Monday, May 27, 2013

NAY WA MITEGO AFUNGUKIA ISHU YA KUPIGWA KIBUTI NA WEMA SEPETU...!!

WIKI iliyopita tulimleta kwenu msanii wa Bongo Fleva anayetamba na ngoma aliyomshirikisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ya Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ili umchambue ambapo mlituma maswali, hapa anajibu na kufafanua moja baada ya lingine. SHUKA NAYO…

PONGEZI
Nakukubali sana kaka na ngoma zako unavyochana ukweli, kaza buti utafi ka mbali. Roja, Dar, 0657888221
NAY WA MITEGO: Asante.

VIPI KUHUSU NISHA?
Nay wa Mitego uliwahi kuwadisi Bongo Movies na kusema kwamba wanawake wote wanaojiuza wanatoka kwenye tasnia hiyo, je, ilikuwaje ukatoka na Salma Jabu ‘Nisha’ kwani yeye si mmoja wa Bongo Movies? Rocky, Moshi, 0715289337
NAY WA MITEGO: Sijawahi kutoka na Nisha ni mshkaji wangu tu.

YEYE NA DIAMOND
Kwanza hongera kwa kazi zako nzuri kaka, naomba kufahamu kuhusu ule wimbo uliokuwa ukimrekebisha tabia dogo (Diamond), hivi aliyetunga ni wewe au yeye au mlikaa chini na kutunga pamoja? Siyo siri umetulia hongereni sana. Julianitha Jamushi, Dar, 0712089824
NAY WA MITEGO: Asante, Muziki Gani tumeandika pamoja.

"USHAURI

Nakukubali kiukweli Nay, mistari yako imesimama kinoma kwani unawachana live, wewe usiwaogope endelea kuwachana mpaka watakapobadilika. Joseph, Dar, 0757247473
NAY WA MITEGO: Hivyo ndivyo ilivyo.

MSAADA


Kaka Nay hongera, wewe ni mkali pia nakukubali ila ningependa unisaidie mimi nina kipaji cha kuimba lakini sielewi nifanyeje, naomba msaada ili kuinua kipaji changu. Ester Samweli, 0718259330
NAY WA MITEGO: Siku tukionana ndiyo tutajua tunafanyaje maana lazima nijue kama kweli unaweza kuimba.
MIPANGO YA BAADAYE
Nay wa Mitego nini mipango yako ya baadaye kuhusiana na fani ya muziki? Mbali na muziki unajishughulisha na nini? Salim Liundi, Dar, 0658110395
NAY WA MITEGO: Mipango ya baadaye ni mingi na itakuwa inaonekana kikubwa tuombeane heri tu, tofauti na muziki mimi ni
mfanyabiashara.
KUHUSU NIKKI MBISHI
Nay vipi una mpango wa kumjibu Nikki Mbishi kwenye wimbo wake mpya alioupa jina la Ney wa Mitego? Riziki Minde, Dar, 0716000045
NAY WA MITEGO: Siwezi kumjibu.

ALIKOTOKEA
Kaka Nay unatokea mkoa gani na una miaka mingapi? Amon, Dar, 0766420999
NAY WA MITEGO: Mimi nimezaliwa Manzese, Dar, Mbeya na Moshi ni kwetu maana mama yangu ni mtu wa Mbeya na baba ni wa Moshi, nina miaka 28.

ANAOMBA UNDUGU
Nakukubali sana Nay kwa kazi yako, ningependa uwe kaka yangu. Amina, Moro, 0652139835
NAY WA MITEGO: Hakuna tatizo, karibu.

VIPI KUHUSU MAGE?
Nakubali kazi zako kaka, eti ni kweli uliwahi kutoka kimapenzi na msichana anaitwa Mage, kipindi hicho ukiwa kinyozi? Sauda, Moro, 0655466809
NAY WA MITEGO: Simjui.

YEYE KUPAKA ‘MEKAPU’
Nay wewe unamtukana Chid Benz kutoboa pua hatukatai ni life staili yake, mbona wewe unapaka ‘mekapu’ na unatinda nyusi hawakusemi? Kapeloo Gamba, Dar, 0713094398
NAY WA MITEGO: Sijawahi kupaka mekapu wala kutinda nyusi.

NI MMACHAME?
Nay mambo vipi, je, ni kweli wewe ni Mmachame wa Uduru (Kilimanjaro)? Msomaji, 0714300280
NAY WA MITEGO: Mimi ni Mmachame lakini sijui wa wapi.

ALIKUWA KINYOZI?
Nakukubali Nay kwa kazi zako ila mimi nakufahamu ulikuwa kinyozi hapo Manzese darajani na ulikuwa na mpenzi anaitwa Magreth, alikuwa anakaa Manzese uzuri na mlishawahi kwenda kupima kwa nia ya kukaa naye lakini pia una mtoto. Msomaji,
0655222782
NAY WA MITEGO: Huyo Magreth simjui kwani katika historia yangu ya uzinzi sijawahi kuwa na msichana mwenye jina hilo, kweli nilikuwa kinyozi na nina mtoto.

ETI WEMA ALIMKATAA?
Kaka Nay nakushauri upige kazi, hivi ni kweli Wema Sepetu alishawahi kukukataa kimapenzi ndiyo maana unampondaga? Msomaji, 0754031039
NAY WA MITEGO: Haijawahi kutokea, Wema ni mshkaji wangu mbona!

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...