KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)
ikiwa chini ya uongozi wa Kampuni ya Pan African Power Solutions (T)
Limited (PAP), imetangaza kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 20 baada
ya kufanya marekebisho makubwa ya injini za mtambo.
IPTL pia imetangaza kuwa bei yao ya umeme inatarajiwa kushuka zaidi,
kulingana na kushuka kwa bei ya mafuta mazito. Marekebisho hayo
yaliyotumia zaidi ya Dola za Marekani milioni 25 ( Sh bilioni 42.5),
yamewezesha mitambo ya IPTL kuwa katika nafasi nzuri ya kuzalisha umeme
wa uhakika kwa kufikia megawati 100 na kuingiza katika Gridi ya Taifa
mara tu baada ya marekebisho yaliyokamilika Desemba mwaka 2014.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo,
Harbinder Singh Sethi, IPTL sasa imepunguza bei ya umeme wake inaoutoza
kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambao sasa utakuwa chini ya bei
ya awali iliyokokotolewa ya senti 23 ya dola ya Marekani (Sh 391) kwa
kilowati; huku ikihakikisha kupatikana kwa umeme wa uhakika. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
“Tukiwa tunaukaribisha mwaka 2015, IPTL inajivunia kutangaza kuwa
imefanikiwa kufanya marekebisho makubwa ya mashine zake ya saa 36,000 ya
kufanya kazi, marekebisho yaliyokamilika ndani ya mwaka wa 2014.
Nimeiomba timu ya IPTL kupanga mapema jinsi gani wanaweza kuongeza
juhudi zaidi kufikia marekebisho ya saa 48,000, katika awamu inayofuata
katika mwaka 2015.
Tunatarajia uwepo wa IPTL kuwa bora zaidi kwa kuwa sasa tunajipanga
kuongeza rasilimali zaidi. “Hii ni sehemu ya ahadi ya PAP kuhakikisha
kuwa IPTL inaendeshwa vizuri na kwa ufanisi. Wakati sasa umefika kwa
Tanesco kuwa na uhakika wa kupata umeme wa uhakika wa megawati 100
katika Gridi ya Taifa wakati wowote utakapohitajika.
“IPTL chini ya PAP haiangalii tu uzalishaji wa umeme wa kutosha,
lakini pia ipo makini kuhakikisha kuwa umeme huo wa kutosha unakuwa
nafuu. Kwa maana hiyo, tumeamua kushusha bei zetu za umeme kufikia chini
ya bei iliyokokotolewa ya hapo awali ya senti 23 dola za Kimarekani kwa
uniti, ambayo sasa inaleta jumla ya punguzo la bei la asilimia 20 kwa
ile iliyokuwa ikitozwa na IPTL kabla ya PAP kuchukua uongozi,” alisema.
Sethi aliongeza kuwa Tanesco itarajie punguzo zaidi la bei ya umeme
kufikia kiwango cha chini ya senti 8 ya Dola ya Marekani (Sh 136) kwa
kila uniti ya umeme mara baada ya mitambo ya IPTL kupanuliwa na kufikia
uzalishaji wa megawati 500, mitambo yake itakapotumia gesi asilia.
Alisema kuwa mpango wa upanuzi wa mitambo hiyo, unaendelea vizuri.
Alisema wako katika hatua za awali za uchanganuzi na upimaji wa
udongo. “Tunatarajia hatua za upanuzi kwenda haraka ili kuhakikisha kuwa
IPTL inatoa huduma bora, ya uhakika na nafuu katika taifa hili,”
alisema. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment