Sunday, January 18, 2015

ARSENAL YAWASHANGAZA MABINGWA WA EPL

 Santi Carzola alifunga bao moja na kutengeza jengine na kuisadia Arsenal kuicharaza Mancity mabao 2-0 nyumbani Manchester.
Ushindi huo wa Arsenal pia ulisitisha msururu wa kutofungwa wa Mancity wa mechi 12.
Mchezaji wa Uhispania Santi Carzola aliyekuwa moto wa kuotea mbali dhidi ya Mancity alifunga mkwaju wa penalty baada ya beki wa Arsenal Nacho Monreal kuangushwa katika eneo la hatari na beki Vincent Kompany.
 
Arsenal iliongeza bao la pili katika kipindi cha pili baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Santi Carzola kuwekwa wavuni na Olivier Giroud.
Matokeo hayo yameiwacha City ikiwa na alama 5 chini ya viongozi wa ligi Chelsea.
City na Arsenal walitoka sare ya 2-2 wakati walipokutana kwa mara ya kwanza katika uga wa Emirates mnamo mwezi Septemba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...