Friday, December 05, 2014

MAREKANI: TULIPANGA KUMWOKOA SOMERS

Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen
Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen.
Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.
"Kwa masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine walikuwepo na waliokolewa," Baraza la Usalama la Taifa, limesema.
Mtu anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013, ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba msaada.
Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen akitishia kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa, yatakapotimizwa.
Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33, alifanyakazi kama mwandishi wa habari na mpiga picha wa mashirika ya huko na kazi zake zikaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa, ukiwemo mtandao wa BBC. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...