Sunday, June 30, 2013

LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMIE MAMBO YA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA AKIWA TANZANIA



Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Alisema  jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.
Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.
Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.
"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.
Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."


JK AMGEUKA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA JAJI JOSEPH WARIOBA

RAIS Jakaya Kikwete amemgeuka Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, kwa kuridhia azimio la Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka uwepo muundo wa serikali mbili.
Rais Kikwete ambaye juzi aliongoza kikao cha Kamati Kuu (CC), mjini Dodoma, aliridhia azimio hilo, huku akijua fika kuwa ndiye aliyemruhusu Jaji Warioba kuingiza kipengele hicho kwenye rasimu wakati alipoifikisha mbele yake kabla ya kuitoa hadharani.
Kutoka na hali hiyo, Kamati Kuu imewataka wanachama wao wote kupitia mabaraza ya CCM kuhakikisha wanakubaliana na msimamo wa chama wa kupinga muundo wa serikali tatu kama ilivyopendekezwa na tume ya Jaji Warioba.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Zanzibar, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa Kamati Kuu
imepitisha azimio la kutaka mabaraza ya Katiba ya chama hicho yajadili na kuridhia msimamo wa kuwa na serikali mbili.
Kamati Kuu ya CCM imekuja na mapendekezo ya namna ya kurekebisha kasoro kubwa za Muungano ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikilalamikiwa na Wazanzibari.

BEYONCE ATINGA VAZI LA KANGA, ILIYOTENGENEZWA NA MTANZANIA



clip_image001[6] 
Christina (katikati)
Utajiskiaje kuona Beyonce akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa kanga yenye maneno ya Kiswahili? ‘Wawili Ninyi Yawahusu….’ yanasomekana maandishi kwenye vazi alilolivaa mwanamuziki wa Marekani, 

 clip_image001
  Beyonce Knowles.
Vazi hili alilolivaa Beyonce kwenye moja ya show zake za tour ya Mrs Carter, limetengenezwa na mwanamitindo wa Tanzania aishie jijini London Uingereza, Christine Mhando mwenye brand ya Chichia London. Chichia London ndio brand iliyo maarufu sana nchini Uingereza kwa kutengeneza nguo za Kitanzania kwa kutumia Kanga na material mengine Kiafrika.
Hizi ni baadhi ya nguo alizotengeneza.
clip_image001[8]

LOWASSA AWATEKA WAENDESHA BODABODA ARUSHA...!!!

Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Diwani wa Mererani, Mathias Manga, ndiyo waliyobuni wazo hilo la kuwaanzishia mfuko vijana wa bodaboda.
Katika harambee hiyo, sh milioni 84 zilipatikana huku Lowassa pamoja na marafiki zake wakichangia sh milioni 10 na pikipiki 1WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amesema usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ni sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kusaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Akizungumza katika haraambee na uzinduzi wa mfuko wa waendesha pikipiki maarufu mkoani Arusha, Lowassa alisema sera hiyo ni ya kuwakomboa vijana.

Alisema kuwa kitendo cha wafanyabishara wa Arusha kujipanga kusaidia bodaboda ni mfano kwa wafanyabishara wengine nchini.

“CCM ni chama kinachotetea wanyonge, na nyinyi ni wanyonge mnaohitaji kunyanyuliwa kimaisha, kitendo hiki cha wafanyabisharaa wa Arusha ni cha kuunga mkono sera ya CCM,” alisema.

Lowassa alisema tatizo la ajira ni bomu linalosubiri kulipuka na kwamba wasipowasaidia vijana kuondokana na tatizo hilo amani itatoweka.

“Ndiyo maana CCM katika ilani yake ya uchaguzi imeliweka hilo na pia kulisisitiza katika vikao vyake vya juu vya Mkutano Mkuu pamoja na Halmashauri Kuu,” alisema.

HUU NDIO WOSIA WA MZEE MANDELA NA MAHALI ANAPOPENDA KUZIKWA

Mzee Nelson Mandela ameandika wosia kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4 ambamo ameagiza azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake huko Qunu, imebainika.

Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini, mwenye miaka 94, bado yuko mahututi lakini lakini hali yake inaimarika hospitalini mjini Pretoria ambako amekuwa huko kwa siku 21 zilizopita akitibiwa maambukizi kwenye mapafu.
Mnamo Januari 1996, wakati akiwa bado Rais, Mzee Mandela aliripotiwa kuandika wosia ambao aliagiza kufanyiwa maziko ya kawaida karibu na kijiji ambako alikulia kwenye rasi ya Mashariki.
Alisema kwamba wakati akifurahia kumbukumbu ya kulitumikia taifa hilo mjini Pretoria angetaka kuzikwa katika eneo la familia hiyo na kuwekewa jiwe la kawaida kama alama ya lilipo kaburi lake.
Gazeti la South African Mail na Guardian yaliripoti yakimnukuu rafiki wa siku nyingi wa familia akisema: "Hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la kufikiriwa, lakini hakuwahi kutaka chochote cha ufahari".
Licha ya ukweli kwamba mauzo ya kitabu cha Mandela cha Long Walk To Freedom, na michoro yenye jina lake, kumpatia mamilioni ya pesa kwa hadhi wosia wake uliripotiwa kutosha kwenye karatasi moja ya ukubwa wa A4.

OBAMA ATOA SABABU YA KUTOFANYA ZIARA KENYA...!!!


Rais Barack Obama.
Wakati Rais wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.



Alitoa kauli hizo mbili kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na baadaye alipozungumza na viongozi vijana wa Afrika akiwa katika ziara yake nchini Afrika Kusini.
Akizungumza jioni jana na vijana katika eneo la Soweto jijini Johannesburg, Obama alisema ataangalia uwezekano wa kwenda Kenya akiwa bado madarakani kwani bado ana miaka mitatu na  miezi saba ya uongozi wake.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...