Wednesday, September 24, 2014

ESTER BULAYA ATANGAZA VITA NA WASIRA...!!!




Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mkoa  wa Mara, Ester Bulaya akizungumza  katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili, Dar es Salaam jana.

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Bunda ambalo linashikiliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira.

Kwa nia hiyo, Bulaya anaweza kuwa ametangaza vita dhidi ya Wasira ambaye hivi karibuni akiwa Bunda, alitangaza kukitetea kiti chake hicho katika Uchaguzi Mkuu 2015.

Julai 8, mwaka huu Wasira akiwa kwenye kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM wilayani Bunda, alitangaza kuwa atatetea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao, huku akijigamba kuwa yeye ni “mwarobaini wa matatizo” yanayowakabili wakazi wa jimbo hilo.

Kabla ya kutangaza nia hiyo, mara kadhaa Wasira amekuwa akihusishwa na suala la urais na ni mmoja wa makada sita wa CCM ambao walipewa adhabu na chama hicho Februari 18 mwaka huu, baada ya kukutwa na makosa ya kuanza mapema kampeni za urais mwaka 2015.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, Bulaya alisema atagombea ubunge katika Jimbo la Bunda na anamtakia kila heri mpinzani wake huyo (Wasira) katika nafasi ya juu ya urais anayotaka kuwania. Alisema ameamua kufanya hivyo baada ya kuombwa na watu kadhaa kutoka jimboni humo wakiwamo vijana, wazee na kinamama. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BUNGE LA KATIBA KUTUMA OFISA SAUDIA KUSIMAMIA KURA




Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba, Andrew Chenge akionyesha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kabla ya kumkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, mjini Dodoma jana. Rasimu hiyo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni leo. 


Ofisi ya Bunge la Katiba itamtuma ofisa wake kwenda Makka, Saudi Arabia kusimamia upigaji kura kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa wajumbe wa Bunge hilo wanaokwenda Hijja.

Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad alipotakiwa kueleza idadi kamili ya wajumbe wa Bunge hilo wanaotarajiwa kuwa nje ya nchi na jinsi watakavyopiga kura.

Juzi, Bunge hilo lilizifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwaruhusu wajumbe watakaokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo wanaokwenda Hijja kuipigia kura Katiba inayopendekezwa, iliyokabidhiwa kwa Kamati ya Uongozi jana.

Chini ya marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya Bunge, ataruhusiwa kupiga kura ya wazi au ya siri kwa njia ya fax au mtandao kama itakavyoelekezwa na katibu kwa kushauriana na mwenyekiti.

Hamad alisema hadi kufikia jana mchana walikuwa wamewatambua wajumbe wanane ambao watakwenda Hijja huko Uarabuni lakini orodha ya watakaokuwa nchi nyingine bado haijajulikana.

Hamadi alisema ofisa wake huyo atasimamia kura za wajumbe wanaokwenda Hijja katika upigaji kura unaotarajiwa kuanza Septemba 29 hadi Oktoba 2 mwaka huu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KINANA, NAPE WAKERWA NA MASHINE ZA EFD NA BVR




Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Kwenjugo, Handeni jana, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Tanga.

Chama Cha Mapinduzi kimeonyesha wasiwasi kuhusu matumizi ya teknolojia ya kielektroniki katika uandikishaji wa wapigakura na mashine za ukusanyaji wa kodi (EFD).

Wasiwasi huo umeelezewa kwa nyakati tofauti na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati wakihutubia mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Chalinze, wilayani Bagamoyo juzi.

Kinana alihoji utaratibu aliouita mbovu katika matumizi ya mashine za kielektroniki za kutunza hesabu za wafanyabiashara (EFD) na Nnauye alieleza wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutumia teknolojia ya Biometric Voter Registration (BVR) katika kuandikisha upya wapigakura.

Nnauye aliishauri Nec kuangalia upya uamuzi wake huo akisema hauna mantiki kwa kuwa utaliingizia Taifa gharama ambazo zinaweza kuepukwa kwa urahisi.

Teknolojia hiyo iliwahi kulalamikiwa bungeni na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe katika hotuba yake ya bajeti mwaka jana, akisema NEC imeanzisha utaratibu huo bila kuwashirikisha wadau.

Akitoa mifano, Nnauye alisema matumizi ya teknolojia hiyo yalizua mtafaruku katika chaguzi za nchi za Kenya, Malawi na Ghana na haitakuwa busara Tanzania nayo kujiingiza kwenye matatizo kama hayo wakati ina uwezo wa kuyaepuka. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 24, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MMILIKI WA ALIBABA ATARAJIRIKA ZAIDI

Mwanzilishi wa Alibaba ndiye tajiri zaidi nchini Uchina 

Mwanzilishi wa mtandao wa Alibaba ndiye tajiri mkubwa zaidi nchini Uchina kulingana na rekodi za kampuni yake.
Hili imethibitishwa na ripoti rasmi ya kifedha ya Hurun.
Bw.Ma ameongoza orodha ya watu tajiri zaidi nchini Uchina kwa mali ya takriban dola bilioni 25 akifuatwa na mwenyekiti wa Wanda Group Wang Jianlin.
Matajiri watano katika ya kumi walio katika orodha hiyo, wanamiliki kampuni za mitandaoni huku wakiwabwaga wale wanaomiliki mali isiyohamishika ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiongoza orodha hiyo.

Orodha hiyo inahusisha pia kiongozi wa Tencent Pony Ma.
Mabwenyenye wengine walio katika orodha hiyo ni mwanzilishi mwenza wa mtandao wa intanet marufu sana nchini China Baidu, Robin Li na pia mwanzilishi wa soko la mtandao la JD.com, Richard Liu Qiangdong.
Bw Liu ambaye kampuni yake ilihusika katika ubadilishanaji wa hisa huko New York hapo Agosti mwaka huu, aliorodheshwa katika nafasi ya kumi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JESHI LABADILI KAULI KUHUSU WANAFUNZI WALIOTEKWA

Wazazi wa wanafunzi waliotekwa nyara na Boko Haram nchini Nigeria wakiishi kwa kilio 

Jeshi la Nigeria limekanusha taarifa ya awali kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule waliotekwa nyara kutoka Chibok na wapiganaji wa Boko Haram, wameachiliwa.
Msemaji wa jeshi nchini Nigeria, Meja Generali Chris Olukolade, ameambia BBC kuwa wanawahifadhi wasichana kadhaa lakini akakana kuwa wasichana hao ni baadhi ya wale waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram kutoka Chibok.
Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na Boko Haram kutoka shule ya mabweni Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno.
Utekaji nyara huo ulisababisha ghadhabu kote nchini Nigeria na duniani kote kiasi cha kusababisha kampeini ya kutaka kuokolewa kwa wasichana hao kwenye mitandao ya kijamii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MHUBIRI ABU QATADA AACHIWA HURU

Abnu Qatada alikabiliwa na tuhuma za kupanga njama ya mashambulizi ya kigaidi nchini Jordan
Mhubiri muisilamu mwenye utata ambaye alihamishwa kutoka Uingereza mwaka 2013, Abu Qatada, ameachiliwa huru nchini Jordan baada ya mahakama kutompata na hatia.
Alikuwa ametuhumiwa na kosa la kuhusika katika njama ya kupanga mashambulizi ya kigaidi ambayo ilitibuliwa mwaka 2000.
Jopo la majaji waliokuwa katika mahakama hiyo, hawakumpata na hatia yoyote bwana Qatada kutokana na madai kuwa alihusika na njama hiyo ya ugaidi.
Uamuzi huo umetolewa baada ya Abu Qatada kutopatikana na hatia mwezi Juni katika kosa lengine la kupanga njama ya mashambulizi mwaka 1998 nchini Jordan.
Abu Qatada alitimuliwa kutoka Uingereza mwezi Julai mwaka 2013 kwa madai ya kueneza itikadi kali Uingereza ikitaka afunguliwe mashitaka nchini Jordan. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JAJA AFUTA KESI YA OKWI FIFA

 

Mhaiti huyo alisema katika timu mbalimbali alizowahi kucheza, amekutana na Wabrazili kadhaa walioonekana kuwa moto wakati wa maandalizi ya ligi, lakini walipotea baada ya mechi tatu hadi nne ligi husika zilipoanza.


Kiwango cha juu kilichoonyeshwa na mshambuliaji Genilson Santos ‘Jaja’ kimefanya uongozi wa Yanga, kutupilia mbali wazo la kumshitaki Emmanuel Okwi kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa( Fifa).

Tangu aliposajiliwa na Yanga, Jaja ameonyesha kiwango cha juu cha ufungaji mabao akiwa amefunga mabao manne katika mechi sita alizocheza hadi sasa katika michuano mbalimbali.

Jaja aliwasahaulisha Wanayanga kabisa habari za Okwi wakati alipofunga mabao mawili ya ufundi wa hali ya juu katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam walioshinda 3-0.

Kwa mujibu wa taarifa ilizolifikia gazeti hili, zinasema kikao kilichofanyika wiki iliyopita kati ya wanasheria na baadhi ya wanachama wa Yanga wamemshauri mwenyekiti wao Yusuf Manji kuachana na jambo hilo kwa sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...