIONGOZA MADRID KUICHAPA SEVILLE MABAO 2-0 NA KUTWAA UBINGWA WA SUPER CUP.

Capture
Cristiano Ronaldo amefunga mabao yote mawili yaliyoipa ushindi wa mabao 2-0 timu yake ya Real Madrid dhidi ya FC Seville kwenye mchezo wa UEFA Super Cup ulipigwa nyumbani kwa Gareth Bale Mjini Cardiff kwenye dimba la Millenium.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United alifunga mabao hayo mbele ya mashabiki 33,500 na kuipa Real ubingwa huo kwa mara nyingine tangu mwaka 2002.mchezo huo pia ulihudhuliwa na kocha wa zamani wa Man Utd Sir Alex Ferguson
Real Madrid kwenye mchezo huo iliwatumia nyota wake iliowasajili msimu huu kiungo mjerumani Toni Kroos pamoja na mshambuliaji raia wa Argentina James Rodriguez.
Nahodha wa timu hiyo Iker Casillas alikaa milingotini siku moja tu baada ya aliyekuwa mpinzani wake msimu uliopita Diego Lopez kujiunga na AC Milan ya Italia.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...