Friday, May 09, 2014

JAQUELINE WOLPER AFUNGUKA KUHUSU KUBADILI DINI, KUCHANA, USAGAJI

Screen Shot 2014-05-09 at 7.02.35 AM 
Ni longtime mwigizaji Mtanzania Jaqueline Wolper amekua kimya na hajasikika akiyatoa ya moyoni kuhusu yote yaliyompata kwenye miezi iliyopita na kumfanya amiliki sana headlines za magazeti, blogs, website pia facebook na twitter huku wengi wakiwa na hamu ya kusikia akiyaongelea.
Kwenye Exclusive interview na mtangazaji Sporah wa The Sporah show, Jaq amekanusha kwamba yeye ni msagaji japo mara kadhaa ameonekana akivaa kiume na kusisitiza ‘sasa hivi nimepunguza sana kuvaa nguo za kiume, wengi walikua wanahisi lakini sijawahi kufanya vitendo vya usagaji na wala sijawahi kushawishiwa na mtu anaejihusisha na vitendo hivyo, boyfriend wangu hana tatizo na mavazi ya kiume ninayovaa… hatujawahi kupangiana mavazi’
Kwenye jibu jingine alilotoa J anasema ‘sijaolewa na wala sijawahi kuolewa, nilishawahi kubadili dini kweli… ni vitu vinatokea na usimuhukumu mtu bila kumuuliza’
Sporah: Ni kweli kwamba ulikutana na mtu ana uwezo wa kifedha na kulikua kuna vitu unataka akununulie akasema hawezi kukufanyia mpaka ubadilishe dini ili upate hizo mali?
J Wolper: ‘Sio hivyo, dini nilikuja kubadilisha wakati nimeshapata mali, nilibadilisha mwishoni kabisa baada ya huyu mwanaume kuja kwetu akitaka kunioa, alinipa mali na vitu vya thamani kabla ya sisi kukutana, unajua unaweza ukawa unachat na mtu mkapendana lakini hamjawahi kukutana… ni mzuri wa kukushawishi, unajua sio rahisi mtu akiwa mbali aweze kukushawishi mkapendana wakati yeye yuko mbali na wewe uko mbali, namsifia kwa uzuri wake… sio wa umbo wala sura bali ana roho nzuri na alinitreat vizuri mpaka nikaona huyu ni sahihi nikabadilisha dini’
Screen Shot 2014-05-09 at 4.43.46 AM 
Sporah:     Ulifikiria kwamba dini yako sio nzuri au?

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 09, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

RAY C AFUNGUKA KUHUSU KUNUSURIKA KIFO KWA GONJWA HATARI LA DENGUE...!!!

http://jambotz8.blogspot.com/
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya DengueAkifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.

http://jambotz8.blogspot.com/Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu. “Huwezi kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue, walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu. 
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja. 
“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray 
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

MAREKANI 'INAIFUNGIA MLANGO' SYRIA

Viongozi wa upinzani wa serikali ya Syria wapo Washington Marekani kwa mashauriano
Marekani imeiwekea vikwazo benki moja ya Urusi inayofanya biashara na Syria kama sehemu ya jitihada za kuzidisha shinikizo za kiuchumi dhidi ya serikali ya Syria.
Hatua hiyo ilitangazwa wakati viongozi wa upinzani walioitembelea Washington wameanza kukutana na maafisa wakuu wa utawala.

Hii ni mara ya kwanza Marekani imeiwekea vikwazo benki ya Urussi inayofanya biashara na Syria.
Maafisa wa hazina ya Marekani wanasema hatua hii inanuiwa kuifungia milango Syria isiweze kuendelea kupenya mfumo wa kifedha wa dunia.
Vikwazo zaidi pia vimewekewa viwanda kadhaa vya kusafisha mafuta pamoja na maafisa sita wa ngazi ya juu katia serikali ya Syria.
Hayo yalitangazwa mda mfupi tu kabla ya kiongozi wa upinzani wa serikali ya Syria Ahmad Jarba alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa wa Marekani John Kerry.
Ahmad Jarba yuko katika ziara ya kwanza rasmi huko Marekani ambako anatarajiwa pia kukutana na rais wa Marekani Barack Obama. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...