Monday, January 05, 2015

IPTL YASHUSHA BEI YA UMEME

Sethi Singh

KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa chini ya uongozi wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), imetangaza kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 20 baada ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo.

IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme inatarajiwa kushuka zaidi, kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito. Marekebisho hayo yaliyotumia zaidi ya Dola za Marekani milioni 25 ( Sh bilioni 42.5), yamewezesha mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme wa uhakika kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika Gridi ya Taifa mara tu baada ya marekebisho yaliyokamilika Desemba mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo, Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake inaoutoza kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao sasa utakuwa chini ya bei ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 ya dola ya Marekani (Sh 391) kwa kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JANUARI 05, 2015

.
.
.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MIILI 37 YA ABIRIA WA AIR ASIA IMEPATIKANA MPAKA SASA

Vikosi vya uokoaji majini wakitafuta miili ya waliokuwa kwenye ndege iliyoanguka 
 
Shirika la uokoaji nchini Indonesia limesema hivi sasa miili 37 imepatikana kutoka kwenye bahari ya Java ambapo ndege ya Air Asia iliangukia mwishoni mwa juma lililopita.
Helikopta na Meli za kijeshi zimekuwa zikifanya doria katika eneo la bahari hiyo ambapo vitu vinavyoelezwa kuwa mabaki ya ndege vimeonekana.hali ya hewa ya eneo hilo kwa sasa imetengemaa ingawa bado mikondo ya bahari ina nguvu.
Vikosi vya wapiga mbizi wa Indonesia na Urusi vina matumaini ya kupata vifaa vya kurekodia mawasiliano ndani ya ndege, ambavyo vitasaidia kujua sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Surabaya kwenda Singapore.
Air Asia ilikuwa imebeba Watu 162 ilipopata ajali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

RAIA WA SYRIA WAPEWA MASHARTI MAGUMU LEBANON

Lebanon imepokea Wakimbizi zaidi ya Wakimbizi milioni moja kutoka nchini Syria 
 
Masharti mapya yamewekwa na mamlaka ya Lebanon kwa Raia wa Syria wanaoingia nchini humo , wakati huu ambapo nchi hiyo inapokea Wakimbizi wengi.
Kwa mara ya kwanza, Raia wa Syria watalazimika kuwa na vielelezo vinavyoeleza kwa nini wanataka kuvuka mpaka na kuingia nchini Lebanon.
Masharti haya mapya yanaanza kutumika siku ya jumatatu.Awali kusafiri kati ya nchi hizo mbili kwa kiasi kikubwa hakukuwa na kikwazo lakini sasa Raia wa Syria lazima wawe na Viza.
Hatua hii inaelezwa kulenga kudhibiti idadi kubwa ya Wakimbizi wanaoingia nchini Lebanon, ambapo kwa sasa Lebanon ina wakimbizi zaidi ya milioni moja.
Hatua hii ya sasa haijulikani italeta athari gani kwa Raia wengi wa Syria walio nchini Lebanon ambao hawajajiandikisha kuwa wakimbizi.
Kabla ya sasa, Raia wa Syria waliweza kukaa nchini Lebanon mpaka miezi sita, lakini sasa raia wa nchi hiyo watalazimika kutimiza vigezo kadhaa ili kupatiwa Viza mpakani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

YANGA YANG'ARA KOMBE LA MAPINDUZI

Timu ya Yanga ya Dar es Salaam 
 
Michuano ya kuwania Kombe la Mapinduzi Zanzibar, linalozishirikisha timu saba za Zanzibar, nne za Tanzania Bara na KCCA kutoka Uganda imezidi kupamba moto ikiwa katika hatua ya kukamilisha michezo ya makundi.
Timu ya Yanga ya Tanzania Bara imezidi kutoa vipigo kwa timu za kundi lake baada ya kuzicharaza timu za Taifa Jang'ombe na Polisi zote za Zanzibar magoli 4-0 kila moja na hivyo kujikusanyia mabao nane na pointi sita ikiwa haijaruhusu nyavu zake kutikiswa na timu pinzani na hivyo kuongoza kundi A lenye timu za Taifa Jang'ombe, Polisi Zanzibar na Shaba pia ya Zanzibar.
Kwa matokeo hayo imefuzu kucheza hatua ya robo fainali.
Wapinzani wao wakubwa pia kutoka Bara, Simba imekuwa na mwendo wa kusuasua ambapo katika mchezo wake wa kwanza katika kundi C ilicharazwa na Mtibwa Sugar bao 1-0 kabla ya kuzinduka na kujipatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar. Katika kundi hilo Simba ina timu za Mtibwa Sugar ya Tanzania Bara, Mafunzo ya Zanzibar na JKU Zanzibar.
Kundi B lina timu za KCCA ya Uganda, Azam ya Tanzania Bara, KMKM na Mtende zote za Zanzibar.
Januari saba michuano hiyo itaingia hatua ya robo fainali kwa timu sita kutoka makundi yote matatu yenye jumla ya timu 12. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

VIGOGO LIGI KUU ENGLAND WATESA FA

 Heka heka katika lango la Hull wakati Arsenal ilipoibuka na ushindi wa 2-0
 
Mechi kadha zimechezwa kuwania kombe la FA kwa vilabu vya ligi kuu ya England na vile vya madaraja mengine.
Mabingwa watetezi Arsenal waliweza kuwacharaza Hull City 2-0 ambao wameshindwa kulipa kisasi baada ya kushindwa katika fainali za mwaka jana timu hizo zilipokutana. Magoli ya Arsenal yalifungwa na Per Mertesacker pamoja na Alexis Sanchez.
Wachezaji wa Chelsea wakipongezana baada ya ushindi 3-0 dhidi ya Watford
Mechi nyingine zilikuwa kati ya Chelsea na Watford, Chelsea ikiibuka na ushindi wa 3-0. Nayo Machester United ikiishindilia Yeovil 2-0. Kwa upande wake Manchester City nao waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Shef Wednesday.
Crystal Palace ilipata ushindi mnono dhidi ya Dover wa mabao 4-0, huku Stoke City ikiicharaza Wrexham magoli 3-1. Sunderland nayo ilivuna goli 1-0 dhidi ya Leeds.
Mechi kumi zimechezwa ambapo kwa ujumla vigogo wa soka England wameonekana kupata matokeo mazuri. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

VINARA LA LIGA WAAMBULIA VIPIGO

  Wachezaji nyota wa ligi kuu ya Hispania, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid
 
Ligi Kuu ya Hispania, La Liga imezidi kuleta ushindani mkubwa baada ya vinara wa ligi hiyo, Real Madrid na Barcelona kupoteza katika mechi zao za mwishoni mwa wiki.
Kikosi cha aliyekuwa kocha wa timu ya Manchester United David Moyes ambaye kwa sasa anainoa timu ya Real Sociedad ya ligi kuu ya Hispania, La Liga, imeiadhibu Barcelona kwa goli 1-0 alilojifunga mwenyewe mchezaji wa Barcelona Jordi Alba, mapema katika dakika ya pili ya mchezo.
David Moyes kocha wa Real Sociedad ya Hispania
Kipigo Real Madrid cha 2-1 kutoka kwa Valencia mapema Jumapili kingewawezesha Barcelona kuelekea mbele katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa ligi hiyo endapo timu hiyo ingeshinda.
Lakini kocha Luis Enrique alianza mchezo huo kwa kutowaanzisha wachezaji wake mashuhuri akiwemo Lionel Messi, Neymar na Dani Alves.
Barcelona ilishindwa kusawazisha goli walilojifunga wakati Moyes akipata ushindi wa pili akiwa meneja wa timu ya Sociedad.
Messi, Neymar na Alves walirejea katika mazoezi Ijumaa wiki iliyopita baada ya mapumziko marefu ya Krismasi Amerika Kusini ambako ligi ilisitishwa ili kusherehekea siku kuu hiyo.
Enrique alifanya mchezo wa kubahatisha kwa kutowapanga wachezaji hao katika mchezo wake na Real Sociedad ambayo imekuwa kikwazo kwa Barcelona katika michezo ya nyuma.
Wachezaji wa Real Sociedad wakishangilia goli katika moja ya michezo yao ya ligi kuu ya Hispania
Na kwa hiyo imethibitika kwa mara nyingine kwamba Barcelona hawana chao katika uwanja wa Anoeta sasa ikiwa ni michezo sita, Barcelona ikipoteza kwa Real Sociedad.
Kwa upande wake Real Madrid ilijikuta ikipoteza mchezo wake dhidi ya Valencia baada ya kucharazwa mabao 2-1 licha ya Real Madrid kuongoza kipindi cha kwanza kwa bao la penalti lililofungwa na Cristian Ronaldo dakika ya 14.
Valencia ilijipatia magoli yake yote mawili kipindi cha pili yakifungwa na Barragán dakika ya 52′ na Otamendi dakika ya 65.
Real Madrid inaongoza msimamo wa ligi ya Hispania ikiwa na pointi 39 katika michezo 16 ikifuatiwa kwa karibu na Barcelona yenye pointi 38 baada ya kucheza mechi 17. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...