Friday, December 05, 2014

AJIFUNGUA MTOTO MWENYE SURA YA CHURA...!!!

       Kitanda cha Upasuaji.         MKAZI wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nusu ya sura yake inafanana na binadamu na nusu ikifanana na chura.
Mtoto huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Mtakatifu Luka kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mpwapwa. Alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa. 

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Edwin Kihura mara baada ya mama huyo kufika katika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu ambao haukuwa na kikomo, lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida licha ya njia ya uzazi kufunguka. 

Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

CAG MPYA ATAKA WANASIASA WAHESHIMU OFISI YAKE

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad (pichani) aliyeapishwa juzi na Rais Jakaya Kikwete amekemea tabia ya wanasiasa na wafanyabiashara kuingilia kazi za kitaaluma, akisema kwa upande wake hatapenda kuona watu wa makundi hayo wakifanya hivyo na kusisitiza kuwa, kufanya hivyo ni kosa.

Aliyasema hayo jana mbele ya waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kila mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), jijini hapa.
Alisema ofisi ya CAG na watendaji wengine watafanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi, huku akiendelea kusisitiza wanasiasa na wafanyabishara kila mmoja aheshimu taaluma ya ukaguzi wa hesabu za serikali kwa faida ya nchi.
Alifafanua kuwa iwapo kila mmoja atawajibika katika nafasi yake na kuaminiana katika shughuli za kila siku, kamwe hakutakuwa na matatizo yoyote.
‘’Matatizo ya watu binafsi yasichanganywe na shughuli za kila siku za ofisi ya CAG na wale wenye kufanya siasa na biashara pia wawajibike katika nafasi zao na ofisi yangu itafanya mambo kwa kufuata Katiba ya nchi inavyoelekeza, na sio vinginevyo,” alisema Profesa Assad aliyekabidhiwa mikoba ya Ludovick Utouh aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.
Alitumia fursa hiyo kuwaasa wahasibu na wakaguzi, akisema wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa na kiwango cha hali ya juu ili taaluma yao iweze kuheshimika nchini. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

IPTL YAZUA KIZAAZAA MAHAKAMANI

Kampuni za Pan Africa Power Solution Tanzania Limited (PAP) na Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), zimewasilisha maombi ya kutaka Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) akamatwe kwa kukiuka amri ya Bodi ya Rufaa za Kodi (TRAB) kwa kufuta Hati za Malipo ya Kodi za Mauzo ya Hisa (Capital Gain Certificate).
Kampuni hizo mbili, ambazo ziko kwenye mgogoro wa umiliki, ndizo zinahusika kwenye sakata la uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyofunguliwa kuhifadhi fedha za malipo ya tozo ya kuuza umeme unaofuliwa na IPTL, kwa Shirika la Umeme (Tanesco), wakati wa kusubiri uamuzi wa mahakama katika kesi ya kupinga tozo hilo.
PAP, ambayo inadai imenunua hisa zote za IPTL, ndiyo iliyolipwa fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti hiyo na kuamsha mjadala mkubwa bungeni ulioisha kwa Bunge kufikia uamuzi wa kuwawajibisha kisheria wote waliohusika, wakiwemo mawaziri. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NAULI MPYA ZA MABASI YAENDAYO MIKOANI

Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Dk Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es salaam jana juu ya hali ya usafiri kipindi cha siku kuu za Krismas na mwaka mpya ambapo ametahadharishja abiria kuto kukubali kutozwa nauri za juu na pindi ikitokea hivyo Sumatra ipewe taarifa haraka.



 
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 05, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAHAKAMA YA TANZANIA SASA KUONYESHA LIVE KESI WAKATI ZIKIENDELEA KATIKA TELEVISHENI NA REDIO.


http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2141854/lowRes/662002/-/o2ggkjz/-/chande+clip.jpg







Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman 

MAHAKAMA inaangalia uwezekano wa kuruhusu vyombo vya habari kurekodi picha na sauti kuwezesha vituo vya radio na televisheni kuripoti habari za mahakama wakati kesi zinaendelea. 

Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alisema jana mahakama inajifunza kutoka kwa nchi zinazoruhusu vituo vya redio na televisheni kurekodi na kuripoti habari wakati kesi zinaendelea. 

Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana wakati wa mkutano baina ya Baraza la Vyombo vya Habari na Mahakama uliofanyika jijini Dar es Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MUGABE ASEMA HANG'OKI MADARAKANI..!!!

Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani. 
 
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Mugabe ameahidi kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe
Hasira ya Mugabe ilionekana kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua yanayodaiwa kuandaliwa na naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAREKANI: TULIPANGA KUMWOKOA SOMERS

Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen
Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen.
Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.
"Kwa masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine walikuwepo na waliokolewa," Baraza la Usalama la Taifa, limesema.
Mtu anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013, ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba msaada.
Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen akitishia kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa, yatakapotimizwa.
Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33, alifanyakazi kama mwandishi wa habari na mpiga picha wa mashirika ya huko na kazi zake zikaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa, ukiwemo mtandao wa BBC. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...