Tuesday, November 19, 2013

KIWANDA CHA KUTENGENEZA VIYWAJI VIKALI CHAFUNGWA SHINYANGA

Kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Trully African kilichopo Mtanda Manispaa ya Shinyanga kimefungwa na Halmashauri ya mji huo kwa kutokidhi viwango vya ubora.... mengi kuhusu sakata hili endelea kusikiliza radio Faraja Fm na kutembelea mtanda huu wa jambotz8.blogspot.com.

Story na Steve Kanyeph na Isaac Edward Kisesa

MWANAFUNZI ANAYEDAI KUBAKWA NA KAPUYA HUYU HAPA AWEKEWA MTEGO NA KUBAINI MAMBO MAZITO

Denti anayedai kubakwa na Prof Kapuya akiongea na GPL.

MNYONGE mnyongeni haki yake mpeni, skandali ya kumbaka na kumwambukiza Ukimwi mwanafunzi, inamtafuna na kumuumiza Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya.
Kuhusu ukweli wa skendo hiyo, vyombo vya sheria vitazungumza lakini gazeti hili limejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa denti husika ni tapeli na anacheza rafu ili kumharibia Kapuya kwa maslahi yake.
Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya.
Gazeti hili, liliamua kumchunguza denti husika ili kumjua kiundani katika kutimiza ahadi ambayo Global Publishers Ltd, ilishaitoa kwenye Gazeti la Risasi, nakala ya Jumamosi iliyopita kuwa waandishi wake watafuatilia kinagaubaga na kuanika kila kitu kupitia magazeti yake, utekelezaji unaendelea.

JAMAA AUWA WAWILI NA KISHA KUJIUA YEYE MWENYEWE ILALA DAR LEO ASUBUHI

Mtu mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake amewaua watu wawili kwa kuwapiga risasi ndani ya gari na kujeruhi mmoja kisha naye akajiua kwa risasi asubuhi hii jirani na Baa ya Wazee iliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam!

Inadaiwa kuna gari ilikua inatoka ndani ya geti kutoka ikiwa na dereva mwanaume, abiria mwanamke mbele, na abiria wengine wawili wakiwa seat ya nyuma.

Pembeni hapo kulikua na jamaa kasimama. Inadaiwa alishushwa hapo dakika chache toka katika tax, walipotokeza abiria hao kupitia gari yao alitoa silaha yake na kupiga risasi gari akilenga zaidi abiria wa mbele pande zote kisha na nyuma. Baada ya kumaliza hapo muuaji huyo naye alijipiga risasi na kufariki hapo hapo.

Dereva na abiria wake wa mbele wamefariki dunia, huku abiria wa nyuma mmoja mama mtu mzima kajeruhiwa na risasi mgongoni na dada mwingine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.

Source: global publishers & Jamii Forums

WACHUNGAJI WAMKALIA KOONI MZEE WA UPAKO KUHUSU RAMBI RAMBI YA MAREHEMU MOSES KULOLA

WACHUNGAJI wa makanisa mbalimbali nchini wamemkalia kooni Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Antony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako, kwa kumtaka atoe rambirambi aliyoahidi mbele ya umati wa watu siku ya kuaga mwili wa marehemu Askofu Moses Kulola Temeke, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mtu wa kamati iliyoratibu mazishi ya kiongozi huyo wa kanisa, viongozi wote wa dini walioahidi kutoa rambirambi hizo wametoa isipokuwa Lusekelo aliyeahidi kwa mbwembwe kutoa shilingi milioni 15.
Katibu Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Mchungaji David Mwasota alisema anamheshimu Lusekelo kwani ni mtumishi wa Mungu, lakini ni bora angetimiza ahadi yake kama walivyofanya wenzake.

“Mzee wa Upako ni mtu mwenye jina kubwa kwenye jamii na kwa Mungu, hivyo anapaswa kuangalia kwa undani kile anachoahidi kwa muda unaotakiwa na amuache mke wa marehemu apumzike kwa kuwa ametokwa na mpendwa wake na bado hana nguvu,” alisema na kuongeza;

MAGAZETI YA LEO JUMANNE NOVEMBA 19, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

KAGAME, MUSEVENI NA KENYATTA WASHTAKIWA KORTI YA JUMUIYA

kagamepx_deab7.jpg
Serikali za Rwanda, Uganda, Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, zimefunguliwa kesi katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki, zikidaiwa kukiuka mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Hatua hiyo inatokana na Serikali hizo kufanya vikao vitatu mfululizo na kuzitenga nchi za Tanzania na Burundi.
Walalamikaji katika kesi hiyo, ni Ally Msangi, David Makata na , John Adam, ambao ni Watanzania, wanaotetewa na wakili Mwandamizi, Jimm Obedi wa jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walalamikaji wamewaomba majaji katika mahakama hiyo, kutoa tamko la kusitisha utekelezaji wa maazimio yote ya vikao vya wakuu wa nchi hizo tatu.
Pia wameomba majaji watoe tamko la kukomesha kurejewa kwa vikao kama hivyo kinyume cha mkataba wa jumuiya hiyo.
Kesi hiyo ya aina yake, ilifunguliwa jana katika Mahakama ya Afrika ya Mashariki na kupokewa na Ofisa Masijala i katika mahakama hiyo, Boniface Ogoti.
Kufunguliwa kwa kesi hiyo, kunakuja siku kadhaa baada ya Rais Jakaya Kikwete kuzilalamikia nchi hizo, kuhusu kuitenga Tanzania kwa kufanya mikutano mbalimbali ya maendeleo ya nchi zao. Nchi nyingine iliyotengwa ni Burundi.
Kikao cha kwanza cha pamoja kilifanyika Aprili mjini Arusha kabla viongozi hao kukutana Juni 25 na 26 jijini Entebbe nchini Uganda, walidai kuwa na nia moja ya kurahisha mawasiliano katika nchi hizo.
Mkutano mwilingine ulifanyika mjini Kigali Rwanda Oktoba 28 ukiwajumuisha Rais Yoweri Museven wa Uganda, Uhuru Kenyatta (Kenya), Salva Kiir (Sudan Kusini) na Paul Kagame.
Wakili wa walalamikaji Obedi, alisema katika kesi ya msingi, wanawashtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Rwanda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Uganda,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Kenya na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...