Tuesday, May 28, 2013

BRAZIL KUIFUTIA MADENI AFRIKA

Rais wa Brazil Dilma Rousseffalitoa matamshi yake katika mkutano wa AU nchini Ethiopia
Brazil imetangaza kuwa itafutilia mbali au kuwa na makubaliano mapya kuhusu madeni inayozidai nchi za Afrika ambayo yanakisiwa kuwa dola milioni 900.

Miongoni mwa nchi 12 zilizo kwenye orodha ya mataifa yanayodaiwa ni pamoja na Congo-Brazzaville yenye uitajiri mkubwa wa mafuta na gesi, Tanzania ambayo hivi karibuni itaanza kuchimba gesi pamoja na Zambia
Wadadisi wanahisi kuwa hii ni njia mojawapo ya Brazil kutaka kukuza uhusiano wa kiuchumi kati yake ambayo ni ya saba kwa ukubwa kiuchumi na Bara la Afrika.

Taarifa rasmi zinaonyesha kuwa uhusiano wa Brazil na bara la Afrika umeongezeka mara tano katika mwongo mmoja uliopita.

Tangazo hili, lilitolewa wakati wa ziara ya tatu kwa miezi mitatu ya rais wa Brazil Dilma Rousseff,aliyehudhuria mkutano wa Muungano wa Afrika nchini Ethiopia.
"takriban madeni yote huenda yakafutwa , '' alisema msemaji wa Rais Rousseff Thomas Traumann.
"ili kukuza uhusiano kati ya Afrika ni muhimu kwa sera ya kigeni ya Brazil."
Aliongeza kuwa nyingi ya madeni hayo yaliongezeka miaka ya sabini na kuwa kulikuwa na mazungumzo kuyahusu wakati huo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Brazil, alisema kuwa baadhi ya nchi huenda zikafaidika na makubaliano mazuri kuhusu namna ya kulipa madeni hayo huku muda wa kuyalipa ukiongezeka.
Congo-Brazzaville, inadaiwa dola milioni 352 ikifuatiwa na Tanzania inayodaiwa dola milioni 237 Zambia nayo ikidaiwa dola milioni 113.4.

Nchi zingine zitakazofaidika ni pamoja na Ivory Coast, Gabon, Guinea, Guinea Bissau, Mauritania, DRC, Sao Tome and Principe, Senegal na Sudan.

Brazil imekuwa ikiimarisha uhusiano wake wa kibiashara na Afrika, kitovu cha madini kama sehemu ya kile kinachojulikana kama ushirikiano wa kanda ya Afrika Kusini.
Kampuni nyingi za Brazil huekeza sana katika sekta ya mafuta na madini na zimekuwa zikifanya miradi mikubwa ya miundo mbinu barani humo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...