Monday, August 04, 2014

SUMAYE ATAJA SIFA 10 ZA RAIS AJAYE...!!!

Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye 

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ametaja sifa 10 za mtu anayefaa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 akiwataka wananchi kuzizingatia na kutokubali kudanganyika.
Alisema mbali na sifa hizo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) inatakiwa kusimamia uchaguzi huo kwa haki na kuhakikisha kuwa daftari la kudumu la wapiga kura linafanyiwa maboresho ili kila Mtanzania apige kura kwa mujibu wa Katiba.
Sumaye alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa albamu Rose Muhando iitwayo ‘Kamata Pindo la Yesu’ katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Sifa 10
Alisema sifa ya kwanza ni kuwa na kiongozi anayetambua, kuulinda na kuthamini umoja... “Kiongozi tunayemtaka lazima atambue hilo na awe tayari kuchukua hatua za kutuimarisha kuwa na nguvu zaidi za kiuchumi na kuimarisha muungano wetu na baadaye muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na hatimaye Afrika.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ASKOFU KAKOBE AWAUNGA MKONO UKAWA KWA KITENDO CHA KUSUSIA BUNGE

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe (asiye vaa suti) akiongoza maandamano ya kuadhimisha miaka 25 ya kuanzishwa kwa kanisa hilo  yalianzia Viwanja vya Chuo Kikuu hadi Kanisani hapo eneo la Mwenge jirani na Mlimani City jijini Dar es Salaam jana. 

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameongeza chumvi katika Mchakato wa Katiba kwa kueleza kuwa anaunga mkono msimamo wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutorejea kwenye awamu ya pili ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba.
Kakobe pia alimtupia lawama Rais Jakaya Kikwete akisema  hotuba yake ya kufungua Bunge hilo ndiyo chanzo cha kuvuruga mchakato mzima wa kupata Katiba Mpya.
Kakobe ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita takriban siku tatu tangu Rais Kikwete alipotoa  hotuba yake ya kila mwezi na kujivua lawama hizo alizokuwa akitupiwa na watu wa kada mbalimbali.
“Naunga mkono Ukawa si kwa asilimia 100 bali asilimia 150 kwa msimamo wao wa kususia vikao. Tena sitegemei kusikia wamerejea bungeni, wakirejea watakuwa wamelogwa. Lazima wahakikishe upungufu huo unafanyiwa kazi kabla ya kurejea kwenye awamu ya pili ya vikao hivyo vilivyopangwa kuanza Agosti 5,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KUHUSU TAARIFA ZA KUACHANA NA JAY Z, BEYONCE ATUMIA 'KUCHA' KUWAJIBU WATU...!!!

Picha: Beyonce atumia
Jay Z na Beyonce wanaendelea na ‘On The Run Tour’ ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
Taarifa za maandilizi ya talaka kati ya wanandoa Jay Z na Beyonce zimendelea kuandikwa na vyombo vikubwa vya habari ambavyo huaminika sana nchini Marekani na Uingereza.
Taarifa hizo zinazotolewa na vyanzo vya karibu zinaeleza kuwa wanandoa hao wameshatengana hata vyumba vya kulala wakati wakiwa wanaendelea na tour yao.
Hata hivyo, Beyonce amekuwa kimya huku akitumia lugha ya picha mara kadhaa kueleza kinachoendelea, na hivi sasa ameamua kutumia kucha zake kuonesha jinsi yeye na mumewe walivyoshibana tofauti na taarifa zilizoripotiwa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 04, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAHASIMU WA SUDANI KUSINI WAKUTANA TENA

Kuna hofu na tisho la njaa Sudan Kusini
Mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na waasi yameanza tena katika nchi jirani ya Ethiopia. Mazungumzo hayo, yalikuwa yameahirishwa kwa wiki kadhaa. Vita vimeendelea nchini Sudan Kusini licha ya makubaliano ya kusitisha vita kufikiwa kati ya pande husika.

Zaidi ya watu milioni moja unusu, wameachwa bila makazi kutokana na vita hivyo. Umoja wa Mataifa na mataifa mengine ya Magharibi yameonya kua Sudan Kusini inakabiliwa na tisho la kukumbwa na njaa.
Maafisa wa baraza la usalama la Umoja huo, wanatarajiwa kuzuru nchi hio wiki ijayo.

Katika mazungumzo hayo, serikali na waasi wanatarajiwa kuzungumzia swala la kubuni serikali ya mpito pamoja na muundo wake. Makataa ya makubaliano hayo ni chini ya wiki moja na huenda muda huo usifikiwe. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KESI YA WANABLOG YAAHIRISHWA

Kesi ya wanablogu kumi waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya ugaidi imeahairishwa hadi Agosti 20.
Kesi hiyo ilianza leo miezi mitatu baada ya tisa kati yao kukamatwa na polisi.
Mmoja wa wanablogu hao alishtakiwa bila kuwepo mahakamani.
Wanakabiliwa na mashitaka ya ugaidi chini ya sheria iliyoshutumiwa ya kupinga ugaidi.
Kesi hii imevutia hisia kubwa nje na ndani ya Ethiopia, hiyo basi hakukuwa na tofauti kubwa ilipoanza hivi leo.
Mahakama hiyo ilijazwa na raia wa Ethiopia, wanahabari hali kadhalika maafisa wa kidiplomasia. Wote walioshitakiwa walifika mahakamani. Mawakili walikuwa wamepinga kwa mapema mashitaka hayo wakisema kuwa hayakuwa na msingi.
Hata hivyo mahakama ilikataa kuwaachilia kwa dhamana wanablogu hao jinsi walivyokuwa wakitaka mawakili wao. Wote kumi wameshitakiwa kwa kubuni kikundi haramu vile vile kushirikiana na makundi ya upinzani yaliyopigwa marufuku ng’ambo na nchini.
Waendesha mashtaka walisema kuwa washtakiwa hao walipokea ufadhili na mafunzo ya kutengeneza vilipuzi.
Kitendo hicho cha kuwakamata wanablogu kimesababisha serikali ya Ethiopia kushutumiwa kimataifa na kutaja kuwa inatumia sheria dhidi ya ugaidi kukandamiza upinzani na uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.
Katika mahojiano ya hivi majuzi na BBC waziri mkuu wa Ethiopia alikanusha madai ya kuwakandamiza wanahabari lakini akasema kuwa serikali haitawavumilia wanablogu na wanaharakati wanaonekana kushirikiana na makundi ya kigaidi nchini humo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...