Afisa wa shirika la afya duniani aeleza kuhusu janga la Ebola Duniani
Shirika
la afya duniani, limetahadharisha kuwa Kenya inaweza kuwa katika hatari
ya kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, kutokana na kasi ya kuenea kwa ugonjwa
huo.
Hatari
hii inatokana na Kenya kuwa kitovu cha usafiri wa ndege huku wasafiri
wengi wanaokwenda Afrika Magharibi wakipitia nchini humo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa onyo ya afisaa mkuu wa shirika la afya duniani WHO.(Martha Magessa)
Hili
ndilo onyo kali zaidi kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kutolewa na shirika
la WHO kwamba Ebola huenda ikaenea katika kanda ya Afrika Mashariki.
Wataalamu
wa afya wanasema kwamba wanajitahidi kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo
Afrika Magharibi, ambako zaidi ya watu 1,000 wamefariki. Canada imesema kwamba itatoa mchango wa dozi 1000 za chanjo ya majaribio ya Ebola kusaidia watu kutoambaukizwa ugonjwa huo.
Kisa cha kwanza cha Ebola,kiliripotiwa nchini Guinea mwezi Februari kabla ya kuenea hadi nchini Sierra Leone na Liberia. Nigeria
ni nchi yenye idadi kuwba ya watu barani Afrika na ndio ya hivi karibuni
kuripoti kuwa na thuluthi moja ya vifo kutokana na Ebola.
Kisa cha tatu kiliripotiwa siku ya Jumanne.
Mkurugenzi
wa shirika la afya duniani tawi la Kenya, Custodia Mandlhate, amesema
kuwa nchi hiyo iko katikahatari kubwa ya kupata Ebola.
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Hatua za kuzuia maambukizi na kuweza kutambua wagonjwa zimeshika kasi mjini Nairobi katika siku za hivi karibuni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Serikali
hata bhivyo imesema kuwa haitasitisha safari za ndege kutoka katika nchi
nne zilizokumbwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi.
"Hatushauri,
safari za ndege kusitishwa kwa sababu ya mipaka yetu ambayo watu
wanaingia na kutoka pasipo vikwazo vingi, '' alisema waziri wa afya
James Macharia.
Kenya hupokea zaidi bya safari 70 za ndegekuoka Afrika Magharibi.
Shirika
la kikanda la Ecowas, limesema kuwa mmoja wa maafisa wake Jatto Asihu
Abdulqudir, mwenye umri wa miaka 36, alifariki kutokana na Ebola nchini
Nigeria.
BBC
No comments:
Post a Comment