Friday, December 05, 2014

MUGABE ASEMA HANG'OKI MADARAKANI..!!!

Rais Robert Mugabe awalaumu baadhi ya wapinzani wake ndani ya chama cha ZANU PF kwa kupanga kumuondoa mamlakani. 
 
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake tawala cha ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza katika kongamano la chama hicho, Mugabe amesema amebaini kuwepo majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi, lakini akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Mugabe ameahidi kupambana na rushwa ndani ya chama na kukabiliana na maafisa wa chama hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea rushwa.
Wanachama wengi wa chama hicho wangali ni wafuasi sugu wa Rais Mugabe
Hasira ya Mugabe ilionekana kufuatia madai ya njama ya kutaka kumuua yanayodaiwa kuandaliwa na naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo Mujuru alikanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Maelfu ya wajumbe wa chama walihudhuria kongamano hilo mjini Harare
Chama tawala cha Zimbabwe kinakumbwa na vita vya ndani kwa ndani kuhusiana na nani atarithi nafasi ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na ambaye ameongoza tangu uhuru wa taifa hilo.Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi.
Hivi karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala, Robert Gumbo aliiambia BBC kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama tawala na kukifanya kama mali yake binafsi.
Bi Joyce Mujuru amedaiwa kupanga njama ya kumuua Mugabe ili achukue mamlaka kutokla kwake.
Gumbo alisema lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace.Bi Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama mtu ambaye anechukua usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...