Saturday, November 30, 2013

MPANGO WA SARAFU MOJA WA EAC KUJADILIWA LEO JIJINI KAMPALA

 Wakuu wa Nchi Tano Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), leo Novemba 30, wanatarajiwa kutia saini mkataba wa kuwa na sarafu moja.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa EAC, Richard Owora aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa kuwa sherehe za kutia saini mkataba huo utakaoanzisha mchakato wa miaka kumi hadi kufikia lengo la kuwa na sarafu moja ya EAC, zitafanyika katika Viwanja vya Kololo jijini Kampala.
Marais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Mseveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkuruzinza wa Burundi na Uhuru Kenyatta wa Kenya wanatarajiwa kuwa jijini hapa kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi za EAC.
Umoja wa sarafu ni moja kati ya mambo makuu manne yaliyoainishwa katika mkataba wa EAC. Masuala mengine ni soko la pamoja na umoja wa forodha ambayo tayari mikataba yake imesainiwa na kuanza kutekelezwa, ingawa kwa kasi isiyotosheleza kutokana na vikwazo kadhaa.
Hatua ya mwisho na juu kabisa katika ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni shirikisho la kisiasa linalolenga kuwa na nchi moja, hatua itakayozihakikishia nchi za ukanda huo nguvu ya soko, biashara, majadiliano na uamuzi katika ngazi ya ndani na kimataifa.
Huu ni mkutano wa kwanza kuwakutanisha wakuu wote wa EAC tangu kuibuka kwa migongano ya kimawazo na mtazamo miongoni mwao kuhusu utekelezaji wa makubaliano na miradi iliyo katika mipango ya EAC pamoja na njia bora na sahihi ya kumaliza vita na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya baadhi ya nchi wanachama.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 30, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...