Kiwango cha juu kilichoonyeshwa na mshambuliaji Genilson Santos ‘Jaja’ kimefanya uongozi wa Yanga, kutupilia mbali wazo la kumshitaki Emmanuel Okwi kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa( Fifa).
Tangu aliposajiliwa na Yanga, Jaja ameonyesha
kiwango cha juu cha ufungaji mabao akiwa amefunga mabao manne katika
mechi sita alizocheza hadi sasa katika michuano mbalimbali.
Jaja aliwasahaulisha Wanayanga kabisa habari za
Okwi wakati alipofunga mabao mawili ya ufundi wa hali ya juu katika
mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam walioshinda 3-0.
Kwa mujibu wa taarifa ilizolifikia gazeti hili,
zinasema kikao kilichofanyika wiki iliyopita kati ya wanasheria na
baadhi ya wanachama wa Yanga wamemshauri mwenyekiti wao Yusuf Manji
kuachana na jambo hilo kwa sasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Ni ukweli ulio wazi hakuna mwanachama yeyote wa
Yanga anayetaka Okwi arudi; kutaka kwenda Fifa ni kupoteza muda na fedha
nyingi ambazo zingeweza kufanya vitu vingine vya maana. Okwi mwenyewe
amekwisha, hizo Dola 60,000 alizochukua ni sadaka tumempa,” alisema
mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina.
Wakili wa Yanga, Sam Mapande alipoulizwa
kuhusiaana na suala hilo alisema “Ni kama limeisha siwezi kulizungumza
kwa undani Katibu Mkuu Beno Njovu ndiyo mwenye mamlaka ya kufanya
hivyo.”
Naye Benno Njovu alipotafutwa kuhisana na suala
hilo alisema “Unajua haya mambo ni ya kimahakama sasa kama kitu kipo
mahakamani siwezi kukizungumzia.”
Alipoulizwa iwapo wameacha kwenda Fifa na badala
yake wamekimbilia mahakamani, Njovu alisema, “Hata huko Fifa ni mtindo
wa mahakama, nisingependa kuongelea kitu kilichopo mahakamani.”
Mwanzoni mwa mwezi huu, TFF kupitia kwa Kamati ya
Sheria na Hadhi ya wachezaji chini ya Richard Sinamtwa ilimuidhinisha
Okwi kuwa ni mchezaji huru na ana uwezo wa kujiunga na timu yoyote baada
ya kubaini Yanga ilikiuka makubaliano ya mkataba na ilikuwa na lengo ya
kumkomoa mchezaji.
Yanga iliingia kwenye mgogoro na mshambualiji
huyo baada ya kushindwa kumtimizia mahitaji yake ya kimkataba ikiwa ni
kummalizia deni lake la Dola 50,000 za usajili, nyumba na bima. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment