Thursday, March 07, 2013

TATOO YAMPONZA MONALISA




SIRI ya kuvunjika kwa ndoa ya staa wa filamu Bongo, Yvonny Cherry ‘Monalisa’ imevuja ambapo imeelezwa kuwa tattoo aliyokuwa ameichora mkononi mwake yenye alama ya kopa na mshale ndiyo chanzo.
Akizungumza na Tollywood Newz jijini Dar es Salaam, Monalisa alisema: “Sikuwahi kuwaza hili hata mara moja. Siku moja Kanisani, Mchungaji aliniambia kwamba tattoo yangu ndiyo chanzo cha kunivurugia uhusiano wangu.

“Aliniambia kwamba, alama ya kopa ambayo humaanisha moyo – upendo, halafu mshale kupita katikati yake, humaanisha maumivu na kuteswa katika uhusiano. Lilikuwa jambo jipya kwangu lakini niliamua kufuta haraka sana na sasa nimeweka nyingine ya ua rose.”Source:Globalpublishers

Prof. Maghembe alichefua kanisa

WAZIRI wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, amelaumiwa na uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa kwa kushindwa kuingilia kati mgogoro wa maji uliopo kati ya mwekezaji wa mashamba ya mpunga Mbarali na Shule ya Sekondari ya Kilimo ya Montfort ambayo inauziwa 
maji ili kuweza kulima. 

Kuibuliwa kwa tuhuma hizo zilizoelekezwa moja kwa moja kwa Waziri Maghembe kunafuatia barua kadhaa zilizoandikwa kwenda wizarani na uongozi wa kanisa hilo na ule wa shule hiyo pasipo kujibiwa na serikali licha ya uwekezaji wa kanisa ulilenga zaidi kuwaendeleza vijana. 

“Bado tunaumizwa sana na suala la maji, tumeipigia sana magoti serikali ili itusaidie tupate maji ya kutosha. Shule yetu ni ya mchepuo wa kilimo, ilisajiliwa tukijua kuwa tutalima kwa vitendo baada ya kujiridhisha kuwa maji yapo, tangu apewe mwekezaji ameamua kutuuzia maji,” alilalamika Mkuu wa Shule hiyo, Ansgar Kigane. 


Kigane alisema kuwa tangu shule hiyo ilipoanzishwa miaka 25 sasa imefanya vizuri sana kwenye masomo ya kilimo kutokana na upatikanaji wa maji uliokuwa ukitolewa na Shirika la Kilimo na Chakula (NAFCO) kabla ya kubinafsishwa. 



“Kwa kuwa shule yetu ni ya kilimo hasa mpunga na kwa kuwa wanafunzi waliweza kulima na kupata mavuno ya kutosha ilikuwa rahisi kwao kupata chakula bure shuleni, sasa hali imekuwa ngumu, mwaka huu imebidi tununue maji kutoka kwa mwekezaji kwa masharti magumu,” alisema. 


Alibainisha kuwa licha ya jitihada kubwa za kuiomba Wizara ya Maji iingilie kati ili kuona uwezekano wa shule hiyo kupata maji kwa kupitia mfereji mdogo ulioruhusiwa wakati wa NAFCO, lakini wamekosa majibu sahihi. 


Ofisa Maji Mkuu wa Bonde la Rufiji ambao ndio wenye mamlaka ya kusimamia maji katika Bonde la Usangu, Idrissa Msuya alisema kwa mujibu wa sheria ya maji, mwekezaji aliyepewa kibali cha kuyatumia haruhusiwi kuyauza na kwamba makubaliano yaliyofikiwa ni uamuzi wa pande mbili ambazo haziihusu mamlaka hiyo. 


Msuya alisema kuwa mvutano huo wa maji umefumuka baada ya serikali kubinafsisha mashamba ya NAFCO kwani huko nyuma hali haikuwa hivyo na kwamba mamlaka hiyo imejitahidi kwa kiasi kikubwa kuleta suluhu ila anashangaa kwanini hawakubaliani. 


Askofu wa Jimbo Katoliki la Iringa, Tarcisius Ngalalekumtwa, katika barua zake amekuwa akifanya jitihada kubwa za kuipigia magoti serikali ili iweze kuiruhusu shule hiyo ipewe kibali cha kutumia maji kutoka kwenye mfereji wa umma uliojengwa na serikali. 


SOURCE::TANZANIA DAIMA::

SNURA ANASWA NA NJEMBA

POZI la staa wa sinema Bongo, Snura Mushi na Dj Ommy Crazy wa Maisha Club kama walivyonaswa na kamera ya Tollywood Newz linatoa ishara kwamba ni wapenzi.
 Fukuafukua za kitaani zinaeleza kuwa wawili hao ni wapenzi lakini Snura anafanya siri ili mpenzi wake huyo asiporwe na wajanja.Snura alipoulizwa uhusiano wake na Dj huyo alisema: “Jamani Ommy ni mtu wangu wa karibu...kama ni suala la picha, napiga na watu wangapi jamani? Kwa nini iwe kwa Ommy tu?”

BARUA YA MWANAFUNZI ALIEMALIZA FORM 4 2012 KWA WIZARA YA ELIMU






Pliz my name is MKUWA RAJAB I am finish fom for. Ze everybody is to say we get za divishen 0, My part I am saying not I am not get divshen 0. I am vere vere intelijens, but pipoz don’t like me.

I have experience in singing bongoflava, so pipoz are jelas, the have put ...majik so I get diveshen 0. But I am clever becoz ask me forekzampo, what is fomula for water? Ze fomula for water iz Hech to O.

Now why you give me dishen 0? Ok ask me anadha forekzampo what iz President of America? Ze president of America iz Obama. Ze gavament shud change my marks to dishen 2, because the youth are ze future of my country.

If we get divishen 0 zen all the future is divishen 0. So giv us more maks becoz of ze future. Pliz mzee put on ze yua fb wall so ze Plezident will see.......
Kwa mantiki hii, tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu nchini kimesababishwa na wanafunzi wenyewe? Au Wazazi? Ama Waalimu? au mitaala ya kufundishia? Piga kura yako upande wa kulia kwenye poll vote side .... Tutabaini tatizo lipo wapi. ....

Kwa hisani ya James Pricenn Brighton

WAUGUZI MOROGORO WAPOKEZANA KUWASHIKIA DRIPU WAGONJWA BAADA YA KUKOSA VITANDA



BAADHI ya wananchi wa mkoani  MOROGORO  wameshangaza na kitendo cha waunguzi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro,kupokezana kuwashika madripu ya dawa wagonjwa waliolaza chini ya wodi za hospital hiyo ya rufaa nya mkoa wa Morogoro baada ya kukosa vitanda.
 .
Skendo zinazidi kuiandama hospital hiyo ambayo imepandishwa hadhi ya kuwa hospital ya rufaa hivi karibuni ambapo ljumaa iliyopita mtangazaji wa Top redio ya mkoani hapa Edward Abed Mganga aliyevamiwa na majambazi na kukimwizwa kwenye hospital hiyo imeilalamikia hospital hiyo kwakumtelekeza bila kumpa huduma kwa zaidi ya masaa matano na kuladhimika kuondoka kwenye hospital hiyo ya serikali na kwenda kutibiwa hospital za watu binafsi. 


Mtandao huu umeibua Skendo nyingine ndani ya hospital hiyo baada ya kushuhudia waunguzi wa hospital hiyo wakipokeza kuwashikia  madripu ya dawa wagonjwa waliolazwa chini ya sakafu baada ya hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha. 
Juzikati hospital hiyo ilivamiwa na majeruhi zaidi ya 60 waliopoteza fahamu baada ya kiwanda  cha kutengeza nguo za michezo cha Mazava kukumbwa na shoti ya umeme na kukimbizwa kwenye hospital hiyo,hivyo uongozi wa hospital hiyo baada ya kuelemewa na wingi wa majeruhi hao ulilazimia kutoa magodoro stoo na kuwalaza chini baadhi ya majeruhi hao kufuatia hospital hiyo kukosa wodi na vitanda vya kutosha.

 " Hii ni aibu kubwa kwa hospitali ya rufaa ya mkoa kuwalaza chini wagonjwa hata kama wakijitetea kwamba wagonjwa wamekuja kwa mkupo. hospital inapopewa hadhi ya rufaa inamaana inamudu kukabiliana na majanga yoyote kwa maana wa kuhudumua majeruhi zaidi ya mia watakaofika kwa mkupuo kwenye hospital hiyo"alisema Bi Asha Abdallah aliyekuwepo ndani ya wodi namba 3 walipolazwa majeruhi hao. 

Vile vile mwandishi wa matandao huu mbali ya kushudia wauguzi hao wakipokezana kuwashikia madripu wagonjwa hao pia walishuhudia wahudumu hao wakilazimika kupita juu ya wagonjwa waliolazwa kwenye eneo la njia za wodi hizo  
Ili kupata ufafanuzi wa jambo hilo Mtandao huu ulimsaka Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo kwa zaidi ya siku tano na kufanikiwa kumpata leo asubuhi ambapo alipotakiwa kueleza hali hiyo Mganga huyo mfawidhi Bi Rita Lyamuya alikuwa na haya ya kusema 
" Nikweli siku ile ya tukio la kiwanda cha Mazava tulitoa magodolo stoo na kuwatandikia chini baadhi ya majeruhi .kiukweli kwa ishu kama ile tulikosa namna ya kukabiliana  nayo kwani walikuja kwa mkupua zaidi ya majeruhi 65 hivyo tulichofanya tuliwapokea na baadhi kuwalaza chini na kuwapatia hudumu ya kwanza huku tukitafuta sehemu muafaka ya kuwalaza"alisema Dr Rita
dustanshekidele blog

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WILAYANI MBEYA VIJIJINI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA UKOSEFU WA VYOO

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WAKIWA DARASANI HUKU DAWATI MOJA WAKIWA WAMEKALIA WANAFUNZI WATANO
HIVI NDIVYO VYOO VYA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WANAFUNZI WA SHULE HIYO AMBAO NI ZAIDI YA 700 WAMESHINDWA KUTUMIA VYOO HIVYO KWA KUOGOPA USALAMA WA VYOO HIVYO NI MDOGO KWANI HAVIJAJENGWA KWA UIMARA UNAOTAKIWA
HII NDIYO HALI HALISI YA VYOO HIVYO KWAKWELI NI HATARI KABISA VIPI WAHUSIKA MPOOO NA MNALIONA HILI?
HIVI NI VYOO VYA WAALIMU WA SHULE HIYO
WANAFUNZI SASA HUJISAIDIA KATIKA VICHAKA HIVI KWAKWELI HATARI SANA KUKUTANA NA NYOKA NA WADUDU WENYE SUMU KALI 



PICHA NA KAMANGA  MBEYA

CHADEMA WAZUA GHASIA MAZISHI YA MOLLEL

Wafuasi wa Chadema, wameibua tafrani ya aina yake wakati wa mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), marehemu Benson Mollel baada ya kung’oa bendera za chama hicho na kuamsha hasira za 
waombolezaji wafuasi wa chama tawala. 

Mollel alikutwa amefariki mwanzoni mwa wiki, katika Hoteli ya Lush Garden Business, Mtaa wa Jacaranda Arusha huku mwili wake ukiwa mtupu.Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana na baadhi ya makada wa CCM walionekana wakiwasaka wafuasi hao wa Chadema. 

Mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea saa 8:30 usiku na baadhi ya wafuasi wanaosadikika kutoka Chadema walichukizwa na kuwapo kwa bendera hizo msibani na hivyo kuanza kuzing’oa.

Matatizo ya mitambo ya uchaguzi Kenya

 
Shughuli ya kuhesabu kura katika mojawapo ya vituo vya kupigia kura nchini Kenya
 
Shughuli ya kuhesabu kura za uchaguzi wa urais nchini Kenya, ilisimamishwa usiku kucha kwa sababu ya hitilafu za mitambo ya tume huru ya uchaguzi na mipaka iliyokuwa inatumika kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa Kenya.
Maafisa wa tume hiyo, wamelazimika kusafiri kwa barabara kutoka umbali wa maelfu ya kilomita ili kwenda katika kituo cha kutangazia matokeo ya kura za urais mjini Nairobi kuwasilisha fumo zao za matokeo.
Mfumo wa Elektroniki, tayari umekosolewa vikali kwa kusababisha kuharibika kwa kura nyingi, zikikisiwa kuwa zaidi la laki tatu.
Maafisa wa uchaguzi wametoa wito wa utulivu na amani kwa wakenya wakati tume ikiendelea kutatua tatizo la kura.
Naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta,ambaye anatakikana na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu, wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya, miaka mitano iliyopita, angalia yuko mbele katika matokeo ya uchaguzi wa urais.
Kufikia sasa asilimia 42 ya kura za urais nchini Kenya zimehesabiwa na kuwasilishwa rasmi kwa tume ya uchaguzi IEBC kupitia mitambo ya electroniki.
Hata hivyo kumekuwepo malalamishi kuhusu kucheleweshwa kwa shughuli ya kujumlisha kura kutokana na hitilafu ya mitambo.
Uhuru Kenyatta, anayekabiliwa na kesi katika mahakama ya uhalifu wa kivita ICC, angali anashikilia uongozi huku kura za urais zikiwa bado zinahesabiwa.
Huu ni uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika tangu ghasia za baada ya mwaka 2007/2008 kufuatia matokeo yaliyozua utata.
Kenyatta aliendelea kuwa mbele kwa hesabu ya matokeo ya mwanzo dhidi ya mpinzani wake waziri mkuu Raila Odinga katika siku ya pili ya shughuli ya kuhesabu kura zaidi ya masaa 36 baada ya shughili ya upigaji kura kukamilika.
Hadi sasa Uhuru ana kura milioni mbili nukta nane wakati Raila Odinga akiwa na kura milioni mbilii nukta mbili
Raila Odinga alidai kuibiwa ushindi wake mwaka 2007 wakati matokeo yalizua ghasia na kusababisha vifo vya watu zaidi ya laki moja huku maelfu wakiachwa bila makao
Wakati mamilioni ya wakenya walijitokeza kupiga kura kwa amani siku ya Jumatatu,watavyopokea matokeo ya mwisho ya kura ndio itakuwa ishara ya uthabiti wa nchi hiyo.
Ni asilimia arobaini na moja ya kura zilizohesabiwa huku kukiwa na vituo zaidi ya elfu thelathini ambako kura zilipigiwa.
Ni zaidi ya kura milioni tano zilizohesabiwa kutoka kwa wapiga kura milioni 14.3 waliokuwa wamesajiliwa.

UN, ''Mauaji ya Albino yaongezeka Tanzania''


Navi Pillay ansema Albino wana haki ya kuishi kama watu wengine
Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa,Navi Pillay, amelaani mashambulizi mabaya yaliyofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino nchini Tanzania ikiwemo mauaji ya mtoto mvulana.
Serikali inapaswa kukomesha mauaji hayo pamoja na unyanyapaa dhidi yao , alisema Bi Pillay.
Muaji ya kinyama yanayofanyiwa watu hao huhusishwa na ushirikina , kulingana na UN.
Watu watano pekee wameshtakiwa mahakamani nchini Tanzania, tangu mwaka 2000 kwa mauaji ya maalbino.
Takriban wengine 72 waliuawa katika kipindi hicho.
Mnamo mwaka 2009, rais Jakaya Kiwete, alisema kuwa mauaji hayo yaliiletea Tanzania aibu kubwa na kulazimu nchi hiyo kufanya kampeini ya kitaifa ili kukomesha dhulma hizo dhidi ya maalbino.
Mnamo mwaka 2010, Salum Khalfani alikuwa mtu wa kwanza mwenye ulemavu huo kuchaguliwa kama mbunge nchini Tanzania.
Bi Pillay alisema kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wana haki ya kuishi kama mtu yeyote ule bila hofu ya kuuawa au kubaguliwa.
Katika taarifa yake, Bi Pillay alisema kuwa mashambulizi manne ya watanzania wenye ulemavu wa ngozi, yaliripotiwa katika siku kumi na sita kati ya mwezi Januari na Februari.
Ni pamoja na mauaji ya mtoto mwenye miaka saba, Lugolola Bunzari. Watu walimvamia walikata paja la uso, mkono wake wa kulia , bega la kushoto.
Babu ya kijana huyo, mwenye umri wa miaka 95, pia aliuawa kwenye shambulizi hilo, alipojaribu kumuokoa mjuu wake.
Bi Pillay alisema mashambulizi kama haya ni mabaya na watu wana haki ya kuishi kama watu wengine bila hofu ya kuuawa au kujeruhiwa vibaya.

NSSF YABISHA HODI KIGOMA VIJIJINI


 Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akiwasili katika Kijiji cha Matyazo wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. 
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kigoma Vijijini, Hamis Betese akizungumza wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. 
Baadhi ya wanakijiji cha Matyazo pamoja na vijiji vya jirani wakiwa katika uzinduzi huo.
Kikundi cha ngoma za kitamaduni cha Changamoto kikitoa burudani.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha kwa hiari kwa wanachama wa NSSF, wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. Zaidi ya Wanachama 500 wameandishwa Uanachama wa Hiari wa NSSF katika Kata ya Kalinzi.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Ramadhani Maneno akizungumza wakati wa Uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akizungumz wakati wa uzinduzi wa kujiandikisha uanachama wa NSSF wa Hiari kwa wakulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO Kigoma Vijijini. 
Wanakijiji wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wakazi wa vijiji vya Matyazo, Rusaba na Makabogo wakiwa katika hafla hiyo.
Meneja Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Mseli Abdalah akiongoza hafla hiyo.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kigoma, James Mashinga akizungumza wakati wa uzinduzi.
Kikundi cha Ngoma cha Changamoto kikitoa burudani.



Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akimkabidhi kadi ya Uanachama wa hiari wa NSSF mkulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO, Mary Wilfred wakati wa hala iliyofanyika Kogoma Vijijini.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akimkabidhi kadi ya Uanachama wa hiari wa NSSF mkulima wa Kahawa wa Ushirika wa RUMAKO, Meckrinda Enock wakati wa hala iliyofanyika Kogoma Vijijini.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kigoma, James Mashinga akipokea zawadi ya Kahawa kutoka kwa Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga  akipokea zawadi ya Kahawa kutoka kwa Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa
Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Meneja Kiongozi, Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akifurahia zawadi ya Kahawa mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Ushirika wa RUMAKO, Omari Mahwisa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...