Thursday, May 28, 2015

MWANASHERIA KENYA AJITOSA KUMUOA MTOTO WA OBAMA...!!!

Rais Barrack Obama wa Marekani akiwa na mtoto wake Malia. 

Mwanasheria kijana nchini ametuma ombi la kumuoa mtoto wa Rais Barack Obama anayeitwa Malia.
Mwanasheria Felix Kiprono alisema jana kwamba yupo tayari kutoa ng’ombe 50, kondoo 70 na mbuzi 30 ikiwa ni mahari ya kumposa mtoto huyo.
Alisema kuwa analazimika kufanya hivyo ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kumuoa mtoto wa Rais Obama.
“Nimevutiwa kumchumbia Malia tangu mwaka 2008,” alisema Kiprono baada ya kuhojiwa na gazeti la The Nairobian. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

ODAMA: NAOGOPA MSAADA WA MASHARTI...!!!

Odama
Jennifer Kyaka ‘Odama

MWIGIZAJI mwenye mvuto katika filamu za Bongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’, amesema anaogopa marafiki wa kiume kwa kuwa huwa na masharti magumu pindi wanapotoa msaada.
“Wasanii wa kiume kwangu sipendi kwa kuwa huwa na masharti kuliko marafiki wa kike ambao husaidia bila masharti ya ajabu,” alisema.
Aliongeza kwamba, marafiki wa kike anakuwa huru kuwaeleza shida na matatizo yake kuliko wa kiume ndiyo maana hiyo ni sababu yake nyingine ya kutopenda marafiki wa kiume kama anavyopenda marafiki wa kike. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 28, 2015 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC03017
DSC03018
DSC03019
Nunua gari bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

"NATAKA KUWA MCHEKESHAJI" INSPEKTA HAROON

INSPECTOR.
Haruna Kaena ‘Insepkta Haroun’

UNALIKUMBUKA kundi la Gangwe Mobb, hapo lazima utamtaja Haruna Kaena ‘Insepkta Haroun’ na Luten Kalama, wawili hao baada ya kutengana kila mmoja akawa anafanya kazi binafsi lakini sasa Inspekta Haroun ameibuka na kudai kwamba anataka kuwa mwigizaji wa vichekesho.
Inspekta Haroun aliyetamba na wimbo wa ‘Mtoto wa Geti Kali’ aliendelea kueleza kwamba fani anazozipenda ni muziki na kuigiza vichekesho.
“Mimi msanii hivyo natakiwa niwe mbunifu, nisibweteke na kazi, fani moja na kwa sasa napenda kuwa mwigizaji wa vichekesho kwa kuwa napenda kazi hiyo na ninaiweza,” alijinadi.
Msanii huyo aliwahi kushirikishwa katika vipengele vya uigizaji katika kipindi cha vichekesho kilichokuwa kikirushwa na televisheni ya Clouds. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

WABUNGE WAMKAANGA MAGUFULI

Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli 

Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli amekuwa hapati wakati mgumu anapowasilisha bajeti ya wizara hiyo, lakini hali ilikuwa tofauti jana wakati wabunge walipoungana kueleza hofu yao katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara kutokana na madeni ya makandarasi.
Wabunge hao walidiriki kueleza kuwa kuna ufisadi katika ununuzi wa kivuko cha Bagamoyo na wengine kueleza kuwa miradi iliyotajwa kwenye hotuba ya bajeti ilishatekelezwa miaka ya 80 na 90.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016 iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti, Profesa Juma Kapuya, deni linalodaiwa na makandarasi ni kati ya Sh850 bilioni na Sh900 bilioni.
“Kamati haijaridhishwa kabisa na hali hii kwani deni hili sasa ni kubwa kuzidi hata bajeti inayotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wizara hii, jambo ambalo linafanya bajeti hii kuonekana ni kiini macho tu,” alisema Profesa Kapuya.
Kambi ya Upinzani
Katika taarifa yake, Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) ilimshutumu Waziri Magufuli kwa kuandika hotuba ndefu ili kuwachanganya wabunge, huku hotuba hizo zikitaja hata miradi ya barabara zilizojengwa miaka ya 80 na 90.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...