Wednesday, March 12, 2014

JK ATANGAZA KIAMA CHA MAJANGILI

Wawakilishi wa Chama cha Uhifadhi wa Wanyama cha Frankfurt (FZS), wakikabidhi magari zaidi ya 11 kwa Rais Jakaya Kikwete Ikulu Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kusaidia vita dhidi ya ujangili wa wanyamapori katika hifadhi na mbuga za taifa.Picha na Ikulu
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imenuia kumaliza kabisa ujangili nchini, ikiwa ni hatua ya kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.
Hakusita kusisitiza kwamba, nia ya dhati ya Serikali ni kuhakikisha mkakati huo unakamilika, japokuwa kumekuwa na changamoto zinazotokana na ukubwa wa hifadhi hizo na uhaba wa vitendea kazi pamoja na askari wa wanyamapori.
Akizungumza wakati wa kupokea magari 11 ya kisasa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kupambana na ujangili kutoka kwa Shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la Ujerumani, Kikwete alisema tatizo hilo limekuwa la muda mrefu, lakini juhudi za kulikomesha zinafanyika.
Alisema, pamoja na ukubwa wa tatizo hilo, bado kuna tatizo la uhaba mkubwa wa wafanyakazi wanaotakiwa kudhibiti majangili, ambapo kwa sasa kuna wafanyakazi 1,155 sawa na asilimia 24 tu ya mahitaji halisi ya wafanyakazi 4,000 wanaohitajika.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

HII NDIO VIDEO YA AJALI YA NDEGE KUMGONGA MTU, MAAJABU...!!!

Screen Shot 2014-03-11 at 4.58.21 PM
Screen Shot 2014-03-11 at 4.57.11 PM
Hii imetokea Florida Marekani ambapo mtu mmoja alikua anaruka akiwa na Parachuti lakini akakutana na ndege hii ndogo ambayo baada ya kumgonga walianguka chini wote huku ndege ikiangukia pua.
Pamoja na ajali hii, hakuna mtu aliepoteza maisha ila wote walipata majeraha madogomadogo baada ya kuanguka kwenye umbali wa futi 75 na wakapelekwa hospitali ambapo mwenye Parachuti John Frost (49) aliruhusiwa kuondoka.
Hili tukio limenaswa jinsi lilivyotokea kwa sababu kulikua na mpiga picha aliekua na camera karibu na alikua anashuhudia kila kitu.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO MARCHI 12, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

KURA BADO KITENDAWILI BUNGE LA KATIBA

Wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakipitisha Rasimu ya Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa mvutano wa takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38 kinachoeleza aina ya kura kati ya wazi na ya siri.
Hata hivyo, wajumbe wawili wa Bunge hilo, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Felix Mkosamali wa NCCR- Mageuzi walisusia kupitisha azimio la kukubali Kanuni za Bunge hilo, wakidai kusalitiwa katika uamuzi huo na wenzao walioko kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wajumbe na viongozi mbalimbali wa vyama vyenye ushawishi bungeni, kwa pamoja waliridhia na kulegeza misimamo yao ili upatikane mwafaka wa kutengeneza Katiba Mpya ndani ya wakati. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

RIDHIWANI, "SIKUSHINIKIZWA KUGOMBEA"

RidhiwaniKikwete_11ac5.jpg
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete ameahidi kuwa atajitahidi kutatua kero za maji, umeme na ajira kwa vijana. Alisema hayo jana baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Bagamoyo, Shija Andrew.
Leo anatarajia kurudisha fomu hiyo. Ridhiwani alipokuwa akienda kuchukua fomu hiyo, alisindikizwa na mamia ya wanachama wa CCM wa majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, wakiwa wanaimba na kucheza kumshangilia mgombea huyo.
Baada ya kuchukua fomu kutoka kwa Ridhiwani alimhakikishia ofisa huyo kuwa atazingatia taratibu zote za uchaguzi na kutoendesha kampeni za matusi na vurugu.
Baada ya kuchukua fomu hiyo na nakala nyingine muhimu za uchaguzi, aliongozana tena na mamia ya wafuasi wake, kuelekea kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Bagamoyo, ambapo alizungumza na waandishi wa habari.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

WAZIRI MKUU WA LIBYA AZUIWAKUSAFIRI


Kiongozi wa mashtaka Nchini Libya Abdel-al-Qader Radwan amemzuia Waziri mkuu wa taifa hilo aliyevuliwa madaraka, Ali Zeidan, kusafiri nje ya taifa hilo hadi pale uchunguzi dhidi yake utakapokamilika.
Anatuhumiwa kwa madai ya ubathirifu wa pesa za umma.
Bwana Zeidan amesimamishwa kazi mapema siku ya Jumanne na Bunge la taifa hilo, baada ya Wabunge kudai kuwa meli ya mzigo ya Korea Kaskazini iliyokuwa imezuiliwa baada ya kunaswa ikibeba mafuta ghafi toka bandari moja linalokaliwa na waasi huko Libya, ilivunja nanga na kusafiri baharini.
Kura ya kutokuwa na imani na Bwana Zeidan iliitishwa baada ya meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Korea Kaskazini kuabiri na kufikia maji makuu ya mipaka ya kimataifa baharini.
Mafuta hayo yalikuwa yamenunuliwa kutoka kwa waasi wanaodhibiti bandari ya Al- Sidra.

Wabunge hawana imani na Waziri Mkuu

Bunge la Libya limemuachisha kazi Waziri huyo mkuu, baada ya kupitisha agizo la kutokuwa na imani naye.
Hilo limeafikiwa baada ya meli ya Korea Kaskazini kuingia katika bandari ya taifa hilo na kuondoka na mafuta ghafi bila idhini ya serikali.
Makundi ya wapiganaji yamekuwa yakidhibiti baadhi ya bandari ya taifa hilo mashariki mwa taifa, tangu Julai mwaka jana na kuuza mafuta nje ya taifa.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...