Friday, November 01, 2013

YANGA SC YAIPIGA JKT 4-0


3_17e1c.jpg
Ngassa alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la umbali wa mita 20, baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki wawili wa JKT Ruvu, wakati bao la pili alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa na beki Mbuyu Twite.
Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma kwa 2-0, lakini JKT Ruvu ndiyo waliocheza soka ya kuvutia ya pasi za hapa na pale, huku Yanga wakitumia mashambulizi ya haraka kwa mabeki kupeleka mipira pembeni, ambako mawinga wanatia krosi washambuliaji wagombanie goli.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na staili yao kushambulia kutokea pembeni, huku JKT Ruvu wakionekana kuanza kupoteza mwelekeo na kutoa mwanya zaidi wa kushambuliwa.
Beki Oscar Joshua aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya pili ya kipindi cha pili, akiunganisha kona maridadi iliyochongwa na kiungo Simon Msuva.

Kona hiyo ilitokana na kazi nzuri ya kipa wa JKT Ruvu, Sadick Mecks aliyepangua shuti kali la kiungo wa Yanga, Frank Domayo.

VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI HIVI HAPA.....!!!


a_97eff.jpg
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa.
b_3754b.jpg
_ Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani).
c_5b2ab.jpg
Waandishi wa habari na maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome(hayupo pichani).
Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO)
UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU
UTANGULIZI
Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi.

MUGABE ANAWZA 'KUTUSIWA' AU KUKOSOLEWA

120927121136_mugabe_un_304x171_reuters_nocredit_35956.jpg
Mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe imebatilisha sheria inayosema kuwa ni uhalifu kumtusi Rais wa nchi.
''Viongozi wa mashitaka hawapaswi kuwa na tamaa sana ya kuwashitaki watu wanaomkosoa Rais Mugabe katika kumbi za ulevi na maeneo mengine ya kijamii,'' iliamua mahakama ya kikatiba.
Angalau watu 80 wameshitakiwa chini ya sheria hiyo katika miaka ya hivi karibuni.
Mnamo mwezi Mei, mwanaharakati Solomon Madzore alikamatwa baada ya kudaiwa kumuita Mugabe 'Punda anayechechemaa.'
Alikanusha kosa la kumtusi Rais.
Chini ya kifungu cha 33 cha sheria ya uhalifu nchini Zimbabwe, mtu anaweza kufungwa jela hadi mwaka mmoja au kutozwa faini ya dola 100 kwa kumtusi Rais.
Sheria hiyo ilipingwa na watu kadha nchini humo akiwemo mkaazi mmoja wa mji wa Bulawayo Kusini mwa nchi, Tendai Danga, aliyekamatwa miaka miwili iliyopita kwa madai ya kumtusi Mugabe wakati alipozozana na polisi ndani ya baa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Harare, Brian Hungwe, majaji tisa waliotoa uamuzi huo, walikubaliana kwa kauli moja kuwa sheria hiyo inahujumu uhuru wa kujieleza na kuifanya vigumu kwa serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wao.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilimpa waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa hadi tarehe 20 Novemba kukata rufaa.
Mwezi Agosti mahakama ilimwachilia huru mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 26 Takura Mufumisi, aliyeshitakiwa kwa kuwa na nia ya kutumia bango la karatasi lenye picha ya Mugabe kama karatasi ya kujipangusia chooni ndani ya baa moja.
Katika kura ya maamuzi iliyofanyika mwezi Machi, wananchi walipitisha katiba mpya ambayo inawapa uhuru zaidi wa kujieleza.
Watu wengi wamepongeza uamuzi wa mahakama wakiamini kuwa sheria ilikuwa imemlinda rais dhidi ya kukosolewa.

MAMA RWAKATARE ATENGWA NA MAKANISA KWASABABU YA KUFUNGISHA NDOA YA MBUNGE ALIYEOLEWA NA KIJANA MDOGO...!!!


MBUNGE wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, ametengwa katika Ushirikiano wa Makanisa baada ya kanisa lake kulalamikiwa kufungisha ndoa inayodaiwa kukiuka taratibu za kikanisa, kisheria na kimaadili, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.Ndoa inayolalamikiwa kufungishwa na kanisa hilo ni ile iliyoibuliwa na gazeti hili wiki iliyopita ambayo inamhusisha Mbunge  wa Viti Maalumu, Rosweeter Kasikila (CCM) mwenye umri wa miaka 60 na kijana Michael Christian wa miaka  26.


Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika kanisa hilo Septemba Mosi mwaka 2011, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge pamoja na majirani wanaoishi jirani na mbunge huyo mjini Bagamoyo, Pwani.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Jamii ya makanisa hayo, Mchungaji William Mwamalanga, alisema uamuzi wa kulitenga kanisa la Mama Rwakatare umetokana na kikao cha Kamati ya Maadili iliyokutana jana jijiji Dar es Salaam.

LULU MICHAEL AMWAGA MATUSI YA NGUONI KATIKA MSIBA WA BABA YAKE WEMA SEPETU....!!!


  Elizabeth Michael ‘Lulu’.

MSANII nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta akiporomosha mitusi mizito ya nguoni kwenye msiba wa baba wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu hali iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kumkodolea macho ya mshangao.Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel, Dar.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Katika tukio hilo la awali, Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa wa harambee ya kuchangia kansa ya matiti kwa akina mama iliyofanyika kwenye hoteli hiyo.
Wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya wachangiaji wote, Lulu alionekana akirudia kuchukua msosi kwa zaidi ya mara tatu (alikula sahani tatu).

TURUDI MSIBANI
Baadhi ya watu waliokuwa msibani hapo walimshangaa Lulu kwa kuporomosha matusi hayo ya nguoni wakati akijua kuwa yeye ni kioo cha jamii na baadhi ya maneno machafu aliyoyatamka hadharani hayaandikiki gazetini.

MSIKILIZE LULU
“Siwapendi nyinyi waandishi hasa wewe (akamtaja jina). ‘I don’t want your f**** story dude, go to hell with you’re f**** shit,” alisikika Lulu akitamka matusi hayo. (hatuwezi kuyatafsiri kwa sababu za kimaadili).

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...