Tabora. Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe amemwagiza Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe
kuhakikisha chama kinapata ushindi katika majimbo mengi kwenye uchaguzi
mkuu ujao.
Mbowe alisema chama chake
kitahakikisha kinachukua majimbo ya Samwel Sitta, (Urambo Mashariki),
Ismail Aden Rage (Tabora mjini) na Jimbo la Kaliua la Profesa Juma
Kapuya, katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Mbowe alimwagiza mbunge
huyo wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kwamba majimbo hayo yanachukuliwa
na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao.
Alimtaka kufanya kampeni za mtaa kwa
mtaa, nyumba kwa
hadi nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.
hadi nyumba na mtu kwa mtu ili kuhakikisha kwamba wabunge hao wa sasa katika majimbo hayo hawachaguliwi tena na wananchi katika uchaguzi huo.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi
Town School mjini Tabora, pamoja na mambo mengine alisema anazindua
kampeni hiyo kwa ajili ya mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi ambapo Zito
Kbwe alikabidhiwa jukumu la kuisimamia kanda hiyo.
Aliwageukia polisi na kuwataka kukiunga mkono chama hicho ili
kikifanikiwa kuingia madarakani kiweze kuwaboreshea mishahara yao kuliko
ilivyo sasa akidai wanalipwa mishahara kiduchu ikilinganishwa na ugumu
wa kazi yao.
“Nyie makamanda nanyi mmepigika kama
sisi, sasa ninachowaomba tuungeni mkono kupambana na hawa CCM ili
tuwakomboe wanyonge,” alisema Mbowe.
Awali Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe alisema Kanda
ya Magharibi ina historia katika nchi kwa Mkoa wa Tabora kuwa kitovu cha
mapambano ya uhuru wa nchi na Kigoma kuwa kitovu cha mapambano ya
mageuzi.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment