Katibu wa Hamasa
wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Paul Makonda amesema
alitamani kuzungumza siku ya mdahalo ulioandaliwa na Kigoda cha Mwalimu
Nyerere Foundation lakini vurugu zikazima ndoto yake.
Makonda ambaye anatuhumiwa kuwa ndiye aliyepanga
vurugu hizo zilizosababisha aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba kushambuliwa, alikana na kudai
kuwa hata yeye alitamani kukisikia kile kilichopangwa kuzungumzwa na
wasemaji wakuu wa mdahalo huo ili ajibu hoja zao katika mkutano huo.
Akizungumza jana katika ofisi za gazeti hili,
Makonda alisema aliingia ukumbini akiwa na nakala ya Katiba
Inayopendekezwa kwa madai kuwa ingeweza kumsaidia kuainisha yale ambayo
yangejadiliwa na ikibidi achangie hoja kwa kutetea au kutoa ufafanuzi wa
kile kilichoandikwa ndani ya Katiba hiyo.
“Nasikitika kwa sababu malengo yangu hayakutimia
kutokana na vurugu zile. Lengo langu lilikuwa; nipate nafasi ya
kuzungumza ili nitoe hoja zangu na kufafanua uzuri wa Katiba
Inayopendekezwa,” alisema.
Hata hivyo, alisema yaliyosemwa na Jaji Warioba
kabla ya mdahalo kuvunjika, yalimpa fursa ya kujua ni vifungu vipi vina
kasoro na vipi viko sahihi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“Kwa maelezo ya Jaji Warioba, asilimia 90 ya maoni
yaliyokuwamo katika Rasimu waliyoipendekeza ndiyo yaliyomo katika
Katiba hii Inayopendekezwa,” alisema Makonda.
Tuhuma zinazomwandama
Kada huyo wa CCM, akizungumzia tuhuma kuwa
alishiriki kumpiga Jaji Warioba, alisema kamwe hawezi kufanya kitu kama
hicho na hakuna mtu yeyote anayeweza kuthubutu kumpiga mzee huyo.
Alisema tuhuma zinazozidi kumwandama sasa ni
mwendelezo wa zile zilizokuwa zikiwatuhumu awali, Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.
“Mimi ni kama napokea kijiti kutoka kwa hawa
watangulizi wangu, walishatuhumiwa sana kuwa walikuwa wakitumwa
kuanzisha vurugu na mambo mengine mengi, lakini hakuna hata mtu mmoja
aliyethibitisha hili, binafsi naona huu ni mchezo tu wa kisiasa wa watu
kutaka kutafuta huruma kutoka kwa watu wengine,” alisema Makonda.
Alisema hata malumbano yanayoendelea hivi sasa
kuhusiana na Katiba hiyo mpya, hayaihusu Tume ya Warioba bali ni baina
ya vyama vya siasa vinavyotaka kujitafutia umaarufu kila kimoja kwa
mtindo wake.
Alipoulizwa ni kwa nini UVCCM iliamua kutoa tamko
linaloashiria kuanza kwa mapambano ya kuhakikisha Katiba hiyo inapita
kwa kupigiwa kura ya ndiyo na Watanzania wote, Makonda alisema: “Mimi
kama msemaji wa UVCCM, hatukuwahi kutoa tamko kama hilo, hii ni
propaganda tu ya wapinzani wetu.” Makonda alisema daima huwa anaamini
katika ukweli na siku zote hupenda kusimamia kile anachokiona kina
masilahi kwa umma wa Watanzania.
Alisema kutokana na msimamo huo, ndio unaomfanya apakaziwe mabaya ili aonekana hafai mbele ya jamii. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“Tanzania hii ya leo kuna watu wako kwa ajili ya
kutengeneza matukio halafu wao wanakaa kando... Binafsi sikumpiga Jaji
Warioba na sitathubutu kufanya hivyo.
“Mimi ninahusika kujenga hoja zenye masilahi kwa
umma na siko kwa ajili ya kujenga hoja za kubomoa, ninajenga hoja za
kulinda na kutetea amani ya nchi na si kuivuruga,” alisema Makonda.
Alisema msimamo huo ndiyo uliosukuma pia kwenda
kuhudhuria mdahalo ule kwa lengo la kusikiliza kile ambacho
kingejadiliwa na kama usingevunjika, alipenda kuchangia hoja ambazo
alikuwa ameziainisha wakati Jaji Warioba alipokuwa akizungumza na kile
alichokizungumza Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph
Butiku.
“Nilitaka kufanya hivyo kwasababu pia mimi ni
mwanasiasa na ni miongoni mwa wajumbe tulioandika hii Katiba
Inayopendekezwa,” alisema Makonda.
Alisema hajisikii vizuri kubambikiziwa kosa ambalo hakulifanya na hatarajii kulifanya.
“Kama Jaji Warioba amekana kuwa hakupigwa katika
vurugu hizo zinazodaiwa kuwa mimi na vijana wangu 23 tulizianzisha, sasa
ni Warioba yupi aliyepigwa na Makonda?” alihoji kada huyo wa Chama cha
Mapinduzi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment