Thursday, February 15, 2018

RAIS WA AFRIKA KUSINI AJIUZULU...!!!

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejiuzulu baada ya shinikizo nyingi kutoka kwa chama chake.

Kapitia hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni alisema anajiuzulu mara moja lakini akaongeza kuwa hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC.

Chama cha ANC kilikuwa kimemuambia aondoke madarakani au akabiliwe na kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

ZARI AMMWAGA DIAMOND SIKU YA WAPENDANAO

Katika siku ya wapendanao,  jana Februari 14, 2018, Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Kati na Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady ametangaza kuvunja rasmi mahusiano yake ya kimapenzi na Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagaram, Zari amefunguka kuwa kilichompelekea kufanya hivyo ni kutokana na Diamond kutokuwa mwaminifu kwenye mahusiano yao huku akibainisha kuwa kuachana katika mahusiano ya kimapenzi hakutaathiri uhusiano wao kama wazazi.

Diamond ambaye alianza mahusiano na Zari takribani miaka mitano iliyopita baada ya kuachana na staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu, amezaa na Zari watoto wawili ambao ni Tiffah na Nilan huku pia akitajwa kuchepuka jambo ambalo limepelekea akazaa mtoto mwingine na mwanamitindo Hamissa Mobeto.

Mbali na Mobeto, Diamond amekuwa akihusishwa kurudiana na Wema ambapo hivi karibuni walionekana kugandana kwenye hafla ya kutambulishwa kwa msanii Mbosso kwenye lebo ya WCB Wasafi.

Bado haijathibitika moja kwa moja iwapo kweli wameachana ama ni kiki kama ambavyo wasanii wengine wamekuwa wakifanya.

KIONGOZI MKUU WA UPINZANI ZIMBABWE AFARIKI DUNIA

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amefariki dunia nchini Afrika kusini.

Kwa mujibu wa kiongozi Mwandamizi wa chama cha MDC, Tsvangirai mwenye umri wa 65, na aliyewahi kushika nafasi ya Uwaziri mkuu nchini Zimbabwe ameripotiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya utumbo.

Makamu Rais wa chama chama cha MDC Elias Mudzuri ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters kwamba marehemu alifariki jioni ya Februar 14.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...