Wednesday, October 09, 2013

WAKUU WA KAMPUNI ZA SIMU KENYA WAHOJIWA


zJo-confino-talks-to-Bob-C-001_a088d.jpg
Polisi nchini Kenya wamewahoji maafisa wakuu watendaji wa kampuni za huduma za simu za rununu kuhusu usajili wa kadi za simu za mkononi zinazotumia huduma za kampuni hizo.
Hatua ya polisi imefuatia ripoti kuwa simu zenye kadi ambazo hazikuwa zimesajiliwa zilitumiwa na magaidi walioshambulia jumba la Westgate mjini Nairobi wiki mbili zilizopia.
Wanne hao walitishiwa kukamatwa mnamo siku ya Jumatatu baada ya maafisa wa serikali kuwatuhumu kwa kuuza kadi za simu ambazo hazijsajiliwa.
Hata hivyo walikana tuhuma hizo.
Mnamo mwaka 2010, serikali ya Kenya ilieleza kuwa sharti mmiliki wa simu kusajili kadi yake ya simu ya mkononi katika hatua ya serikali kuzuia visa vya uhalifu wa kutumia simu za mkononi. Hata hivyo sheria ilianza kutekelezwa mwaka jana.
Takriban watu 67 waliuawa kwenye mashambulizi hayo na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulizi yaliyofanywa na kundi la kigaidi la al-Shabab .
Katika taarifa yao ya pamoja, maafisa hao wakuu wa kampuni za huduma za simu,Safaricom, Bharti Airtel, Orange Kenya na Yu Essar – walisema kuwa walitoa taarifa kwa polisi asubuhi ya leo.

WAPINZANI WASITISHA MAANDAMANO

zzzwapinzani_a58b3.jpg
Vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi vimeahirisha maandamano ambayo yalitakiwa kufanyika kesho (Alhamisi).
Vyama hivyo vilipanga kuandamana nchi nzima ili kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete asisaini muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwa una kasoro nyingi ikiwamo Zanzibar kutoshirikishwa katika mchakato.
Viongozi wa vyama hivyo wamesitisha uamuzi huo baada ya Rais Kikwete kusema yuko tayari kufanya nao mazungumzo kujadili suala hilo.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo Jumanne mara baada ya kukutana na viongozi wenzake katika Ofisi za NCCR-Mageuzi, Ilala Dar es Salaam.
Mbele ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Profesa Lipumba alisema viongozi wa vyama hivyo wametafakari na kuona ni busara kumsikiliza Rais Kikwete kwanza kabla ya kuamua kuendelea na uamuzi wao au la.
"Lengo la kuandaa maandamano ni kuhakikisha kwamba tunapata Katiba bora isiyo na kasoro, ndiyo maana tunaona kwa kuwa Rais ameonyesha nia ya kuzungumza na sisi tumeona ni bora tukakutana naye kwanza," alisema.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 09, 2013

DSC 0010 46ff2
DSC 0011 13794

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...