Jeshi
la Nigeria limekanusha taarifa ya awali kuwa baadhi ya wanafunzi wa
shule waliotekwa nyara kutoka Chibok na wapiganaji wa Boko Haram,
wameachiliwa.
Msemaji wa jeshi nchini Nigeria, Meja Generali Chris
Olukolade, ameambia BBC kuwa wanawahifadhi wasichana kadhaa lakini
akakana kuwa wasichana hao ni baadhi ya wale waliotekwa nyara na
wapiganaji wa Boko Haram kutoka Chibok.
Zaidi ya wasichana 200 walitekwa nyara na Boko Haram kutoka shule ya mabweni Kaskazini Mashariki mwa jimbo la Borno.
Utekaji
nyara huo ulisababisha ghadhabu kote nchini Nigeria na duniani kote
kiasi cha kusababisha kampeini ya kutaka kuokolewa kwa wasichana hao
kwenye mitandao ya kijamii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Maandamano yenye kauli mbiu,
(#BringBackOurGirls) yaliandaliwa kutoa wito kwa watawala kuongeza
juhudi za kuwanusuru wasichana hao,
Muda mfupi baada ya kuwateka
nyara,Boko Haram, ilitoa kanda ya video wakisema kuwa wasichana hao
wataachiliwa tu ikiwa serikali itakubali kuwaachilia wapiganaji wa kundi
hilo ambao wanazuiliwa.
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na
ripoti ambazo hazijathibitishwa zikisema kuwa serikali ya Nigeria
imekuwa ikifanya mazungumzo na Boko Haram, kubadilishana wasichana hao
na wapiganaji wao wanaozuiliwa.
Tangu kutolew kwa amri ya kutotoka
nje nyakati za jioni, katika eneo la Kaskazini Mashariki kwa lengo la
kutatiza harakati za Boko Haram, kundi hilo limekuwa likiendeleza
mashambulizi.
Wanawake wengi na watoto, wakiwemo wasichana wamekuwa wakitekwa nyara.
Awali,
Generali Olukolade aliambia BBC kuwa shughuli inaendelea ya kuwaokoa
wasichana hao na kwamba baadhi ya wasichana haio wako salama katika
kambi za jeshi.
Hata hivyo msemaji huyo baadaye alisema kuwa jeshi
linajaribu kuwatambua wasichana hao ambao wako chini ya ulinzi wa jeshi
lakini hawakurejea kutoka Chibok. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment