Monday, April 29, 2013

ASKARI MWANAUME ABAKWA NA WANAWAKE WANNE BAADA YA KUTEKWA

Askari mmoja mwanaume anadaiwa kutekwa kisha kudhalilishwa kijinsia na wanawake wanne kwa karibu wiki moja kabla ya kupigwa mawe na kutupwa katikati ya milima.

Mateso ya muathirika huyo mwenye miaka 25 yalianza pale alipopata lifti ya gari kuelekea mji wa Mutare nchini Zimbabwe.
Wanawake wawili na mwanaume mmoja walikuwa kwenye gari, Mercedes Benz, na, baada ya kuendesha kwa takribani saa moja kuelekea mji huo, dereva wa gari hilo akabadili mwelekeo wa safari hiyo.
Ndipo muathirika huyo akalalamika, alitishiwa kwa kisu.
Msemaji wa polisi wa Manicaland, Inspekta Msaidizi Nuzondiwa Clean, alieleza: "Baada ya kubadilishwa mwelekeo huo, mlalamikaji alihoji wapi walikokuwa wakielekea na walimweleza walikuwa wakienda kupata chakula.
 
"Askari huyo alitaka kushushwa, lakini dereva huyo akatoa kisu na kumtishia nacho. Mmoja wa abiria wanawake akamfunga kwa kitambaa cheusi machoni mtuhumiwa huyo."
 Kwa mujibu wa Nuzondiwa,watesi  hao  walimpeleka mlalamikaji kwenye nyumba isiyojulikana ambako walimvua nguo zote na kumpora simu yake na Dola za marekani 35.
 Watuhumiwa walimwamuru mtu huyo kulala na mmoja wa wanawake hao katika matukio kadhaa na alishikiliwa kati ya Aprili 19-23.
 
 Kisha akafungwa tena kitambaa machoni na kushushwa kwenye Milima ya Dangamvura ambako, kwa mujibu wa polisi, alipigwa mawe katika mguu wake wa kushoto, na kumsababishia majeraha makubwa.
 Watuhumiwa hao kisha wakawasha gari lao na kutokomea kusikojulikana.Askari huyo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Sakubva

Mbowe amtwisha mzigo mzito Zitto

Tabora. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kuhakikisha chama kinapata ushindi katika majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Mbowe alisema chama chake kitahakikisha kinachukua majimbo ya Samwel Sitta, (Urambo Mashariki), Ismail Aden Rage (Tabora mjini) na Jimbo la Kaliua la Profesa Juma Kapuya, katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe alimwagiza mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kwamba majimbo hayo yanachukuliwa na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Alimtaka kufanya kampeni za mtaa kwa mtaa, nyumba kwa
hadi nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Town School mjini Tabora, pamoja na mambo mengine alisema anazindua kampeni hiyo kwa ajili ya mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi ambapo Zito Kbwe alikabidhiwa jukumu la kuisimamia  kanda hiyo.
Aliwageukia polisi na kuwataka kukiunga mkono chama hicho ili kikifanikiwa kuingia madarakani kiweze kuwaboreshea mishahara yao kuliko ilivyo sasa akidai wanalipwa mishahara kiduchu ikilinganishwa na ugumu wa kazi yao.
“Nyie makamanda nanyi mmepigika kama sisi, sasa ninachowaomba tuungeni mkono kupambana na hawa CCM ili tuwakomboe wanyonge,” alisema Mbowe.
Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alisema Kanda ya Magharibi ina historia katika nchi kwa Mkoa wa Tabora kuwa kitovu cha mapambano ya uhuru wa nchi na Kigoma kuwa kitovu cha mapambano ya mageuzi.
Mwananchi

SHILOLE ALONGA BAADA YA KUNASWA AKILA BATA COCO BEACH NA BARNABA

MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa hakuna kinachoweza kumtenganisha na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Elius Barnabas ‘Barnaba’ kwani walikotoka ni mbali.

Shilole na Barnaba hivi karibuni walinaswa maeneo ya Coco Beach wakila bata lakini baada ya kuwaona mapaparazi wakizunguka kutafuta matukio, Barnaba alitimua mbio na kumuacha Shilole ambaye bila hiyana alitiririka: 

“Jamani mimi na Barnaba hakuna cha kututenganisha japokuwa watu wanachonga sana hata kuandikwa kwenye magazeti lakini bado tunaendelea tu, hivyo najua hakuna mtu anayeweza kututenganisha.”

PADRI AFUMANIWA NA MKE WA MTU! STORY NA PICHA KAMILI HIZI HAPA

KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu, Ijumaa Wikienda lina sakata zima.
MSHANGAO: Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!
Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.
“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.

MSAMAHA: Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.
Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe (jina tunalo) alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.
Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.
“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani."

MAGAZETI LEO JUMATATU APRIL 29, KURASA ZA MWANZO NA MWISHO ZA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.

MIAKA 13 YA LADY JAY DEE KWENYE MUZIKI KUDONDOSHA BONGE LA PARTY

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika mwaka huu 2013, Inatimia miaka13 tangu nianze kazi ya muziki.
Nashukuru MUNGU tukopamojanapia, nashukuru umma wa Tanzania kwa kuendelea ku support muziki wa Tanzania nakunipa nguvu mimi kama msanii.
Nashukuru vyombo vyotevya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya Tanzania bila kujali maslahi binafsi.
Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE, katika muziki. Na mdhamini mkuu kwa upande wa media ni East Africa TV. Shereheyamiaka 13 ya Lady Jay Dee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la NOTHING BUT THE TRUT ambayo ina jumla ya nyimbo 10.

Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za Jay Dee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.
Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.

Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu awabariki

AY Kuachia "JIPE SHAVU" Jumatano Hii ..


!!! YEEESAYAAH !!! 
Mwanamuziki kutoka Tanzania, Ambwene Yessayah a.k.a AY au pia unawweza kumuita "Zee La Commercial" anataraji kuachia ngoma yake nyingine hivi karibuni ...
AY ambae bado machoni mwako anafanya vizuri na video SPEAK WITH YA BODY, PARTY ZONE na MONEY zinazopigwa katika televisheni kubwa duniani kama Channel O na TRACE TV ya Ufaransa soon anaachia JIWE hilo litakalofahamika kama JIPE SHAVU ...
JIPE SHAVU is the next single from AY akiwa amemshirikisha mshkaji wake wa karibu akijulikana Fid Q [that Illest Hip-Hop dude from MWANZA City] ...
Hapa "Zee La Commercial" na hapa pembeni ni "Zee La Hardcore" ... JIPE SHAVU ...
Dundo hilo according to AY, limefanywa na Producer Q ikiwa ni katika studio za MPO AFRICA zilizopo maeneo ya mikocheni ...
AY anasema ngoma hiyo itaachiwa rasmi jumatano hii katika sehemu tofauti ... As to fans wakae tayari kupokea kazi nyingine bora kabisa kutoka kwake ...
AY na rapper Fid Q waliwahi kufanya ngoma mbali mbali nzuri za pamoja ikiwemo USIJARIBU yenye video yake pia ...
Let's wait for JIPE SHAVU afu tuone ...

"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER

Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo.

Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
 
“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
 
Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
 
Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.

Source: Mwananchi

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...