Thursday, August 14, 2014

UKAWA WAOMBWA KURUDI BUNGENI


UKAWA waombwa kukubali maoni ya watanzania walio wengi ya kuheshimu pesa za walipa kodi kwa kurudi bungeni na kupingana kwa hoja kwani hoja zao zikiwa za huakika hazitapingwa bali kanuni na taratibu zinazoendesha bunge zitafuatwa badala ya kuendelea kulalamika katika majukwaa ya kisiasa.

Kauli hiyo imetolewa na balozi wa amani Tanzania Risasi Mwaulanga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo leo jijijni Dar es Salaam.

"Nawaomba UKAWA warudi bungeni ili tuweze kupata katiba mpya itayoyokidhi changamoto za watanzania wote na sio masuala ya vyama vya kisiasa na maslahi binafsi kwani vyama hiyvo vinaweza kutoweka wakati wowote na nchi ikabaki palepale".Alisema Mwaulanga.

Aidha Mwaulanga anaiomba iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya jaji Warioba, viongozi wa dini, na asasi za kiraia kuendelea na jitihada za kuitaka UKAWA kurejea Bungeni ili kurahisisisha upatikanaji wa Katiba mpya yenye maslahi mapana kwa ummma kuliko ya kisiasa.

Balozi huyo wa amani amesema kuwa kauli za vitisho na uvunjifu wa amani unapaswa kupigiwa kelele na kulaniwa na kila mwanademokrasia duniani katika kipindi hiki cha kuandaa Katiba mpya ili wajumbe waweze kuwa huru wakati wa kutoa maoni.

Tanzania ni nchi ya amani,umoja, upendo na maelewano na siyo nchi ya vita,chuki na mafarakano hivyo watanzania tunapaswa kutambua ni Katiba gani tunayoitaka na kuwa na mtazamo sahihi na maamuzi bora. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
 
 Na Rose Masaka-MAELEZO

ASKOFU ATUPWA JELA MIAKA 32 KWA UJAMBAZI BENKI...!!!




Benki ya NBC tawi la Moshi. Picha ya Maktaba

Askofu wa Kanisa la Christian Fellowship Assemblies of God la Arusha, Jumanne Kilongola amehukumiwa kifungo cha miaka 32 jela baada ya kupatikana na hatia ya kupora Sh5.3 bilioni ndani ya Benki ya NBC, Tawi la Moshi Mei 21, 2004.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kilimanjaro, Simon Kobelo, askofu huyo amehukumiwa kifungo hicho pamoja na raia watano wa Kenya baada ya kupatikana na hatia ya kufanya wizi huo kwa mtutu wa bunduki.

Kati ya fedha hizo, Sh126.2 milioni zilikuwa mali ya Benki ya NBC wakati Sh5.1 bilioni ni mali ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ilikuwa ikitumia NBC Moshi kama kituo chake kidogo.

Ilielezwa mahakamani hapo wakati wa ushahidi kuwa Askofu Kilongola ndiye aliyekodi gari aina ya Toyota Landcruiser lililotumiwa kubeba fedha hizo kwa Sh320,000 na alimweleza mmiliki wake kuwa alikuwa anakwenda kubeba wanakwaya wake.

Raia wa Kenya waliohukumiwa kifungo hicho cha miaka 32 ni Wilfred Onyango Nganyi, Patrick Muthee Murithi, Gabriel Kungu Kariuki, Jimmy Maina Njoroge na Simon Ndungu Kiambuthi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KENYA HATArINI KUPATA EBOLA...!!!

Afisa wa shirika la afya duniani aeleza kuhusu janga la Ebola Duniani
Shirika la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo.
Hatari hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.(Martha Magessa)
Hili ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.
Wataalamu wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki. Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia. Nigeria ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani Afrika na ndio ya hivi karibuni kuripoti kuwa na thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema kuwa nchi hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Serikali hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri, safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka Afrika Magharibi.
Shirika la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini Nigeria.
BBC

SOMA HAPA UPATE ELIMU KUHUSU KUJIKINGA NA UGONJWA HATARI WA EBOLA

Hivi karibuni tumesikia Mlipuko wa Ugonjwa Hatari wa Ebola ambapo tayari umesharipotiwa kuua zaidi ya watu 1000 huko Guinea, Siera Lione, Liberia ...Na Juzi umeripotiwa Kuingia Nigeria......na Mpaka Sasa watu takribani 1750 wameripotiwa kuathirika na Ugonjwa huu.
SASA TUJIFUNZE KIDOGO

Ebola Ni Nini?

Ebola ni ugonjwa wa Mlipuko ambao virusi vyake hushambulia mfumo wa Damu wa Binadamu. Kwa Lugha ya Kisayansi Ebola huitwa haemorraghic fever, Ugonjwa huu hupelekea Muathirika kuvuja damu sehemu karibu sehemu yoyote ile ya mwili wake na hatimaye kusababisha kifo kutokana na muathirika huyo kupoteza damu nyingi. Na Kuvuja Damu huko kunaweza kuwa ni ndani ya Mwili au Nje ya Mwili.

Dalili za Ugonjwa Wa Ebola huanza kuonekana siku mbili hadi wiki tatu mara baada ya mtu kuambukizwa virusi hivyo na Kupelekea Homa, Muscle kuuma pamoja na Kichwa Kuuma huku dalili zingine zikiwa ni Kutapika, kuharisha kukifuatiwa sambasamba na Kupungua kwa ufanyaji kazi wa Ini na Figo katika Mwili wa Binadamu.

Virusi Vya Ebola vinaweza kupatikana kwa kugusa damu au majimaji kwenye mizoga ya Wanyama hususani Nyani na Popo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI YA MIVUMONI ILIYOPO KWENYE MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI YATEKETEA KWA MOTO

 Moto Mkubwa ukiendelea kuwaka katika eneo la juu la Jengo la Shule ya Sekondari ya Kiislam ya Mivumoni (Mivumoni Islamic Seminary) iliyopo ndani ya Msikiti wa Mtambani,Kinondoni B Jijini Dar es Salaam leo.

 Moto mkubwa ukiendelea kuwaka kwenye eneo hilo.
 Ulinzi mkali wa Polisi ulitawala katika eneo la Msikiti huo wa Mtambani kuhakikisha Usalama unakuwepo kwenye eneo hilo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BIASHARA MPYA, KONDOM ZAAGIZWA KWA SIMU, ZINALETWA MAHALI ULIPO, SIKILIZA HII...!!!

Huenda uliwahi kupata huduma ya taxi au kuletewa chakula popote ulipo kwa kupiga tu simu, lakini je utanyanyua simu kwa kutaka huduma ya condom?
Kundi la wafamasia nchini Uganda wameibuka na ubunifu wa kipekee wa kupata huduma ya condomu kwa kupiga tu simu.
Huduma hiyo inaitwa DIAL A CONDOM...yaani unapiga simu tu na kuaguza Condom.
Na hutoa nambari za simu ambazo wateja huweza kupiga, kwa ahadi kuwa watapelekewa aina yoyote ya condom katika kipindi cha dakika 15 au chini ya hapo.
Muliro Telewa anaelezea zaidi kuhusu huduma hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

AFANDE SELE AFIWA NA MAMA TUNDA....!!!



Msanii kutoka Morogoro Selemani Mshindi maarufu kwa jina la Afande Sele kupitia ukurasa wa facebook ametoa taarifa ya kufiwa na mzazi mwenzake mama Tunda. Afande Sele ameandika;-

“Ndugu zangu!! Nimefiwa na mzazi mwenzangu (Asha) /mama wa wanangu (mama Tunda) ..ni pigo kubwa kwangu na wanangu. SISI NI WAJA WA MWENYEZI MUNGU NA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA; MUNGU AMPUMZISHE PEMA." Jambo Tz tunatoa pole kwa Afande Sele na famila kwa ujumla kwa kuondokewa na kipenzi chao.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS AGOSTI 14, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HIZI NDIZO HATUA ZAIDI ZA KUZIA KUSAMBAA KWA EBOLA

Jitihada zaidi zafanywa kupambana na Ebola
Jitihada zinaendelea kuzuia kusambaa kwa maradhi ya Ebola, Afrika Magharibi.Tangu mwezi Machi kirusi hicho kimeua zaidi ya watu elfu moja, wengi wao kutoka Sierra Leone, Liberia na Guinea.
Nigeria nayo imetangaza kuwepo kwa mtu wa tatu aliyekuwa na ugonjwa huo. Wakati huohuo, Shirika la Afya Dunia limeielezea Kenya kuwa katika hatari kwani kuna uwezekano mkubwa wa kusambaa kwa virusi hivyo kutokana na kuwepo safari nyingi za ndege kutoka nchi hiyo kuelekea Afrika magharibi.

Huko nchini Nigeria ambako tayari Ebola imesababisha vifo vitatu, serikali imewataka watu wote kushirikiana na wataalamu wa afya hasa baada ya kuwapo kwa taarifa ya muuguzi aliyetoroka hosipitalini baada ya kuwekwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya kufuatia kuhofiwa kuwa ameathirika na Ebola. Muuguzi huyo ameelekea nyumbani kwake huko mashariki mwa Nigeria hali inayowatia hatarini watu wengi.

Hivi sasa kiasi kidogo cha dawa za majaribio kimefika nchini Liberia kuwatibu madaktari wawili. Maabara iliyotoa dawa hiyo huko marekani inasema imeishiwa kabisa dawa hizo.
Siku moja tu baada ya shirika la afya duniani kutoa ruhusa ya kutumiwa dawa hizo Canada nayo imetangaza kuwa itatuma dozi 1000 za chanjo kwenda afrika magharibi ambako wahudumu wa afya ndio watakaopewa dawa hiyo ingawa haijawahi kufanyiwa majaribio.

Huko Sierra Leone daktari bingwa mwingine amefariki kwa ugonjwa wa ebola. Modupeh Cole amekuwa akifanya kazi mjini Freetown na kifo chake kinakuja baada ya mtaalamu pekee wa virusi nchini humo kufariki wiki mbili tu zilizopita. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAREKANI KUTUMIA NJIA MBADALA IRAQ

Marekani kutumia njia mbadala kuokoa Wayazidi
Marekani sasa imesema inafikiria kutumia njia mbadala za kuwaokoa maelfu ya Wayazidi, wananchi wa Iraq waliokwama katika mlima kaskazini mwa Iraq wakikimbia kushambuliwa na wapiganaji wa dola ya
Kiislamu.
Ikulu ya Marekani imerudia kauli yake kuwa haitatumia majeshi ya ardhini kupambana na wapiganaji hao wa dola ya kiislam lakini ikasema inaweza kuwatumia katika kutoa msaada wa kibinadamu.
Msemaji wa Ikulu ya marekani Ben Rhodes amesema Serikali yake ilikuwa ikijadili wazo la Ufaransa, Australia na Canada nao kutoa msaada wa kibinadamu.
Kwa upande wa Uingereza Waziri Mkuu David Cameron amesema mipango thabiti ilikuwa ikiwekwa sawa kwa ajili jumuia ya kimataifa kuwaokoa Yazidi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...