Thursday, April 23, 2015

AJARI ZARUDI TENA, BASI LAUA 10 SHINYANGA

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.

Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga
SIKU sita tangu ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace kuua watu 19 mkoani Mbeya, nchi imeendelea kukumbwa na ajali za barabarani. Safari hii watu kumi wamekatishwa uhai, kutokana na ajali ya basi na lori, iliyotokea mkoani Shinyanga jana.


Katika ajali hiyo, watu tisa walikufa papo hapo na mmoja aliaga dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Abiria 51 walijeruhiwa na wanatibiwa hospitali hapo, wakati tisa, akiwemo dereva wa basi, wako katika hali mbaya.

Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Ibingo Kata ya Samuye wilayani Shinyanga Vijijini na ilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha.

Alisema ajali ilitokea majira ya saa 9:30 alasiri baada ya basi la kampuni ya Unique, lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Tabora kugongana na lori la kampuni ya Coca Cola, lililokuwa linatoka Kahama. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ORODHA VYAMA VYA KIJAMII VITAKAVYOFUTWA KUANZA KUTOLEWA

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch, Isaac Nantanga.
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wowote wiki hii itaanza kutoa orodha ya vyama vya kijamii vitakavyofutwa kwa kuanzia na mkoa wa Dar es Salaam.

Imesema vyama hivyo vitafutwa kutokana na kutotekeleza matakwa ya kisheria ya kuwasilisha taarifa za mwaka za ukaguzi wa hesabu za vyama na vile ambavyo havilipi ada ya mwaka kama sheria inavyoelekeza.

Msemaji wa wizara hiyo, Isaac Nantanga alisema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufafanua suala la uhakiki wa vyama vya kijamii nchini.

Alisema vyama vitakavyobainika vitafutwa katika Daftari la msajili wa vyama vya kijamii na wala siyo Taasisi zisizo za kiserikali (NGO,s) kwani haihusiki nazo.

“Orodha ya vyama vitakavyofutwa itaanza kutolewa kwa awamu kuanzia wiki hii na kwa kuanzia orodha hiyo itahusu vyama vilivyosajiliwa mkoa wa Dar es Salaam”Alisema 

Alisema kufuatana na orodha iliyopo vyama 10,000 vya kijamii na Taasisi za Dini vimesajiliwa na wizara hiyo na vitakavyofutwa ni vile tu ambavyo haviwasilishi taarifa za kila mwaka za ukaguzi wa hesabu zao na pia kama havilipi ada ya kila mwaka kama sheria inavyotaka.

Juzi, gazeti moja la kila siku liliandika kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe anaanza kuhakiki NGOs jambo ambalo siyo la kweli kinachofanyika ni kwa taasisi za kijamii. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRILI 23, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC01667
DSC01668
DSC01669 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

VOLCANO YALIPUKA CHILE

Mlipuko wa Volcano 
 
Volcano aina ya Calbuco imelipuka kwa muda mfupi huko ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya zaidi ya miaka 40. Watu waliokuwa wakiishi maeneo jirani na ulikotokea mlipuko wa Volcano hiyo wamelazimika kuyahama makazi yao.

Picha za televisheni zilionyesha wingu zito na majivu vikipanda hewani umbali kilomita kadhaa angani katika jimbo la Los Lagos kusini mwa Chile.

Mamlaka nchini humo zimetoa tangazo la hali ya hatari kwa wakazi wote ambao wapo umbali wa kilomita la mlipuko wa Volcano hiyo huku safari za ndege kuelekea eneo hilo zikiwa zimeahirishwa. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

HALI MBAYA YEMEN...!!!

Wapiganaji wa Houthi nchini Yemen 
 
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya nchini Yemen, huku Mji mkuu Sanaa ukikosa umeme na maji kwa kipindi cha siku tisa zilizopita.

Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika hilo nchini humo Robert Mardini amesema ameshuhudia miili kadhaa kwenye mitaa alipotembelea mji wa Aden, na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni upelekaji wa huduma za kitabibu.

Awali Saudi Arabia ilisema itaendelea kutumia jeshi kuzuia waasi wa kihudhi kudhibiti Yemen, waasi nao wametaka kumalizwa kwa mashambulizi ya anga dhidi yao na kuanza mazungumzo.
Mpiganaji anayemuunga mkono Rais Abdrabbuh Mansour Hadi amesema ni mapema mno kuanza kuzungumzia makubaliano kati ya pande mbili. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

TIMU 4 ZATINGA NUSU FAINALI ULAYA


Javier Hernandez akishangilia goli mbele ya mashabiki wa Real Madrid
Timu nne zimetinga hatua ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyokamilika hapo jana, baada ya Real Madrid ya Hispania na Juventus ya Uitaliano kufanikiwa kuingia nusu fainali.
Timu ya Juventus
Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, Madrid walilazimika kusubiri hadi dakika ya 88, walipopata bao lao la pekee lililotiwa kimia Javier Hernandez almaarufu kama Chicharito,na hivyo kuhitimisha safari ya Atletico Madrid.
Katika msimu uliopita, huko Lisbon Ureno, Atletico walitolewa na Real Madrid katika hatua ya fainali.
Nayo Juventus imezima matumaini ya Monaco ya Ufaransa kwa kulinda bao lake lililofungwa katika mechi ya awali na hapo matokeo ikawa sare ya bila kutofungana. Hata hivyo nyota ni njema kwa Spain ambao sasa wanawakilishwa na timu mbili ambazo ni Real Madrid na Barcelona. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...