Monday, May 27, 2013

NAY WA MITEGO AFUNGUKIA ISHU YA KUPIGWA KIBUTI NA WEMA SEPETU...!!

WIKI iliyopita tulimleta kwenu msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma aliyomshirikisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ili umchambue ambapo mlituma maswali, hapa anajibu na kufafanua moja baada ya lingine. SHUKA NAYO…

PONGEZI
Nakukubali sana kaka na ngoma zako unavyochana ukweli, kaza buti utafi ka mbali. Roja, Dar, 0657888221
NAY WA MITEGO: Asante.

VIPI KUHUSU NISHA?
Nay wa Mitego uliwahi kuwadisi Bongo Movies na kusema kwamba wanawake wote wanaojiuza wanatoka kwenye tasnia hiyo, je, ilikuwaje ukatoka na Salma Jabu ‘Nisha’ kwani yeye si mmoja wa Bongo Movies? Rocky, Moshi, 0715289337
NAY WA MITEGO: Sijawahi kutoka na Nisha ni mshkaji wangu tu.

YEYE NA DIAMOND
Kwanza hongera kwa kazi zako nzuri kaka, naomba kufahamu kuhusu ule wimbo uliokuwa ukimrekebisha tabia dogo (Diamond), hivi aliyetunga ni wewe au yeye au mlikaa chini na kutunga pamoja? Siyo siri umetulia hongereni sana. Julianitha Jamushi, Dar, 0712089824
NAY WA MITEGO: Asante, Muziki Gani tumeandika pamoja.

"USHAURI

MIDUME YAPIGANA VIKUMBO KUGOMBANIA PENZI LA WASTARA...!!

TAKRIBAN  wiki moja baada ya kumaliza eda tangu alipofariki mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ Januari 2, mwaka huu, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma anagombewa na midume ikitaka kumuoa.
 
Akizungumza na mwandishi wetu  akiwa nchini Oman, Wastara alifunguka kuwa tangu amalize eda yake hiyo amekuwa akipata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume mitandaoni na wanaomtamkia mwenyewe.
“Jamani mpaka nahisi kuchanganyikiwa kabisa, wanaume zaidi ya mia tano hata sijui walipotokea wanataka kunioa, hadi nahisi majanga,” alisema Wastara.

Wastara alisema kuwa wanaume hao wamekuwa wakihangaika bure kwa sababu kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa kwani anapotembea bado anasikia harufu ya mumewe Sajuki.
 
“Bado harufu ya Sajuki ipo mwilini mwangu, wanaume wanaonitolea macho mtoto wa mwenzao wanakosea sana, sifikirii kabisa suala hilo kwa sasa,” alisema Wastara mwenye mtoto mdogo aliyezaa na Sajuki.

MAMA AMUUNGUZA MOTO MWANAE WA KUMZAA.....!!!

 Mkono wa Fikiri Haus 13 uliounguzwa unavyo onekana kwa karibu huo ni ukatiri ulio kithiri
Mtoto Fikili Hausi Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Shule ya Msingi ya Majengo Mansipaa ya Songea akiwa amelazwa Hospitali ya Mkoa baada ya Kunguzwa Moto na Mama yake.
Jeshi la Police lina endelea kumtafuta mama yake Fikili Hausi
  Msomaji hebu angalia Jamii ya watanzania kila siku inafanya makongamano ya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na mama, je kitendo kama hiki watanzania tunaenda wapi?
(Picha na Songea Habari)

MKE AMNASA MUMEWE AKIMLAWITI SHOGA WAKIWA GESTI, MKE AANGUA KILIO....HII NI ZAIDI YA LAANA...!!!

OPARESHENI Fichua Maovu 'OFM' inayoendeshwa namtandao huu, hivi karibuni mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Ezekiel Malika 'Baba Kulwa' amenaswa gesti na mkewe akiserebuka na shoga aitwaye Aunt Steve na kuibua mtiti mzito, 


 

Tukio hilo lililovuta umati lilijiri Mei 20, mwaka huu kwenye gesti moja (jina tunalo) iliyopo Mwananyamala, Dar ambapo mke wa Ezekiel alivamia na kutembeza mkong’oto wa hasira kwa mumewe.
ILIKUWAJE?
Mei 19, mwaka huu, saa 3:15 asubuhi, mwanamke mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya heshima yake mtaani alilipigia simu gazeti hili na kutoa malalamiko kwamba mumewe amekuwa na tabia ya kulala na wanaume wenzake ambao ni mashoga.
“Jamani, mimi naitwa… (akataja jina), naomba jina langu lisiandikwe gezetini. Malalamiko yangu ni kwamba, mume wangu amekuwa na tabia ya kulala na mashoga, hivi ninavyoongea ana ahadi ya kukutana na mmoja wao gesti kama si kesho basi keshokutwa, niliona meseji kwenye simu ya mume wangu.



“Nawaomba chondechonde, mnisaidie ili hii tabia ikome. Nipo tayari kusikia maelekezo yenu kwa sababu nimesoma kwenye gazeti lenu kwamba mnafichua maovu na huu nao ni uovu,” alisema kwa masikitiko mwanamke huyo.
MKE APEWA MAELEKEZO
Mratibu wa Oparesheni Fichua Maovu alimpa maelekezo mwanamke huyo akimtaka kufuatilia kwenye simu ya mumewe ili kubaini siku ya wawili hao kukutana gesti.
“Nawaahidi kwamba leo hiihii kabla giza halijaingia nitakuwa nimejua siku yao ya kukutana, naomba msiache kupokea simu yangu jamani.”
OFM: Sawa mama, pole sana.


Mwanamke: Asante sana.

ANGALIA PICHA ZA LADY J DEE AKIWA MAHAKAMANI LEO

Mwanamuziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Jay Dee' akiwa na mumewe Gadner Habash kabla ya wakisuburi kesi kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kindondoni leo asubuhi saa 3, angalia picha zaidi

KESI YA LADY JAYDEE NA LWAKATARE KUNGURUMA LEO



WAKATI kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare ikitarajiwa kusikilizwa leo Mei 27 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kesi ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judith Wambura (Lady JayDee) pia inatarajia kusikilizwa tarehemu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kesi hizo zinatarajia kuvuta hisia za watanzania kutokana na mvuto na aina ya kesi hizo,Lwakatale atapanda kizimbani kwa mara nyingine huku akitarajia kupata dhamana ya kesi yake baada ya Mahakama Kuu kumfutia mashtaka ya Ugaidi yaliyokuwa yakimkabili awali na kubaki na shitaka la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky ambayo inadhaminika.
 Kwa upande wa Lady JayDee anatarajia kupanda kizimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani hapo kesho mei 27 .

Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.

WALIOFELI KIDATO CHA NNE WAULA, UFAULU SASA WAONGEZEKA....!!!



Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako  

Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 27, 2013

7 bc143
3 47ad9

FEZA KESSY NA AMMY NANDO NDIO WAWAKILISHI WA TANZANIA KWENYE BBA ‘THE CHASE’



ANGALIA PICHA ZA LULU ANAVYOZIDI KUWA NA MVUTO


Muigizaji wa kike aliyekulia kwenye tasnia ya bongo movie, kwa kuwa alianza tangu akiwa mdogo na hadi sasa kipaji chake kinazidi kung’aa. Haishii kung’arisha kipaji chake tu bali anazidi kuwa na muonekano wenye mvuto pia.

Lulu anaonekana hana stress tena kama ilivyokuwa siku kadhaa zilizopita alipokuwa chini ya ulinzi mkali akituhumiwa kusababisha kifo cha muigizaji mwenzake Steven Kanumba.

Huu ndio muonekano wa Lulu sasa hivi:

 
 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...