Sunday, January 18, 2015

UPINZANI DRC: KATIBA IMEPINDULIWA

 
Wabunge wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wamekubali mswada ambao wadadisi wanasema unakusudiwa kumpa Rais Joseph Kabila idhini ya kubaki madarakani, baada muhula wake wa pili kumalizika.
Mswada huo unapendekeza kufanywe sensa ya taifa kabla ya uchaguzi ambayo serikali inasema inaweza kuchukua miaka kadha kukamilisha.
Rais Kabila anamaliza muhula wa pili mwaka ujao.
Katiba ya nchi haimruhusu kugombea muhula wa tatu.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema wabunge wengi wa upinzani walisusia kura hiyo ya bunge, na kuielezea kuwa mapinduzi ya katiba. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...