Mwanzilishi wa mtandao wa Alibaba ndiye tajiri mkubwa zaidi nchini Uchina kulingana na rekodi za kampuni yake.
Hili imethibitishwa na ripoti rasmi ya kifedha ya Hurun.
Bw.Ma
ameongoza orodha ya watu tajiri zaidi nchini Uchina kwa mali ya
takriban dola bilioni 25 akifuatwa na mwenyekiti wa Wanda Group Wang
Jianlin.
Matajiri watano katika ya kumi walio katika orodha hiyo,
wanamiliki kampuni za mitandaoni huku wakiwabwaga wale wanaomiliki mali
isiyohamishika ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiongoza orodha hiyo.
Orodha hiyo inahusisha pia kiongozi wa Tencent Pony Ma.
Mabwenyenye
wengine walio katika orodha hiyo ni mwanzilishi mwenza wa mtandao wa
intanet marufu sana nchini China Baidu, Robin Li na pia mwanzilishi wa
soko la mtandao la JD.com, Richard Liu Qiangdong.
Bw Liu ambaye
kampuni yake ilihusika katika ubadilishanaji wa hisa huko New York hapo
Agosti mwaka huu, aliorodheshwa katika nafasi ya kumi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kulingana na mtafiti mkuu
ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Hurun Report, Rupert Hoogewerf amesema
orodha hiyo imeonyesha kwamba ari ya kufanya biashara kati ya wananchi
wa Uchina bado haijafa.
"Jack Ma ambaye ameorodheshwa wa kwanza,
ni wa kumi na moja kuwahi kushikilia nafasi hiyo katika muda wa miaka
16. Hii inaonyesha mabadiliko makubwa katika uchumi wa Uchina na
kutukumbusha uwezo ulio na masoko mapya yanayojitokeza kwa sasa.”
Orodha ya matajiri inayotolewa na Hurun Report ndiyo inayoaminika sana kwa kuwa hukadiria vizuri utajiri nchini Uchina. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment