Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi kwenye Ufukwe wa Coco kujiandaa na
mchezo dhidi ya Ruvu Shooting juzi jijini Dar es Salaam.
Ni presha kila
kona Simba. Ndivyo unavyoweza kusema wakati kamati ya utendaji ya klabu
hiyo ikikutana leo, kocha Patrick Phiri ameanza upya kuwanoa wachezaji
kwa kuwapeleka ufukweni ili kujenga stamina.
Dharura hiyo ya kikao cha kamati ya utendaji
inaonyesha hali si shwari ndani ya Simba, jambo linalowafanya viongozi
wahangaike ili kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.
Kwa upande wao, viongozi wanawatuhumu baadhi ya
wachezaji kucheza chini ya kiwango, utovu wa nidhamu huku kocha Patrick
Phiri akipewa mtihani wa mechi ili akishindwa, iwe sababu ya kutimuliwa.
Mashabiki wengi wa klabu hiyo wanaamini kuwa kocha
anaonewa, tatizo lipo kwa uongozi unaotakiwa kujichunguza ili kuona
wapi umekosea na kuondoa kasoro zilizopo na si kukimbilia kumlaumu
kocha. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Rais wa Simba ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya
utendaji, Evance Aveva alisema jana kuwa kamati yake inakutana leo
kujadili mwenendo mbovu wa timu pamoja na suala la kocha na wachezaji
waliosimamishwa.
Wachezaji waliosimamishwa, Amri Kiemba, Shaaban Kisiga na Haroun Chanongo, wanadaiwa pia kuhusika na utovu wa nidhamu.
“Kamati ya Utendaji itakutana Jumatano (leo) ili
kuamua hatima ya wachezaji na kesho tutatoa majibu, waendelee na adhabu
au la,” alisema Aveva.
Kuhusu mwenendo wa sare za timu hiyo msimu huu,
Aveva alisema hiyo ni sehemu ya mchezo na klabu yake siyo ya kwanza
kupata matokeo hayo, ijapokuwa si mazuri, wala si mabaya.
Pamoja na Aveva kukubali matokeo, uongozi wake
umempa Phiri mechi mbili akiwa amebakiza moja dhidi ya Ruvu Shooting
Jumamosi ili kunusuru kibarua chake.
Baada ya sare na Mtibwa Sugar, Jumamosi iliyopita,
Phiri ameamua kuwarudisha mazoeni wachezaji wake, safari hii ufukweni
ili kuwaongezea stamina.
Alisema kikosi chake kinacheza vizuri kwa muda
mfupi, kadri muda unavyokwenda, kipindi cha pili wachezaji huchoka,
kuwaruhusu wapinzani kutawala na kusawazisha mabao.
“Nimeona kuna tatizo la kukosa stamina, jambo
ambalo limekuwa likitugharimu, kipindi cha pili, kwani mara nyingi sisi
huanza kufunga, lakini mabao yanarudi, hicho si kitu kizuri.
“Ndiyo maana nimeamua kuwapeleka wachezaji ufukweni kuwajengea
stamina na kuwaongezea nguvu ili wacheze kwa ufanisi, najua mashabiki
wanaumia kwa matokeo mabaya tunayopata, ninawaomba waendelee kutuunga
mkono kwani bado hatujafanya vibaya, wasichoke, tunawahitaji kwa kiasi
kikubwa ili kuwapa morali wachezaji wafanye vizuri,” alisema Phiri.
Aliyekuwa kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameibuka na kusema, tatizo siyo kocha ni uongozi.
“Phiri ni kocha mzuri ndiyo maana wanamwajiri mara
kwa mara, si mara ya kwanza kuifundisha Simba, angekuwa mbovu
wasingemwomba mara kwa mara awafundishie.
“Kiwango cha wachezaji kidogo, pia umri bado,
Phiri siyo anayefunga, kazi yake kufundisha, kama wachezaji hawafungi
yeye afanyaje?
“Tatizo lipo kwao (viongozi), Aveva na wenzake
wanayajua, wajitathimini kwanza kabla ya kumfukuza Phiri, huo siyo
mwarobaini wa kufanya vizuri wakati viongozi ni wale wale.” Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment