Thursday, November 06, 2014

NUSU YA WANAFUNZI WAFAULU DARASA LA SABA


Wanafunzi wa Shule ya Msingi Peaceland ya mkoani Mwanza wakishangilia baada ya kupata taarifa ya shule yao  kushika nafasi ya tatu kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa mwaka 2014 yaliyotangazwa jana. 

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2014 yakionyesha kuwa zaidi ya nusu ya wanafunzi waliofanya mtihani huo Septemba mwaka huu, wamefaulu.
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde yanaonyesha kuwa wasichana wamefanya vizuri zaidi ya wavulana, huku ufaulu kwa jumla ukiwa umeongezeka kwa asilimia 6.38 ikilinganishwa na mwaka 2013.
Katika matokeo hayo Shule ya Twibhoki iliyopo mkoani Mara iliibuka ya kwanza kitaifa kati ya shule 15,867 zilizofanya mtihani huo ikifuatiwa na Mugini, Peacland na Alliance zote za mkoani Mwanza.
Shule ya tano ni Kwema ya Shinyanga ikifuatiwa na St Severine ya Kagera, Rocken Hill ya Shinyanga, Tusiime ya Dar es Salaam, Imani ya Kilimanjaro na iliyoshika nafasi ya 10 ni Palikas ya Shinyanga.
Wakuu wa shule vinara wazungumza
Mkuu wa Shule Twibhoki iliyopo Mugumu - Serengeti, Alphonce Magori alisema siri ya mafanikio hayo ni kila mwalimu kutambua nafasi yake. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WASOMI, WANASIASA WAPINGA KAULI YA KIKWETE




Rais Jakaya Kikwete. PICHA|MAKTABA 
Makundi mbalimbali ya wasomi, wanaharakati na wanasiasa nchini wamepinga kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuzuia kampeni za utoaji wa elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa wakisema yeye mwenyewe na chama chake ndiyo waliohusika kuanza kampeni mapema hivyo hana haki ya kuzuia makundi mengine.

Juzi, Rais Kikwete alisema muda wa kampeni za ama kuiunga mkono au kuipinga Katiba Inayopendekezwa bado na hakukuwa na sababu ya wanasiasa na taasisi za kiraia kuanza kampeni mapema, lakini wakati huo huo yeye na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein wamenukuliwa wakiipigia debe.

Wakati Mwenyekiti wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Penina Mlama akisema si sahihi kuzuia makundi fulani kutoa elimu hiyo wakati wengine wakiendelea na kampeni za kuipigia debe, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema Kikwete ameshindwa kuficha hisia zake kama mwenyekiti wa CCM. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAKONDA: "VURUGU ZILIZIMA NDOTO ZANGU"



Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa gazeti la Mwananchi alipotembelea makao makuu ya Mwananchi Communications Limited, Tabata jijini Dar es Salaam jana. 

Katibu wa Hamasa wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda amesema alitamani kuzungumza siku ya mdahalo ulioandaliwa na Kigoda cha Mwalimu Nyerere Foundation lakini vurugu zikazima ndoto yake.

Makonda ambaye anatuhumiwa kuwa ndiye aliyepanga vurugu hizo zilizosababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba kushambuliwa, alikana na kudai kuwa hata yeye alitamani kukisikia kile kilichopangwa kuzungumzwa na wasemaji wakuu wa mdahalo huo ili ajibu hoja zao katika mkutano huo.

Akizungumza jana katika ofisi za gazeti hili, Makonda alisema aliingia ukumbini akiwa na nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa madai kuwa ingeweza kumsaidia kuainisha yale ambayo yangejadiliwa na ikibidi achangie hoja kwa kutetea au kutoa ufafanuzi wa kile kilichoandikwa ndani ya Katiba hiyo.

“Nasikitika kwa sababu malengo yangu hayakutimia kutokana na vurugu zile. Lengo langu lilikuwa; nipate nafasi ya kuzungumza ili nitoe hoja zangu na kufafanua uzuri wa Katiba Inayopendekezwa,” alisema.

Hata hivyo, alisema yaliyosemwa na Jaji Warioba kabla ya mdahalo kuvunjika, yalimpa fursa ya kujua ni vifungu vipi vina kasoro na vipi viko sahihi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 06, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

OBAMA AAHIDI KUSHIRIKIANA NA REPUBLICAN


Rais Barack Obama

Kiongozi mpya wa Baraza la Senate la Marekani kutoka chama cha Republican na Rais Barack Obama wote wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani.
Wanachama wa Republican wamepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi wa nusu muhula na kwa sasa wanadhibiti mabunge yote mawili nchini Marekani. Kiongozi wa baraza la Senate anayeingia madarakani Mitch McConnell amesema ataliwezesha baraza hilo kufanya kazi na kupitisha miswada ya sheria.
Bwana Obama amesema alikuwa na "hamu ya kufanyakazi na baraza jipya la Congress na kufanya miaka miwili yake aliyobaki kukaa madarakani kuwa na tija kadiri iwezekanavyo".

Senata Mitch McConnell kiongozi wa Republican katika Baraza la Senate, akipunga mkono na mke wake.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANAJESHI WA LIBYA WAFUKUZWA UINGEREZA

Wanajeshi wa Libya
Wanajeshi kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi.
Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300 kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na unyanyasaji wa kimapenzi.
Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo.
wanajeshi wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko Cambridge, ambapo wawili wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka ya ubakaji.
Baadhi ya wakazi wa eneo jirani na kambi ya jeshi walipo wanajeshi hao wa Libya,wamesema kuwa wamekuwa wakiwaona wanatoka nje ya ngome za jeshi kwaajili ya kununua pombe, na tayari waziri wa ulinzi amekiri kupokea mashtaka hayo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanajeshi hao wa kigeni.
Waziri Libya amesema wanajeshi hao wanaruhusiwa kutoka nje ya kambi kwa saa tatu wiki kwani ameongeza kuwa madhara ya askari hao kuzagaa mitaani ni makubwa na wengine hujitumbukiza katika matumizi dawa za kulevya na ulevu wa kupindukia. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

BURKINA FASO KUFANYA UCHAGUZI MKUU 2015

Luten Kanal Isaac Zida
Vyama vya siasa nchini Burkina Faso vimekubaliana kuwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2015 ikiwa ni harakati za kurejesha utawala wa kiraia na demokrasia..
Hata hivyo mazungumzo hayo yameisha bila kuwa na ufumbuzi kuhusiana na nani atakayekuwa kiongozi wa mpito hadi kufikia muda wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa aliyekuwa raisi wa taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore.
Jeshi la nchi hiyo limekuwa likishikilia madaraka ya tangu aondolewe madarakani kutokana na maandamano ya raia waliokuwa wakishinikiza Rais Compaore.
Umoja wa Afrika jumatatu wiki hii umetoa muda wa wiki moja kufanyika kwa mabadiliko ya utawala na kukabidhiwa kwa wananchi na siyo jeshi tena.
Luten Kanal Isaac Zida ambaye ni kiongozi wa mpito wa kijeshi ameahidi kufuata ushauri huo wa umoja wa Afrika kwa kukabidhi madaraka kwa wananchi ndani ya muda huo wa wiki mbili. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BADO HAKIJAELEWEKA SIMBA


 
Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi kwenye Ufukwe wa Coco kujiandaa na mchezo dhidi ya Ruvu Shooting juzi jijini Dar es Salaam.

Ni presha kila kona Simba. Ndivyo unavyoweza kusema wakati kamati ya utendaji ya klabu hiyo ikikutana leo, kocha Patrick Phiri ameanza upya kuwanoa wachezaji kwa kuwapeleka ufukweni ili kujenga stamina.
Dharura hiyo ya kikao cha kamati ya utendaji inaonyesha hali si shwari ndani ya Simba, jambo linalowafanya viongozi wahangaike ili kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.
Kwa upande wao, viongozi wanawatuhumu baadhi ya wachezaji kucheza chini ya kiwango, utovu wa nidhamu huku kocha Patrick Phiri akipewa mtihani wa mechi ili akishindwa, iwe sababu ya kutimuliwa.
Mashabiki wengi wa klabu hiyo wanaamini kuwa kocha anaonewa, tatizo lipo kwa uongozi unaotakiwa kujichunguza ili kuona wapi umekosea na kuondoa kasoro zilizopo na si kukimbilia kumlaumu kocha. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...