Sunday, June 30, 2013

OBAMA ATOA SABABU YA KUTOFANYA ZIARA KENYA...!!!


Rais Barack Obama.
Wakati Rais wa Marekani, Barack Obama amesema asingeweza kufanya ziara Kenya kutokana na Rais wake, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Rutto kukabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), pia amehadharisha Afrika kuhakikisha kuwa kampuni za kigeni zinaajiri wafanyakazi wazalendo ili wawekeze nchini mwao.



Alitoa kauli hizo mbili kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na baadaye alipozungumza na viongozi vijana wa Afrika akiwa katika ziara yake nchini Afrika Kusini.
Akizungumza jioni jana na vijana katika eneo la Soweto jijini Johannesburg, Obama alisema ataangalia uwezekano wa kwenda Kenya akiwa bado madarakani kwani bado ana miaka mitatu na  miezi saba ya uongozi wake.

Alisema hayo alipojibu swali la mmoja wa vijana wa Kenya waliokuwa wakifuatilia kwa njia ya televisheni, aliyetaka kujua sababu ya yeye kutokwenda Kenya katika ziara hii.
Akifafanua, alikiri suala la Mahakama ya ICC nalo limechangia kutokana na kwamba ni suala la kimataifa.
“Mnakumbuka nilifanya ziara ya Ghana mwaka 2009 na safari hii nilitaka nifike pia Kusini mwa Afrika na Tanzania nilishapanga muda mrefu ... Kenya nilishafika mara nyingi kwa kuwa ni nyumbani, lakini nitakuja tena," alisema Obama.
Alipongeza uchaguzi wa Kenya safari hii, ambao alisema uliendeshwa vizuri  bila kusababisha ghasia kama uliotangulia.
Kabla ya kujibu swali hilo alisalimia “hamjambo” na kumalizia na “ahsante” baada ya kuulizwa swali hilo.
Alisema ni vigumu kwake kutembelea nchi ambayo Rais wake (Uhuru Kenyatta) na Naibu wake (William Ruto) wanashitakiwa katika Mahakama ya ICC.
Kenyatta na Ruto wanakabiliwa na mashitaka katika Mahakama hiyo, kwa madai ya kushiriki ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, ambazo zilisababisha vifo vya watu 1,300 na wengine kadhaa kukosa makazi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...