Sunday, January 18, 2015

MATOKEO YA MECHI ZA EPL LEO JUMAPILI HAYA HAPA


article-2915617-24D1DC2000000578-487_964x390 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
 
EnglandPremier LeagueJanuary 18
FT West Ham United 3 – 0 Hull City
FT Manchester City 0 – 2 Arsenal

UPINZANI DRC: KATIBA IMEPINDULIWA

 
Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wamekubali mswada ambao wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais Joseph Kabila idhini ya kubaki madarakani, baada muhula wake wa pili kumalizika.
Mswada huo unapendekeza kufanywe sensa ya taifa kabla ya uchaguzi ambayo serikali inasema inaweza kuchukua miaka kadha kukamilisha.
Rais Kabila anamaliza muhula wa pili mwaka ujao.
Katiba ya nchi haimruhusu kugombea muhula wa tatu.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema wabunge wengi wa upinzani walisusia kura hiyo ya bunge, na kuielezea kuwa mapinduzi ya katiba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

BOKO HARAM WAFANYA UVAMIZI CAMEROON

Askari jeshi wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kundi haramu Boko Haram wameteka watu zaidi ya 60 katika nchi jirani ya Cameroon imethibitika.
Inasemekana miongoni mwa mateka wengi wao ni watoto waliokamtwa mpakani mwa nchi mbili hizo.Na inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa wakati wa utekelezaji wa tukio hilo.
Boko Haram siku za hivi karibuni zimekamata udhibiti wa miji kadhaa na vijiji upande wa kaskazini Mashariki mwa Nigeria, na sasa wameanza kuwa tishio kwa nchi jirani wanazopakana na Nigeria .Katika shambulio hilo la siku ya Jumapili askari hao walivamia vijiji viwili vilivyoko eneo la Tourou .
Katika uvamizi huo nyumba kadhaa zilichomwa moto na idadi ya mateka ni themanini kati yao watu wazima ni thelathini,na watoto wapatao hamsini na walielekea upande wa Kaskazini mwa Cameroon .
Kundi hilo limepigana vita takribani miaka sita sasa, wakijaribu kuusimika utawala wa dola ya kiislam nchini humo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ARSENAL YAWASHANGAZA MABINGWA WA EPL

 Santi Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza Mancity mabao 2-0 nyumbani Manchester.
Ushindi huo wa Arsenal pia ulisitisha msururu wa kutofungwa wa Mancity wa mechi 12.
Mchezaji wa Uhispania Santi Carzola aliyekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Mancity alifunga mkwaju wa penalty baada ya beki wa Arsenal Nacho Monreal kuangushwa katika eneo la hatari na beki Vincent Kompany.
 
Arsenal iliongeza bao la pili katika kipindi cha pili baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Santi Carzola kuwekwa wavuni na Olivier Giroud.
Matokeo hayo yameiwacha City ikiwa na alama 5 chini ya viongozi wa ligi Chelsea.
City na Arsenal walitoka sare ya 2-2 wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika uga wa Emirates mnamo mwezi Septemba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

VIWANJANI MWISHONI MWA WIKI

Ligi kuu ya England imeendelea kwa mechi mbili ambapo..Arsenal imeibamiza Man City ,Huku Westham Ikiibamiza Hull City bao 3-0
Nayo Michuano ya Kombe la Mataifa barani Afrika ikiwa imeng'oa nanga hapo jana kwa Gabon Kuilaza Burkina faso bao 2-0 Huku Pierre Emerick Aubemeyang aking'ara vilivyo.Nao wenyeji Equitorial Guinea wakishikwa shati na Congo Brazaville kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.
Ligi kuu ya England ambapo Jumapili zimechezwa mechi mbili ,Katika mechi ya awali Westham United iliibamiza Hull City bao 3-0 mabao yaliyotiwa kambani na Andy Carrol katika dakika ya 49,Amalfitano katika dakika ya 69 na Stewart Downing aliyehitiisha ushindi huo mnono wa Westham katika ya 72 akimalizia pasi murua ya kiungo Mcameroun aliyeko kwenye Fomu Alexandre Song.
Kwa matokeo hayo Westham imefikisha Point 36 wakiwa nafasi ya 7,wakiwa pointi moja mbele ya Liverpool wenye pointi 35 walioko nafasi ya 8,huku timu hizo zikitaraji kukutana katika mechi ijayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...