Vyama
vya siasa nchini Burkina Faso vimekubaliana kuwa na uchaguzi mkuu mwezi
Novemba 2015 ikiwa ni harakati za kurejesha utawala wa kiraia na
demokrasia..
Hata hivyo mazungumzo hayo yameisha bila kuwa na
ufumbuzi kuhusiana na nani atakayekuwa kiongozi wa mpito hadi kufikia
muda wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa
aliyekuwa raisi wa taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore.Jeshi la nchi hiyo limekuwa likishikilia madaraka ya tangu aondolewe madarakani kutokana na maandamano ya raia waliokuwa wakishinikiza Rais Compaore.
Umoja wa Afrika jumatatu wiki hii umetoa muda wa wiki moja kufanyika kwa mabadiliko ya utawala na kukabidhiwa kwa wananchi na siyo jeshi tena.
Luten Kanal Isaac Zida ambaye ni kiongozi wa mpito wa kijeshi ameahidi kufuata ushauri huo wa umoja wa Afrika kwa kukabidhi madaraka kwa wananchi ndani ya muda huo wa wiki mbili. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment