Sunday, December 21, 2014

BIBI AMUUA MJUKUU WAKE KWA KUMTUPA NJE YA BASI

 
Mmoja wa abiria waliokuwamo kwenye basi hilo, Ebenezer Hans alilieleza gazeti hili kwamba mama huyo akiwa miongoni mwa abiria, alikuwa na mtoto wake mwenye umri unaokadiriwa miaka 14 na wajukuu wawili, ambao alikuwa akisafiri pamoja nao. PICHA|MAKTABA  

Jeshi la Polisi mkoani Singida, linamshikilia Nawaridi Saidi (45), mkazi wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kumtupa mjukuu wake Mayasa Meshack (6) kutoka ndani ya gari wakati akisafiri kwenda Kigoma akitokea Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 18, saa 2 usiku katika Kijiji cha Igugumo, wilayani Iramba ambapo mama huyo akiwa kwenye basi aina ya Scania, alifungua dirisha kutoka katika kiti alichokaa na kumtupa Mayasa wakati basi likiwa katika mwendo.

“Mama alikuwa anaenda mkoani Kigoma kwa ajili ya Sikukuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, aliambatana na mtoto wake mwingine ambaye jina bado halijafahamika,” alisema Kamanda Sedoyeka. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

SERIKALI YAONYA DAFTARI LA WAPIGAKURA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mh. Willium Lukuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William Lukuvi, ameonesha kutoridhishwa na utaratibu mbovu unaotumika kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura, kutokana na kuwa na mianya inayoweza kuingiza wasio raia wa Tanzania.
Lukuvi aliyasema hayo jana, wakati alipotembelea kituo cha Bunju A kuangalia uandikishwaji wa wananchi kwa kutumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MITAA 89 KURUDIA UCHAGUZI LEO DAR



Jumla ya mitaa 89 kutoka wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, leo zinatarajiwa kufanya uchaguzi wa marudio wa Serikali za Mitaa kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika Desemba 14 mwaka huu.

Moja ya kasoro hizo ni kuchanganywa kwa majina ya wagombea wa uenyekiti na wajumbe.

Manispaa ya Temeke ina mitaa 10, Kinondoni 16 na Ilala 63 .

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, ameingia kwenye mvutano mkubwa na Chama cha Wananchi (CUF), kuhusu uamuzi wake wa kutaka uchaguzi urudiwe katika Mtaa wa Mwinyimkuu huku ikidaiwa chama hicho kilishinda.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 21, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

AFUNGULIWA MASHTAKA KWA KUSABABISHA KIFO CHA PUNDA...!!!

pua 
Mwanaume mmoja nchini Hispania amefunguliwa mashtaka ya kutesa wanyama baada ya kusababisha kifo cha punda aliyemuua wakati akimkalia kwa lengo la kupiga nae picha.
Sabu ya kifo cha punda aliejulikana kwa jila na Platero inasemekana ni uzito uliopitiliza wa mwanaume huyo na kusababisha kumpa maumivu makali mnyama huyo hadi alipopoteza maisha baada ya siku tatu.
dd
Picha hiyo iliwekwa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 38 akitabasamu huku akipiga picha na mnyama huyo.
Baada ya siku mbili Punda huyo aliyekua akiugulia maumivu alishindwa kusimama na baada ya uchunguzi wa Polisi aligundulika kuvunjika baadhi ya viungo vyake kutokana na kubeba kitu kizito. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

POLISI WAWILI WAUAWA MAREKANI

Eneo la mauaji ya polisi wawili mjini New York nchini Marekani.
 
Maafisa wawili wa polisi mjini New York Marekani wameuawa kwa kupigwa risasi walipokuwa ndani ya gari lao eneo la Brooklyn.
Kamishna wa idara ya polisi mjini New York Bill Bratton amesema kuwa maafisa hao walilengwa na kuuawa kutokana na sare walizokuwa wamevaa.
Alisema kuwa awali mwanamume huyo alikuwa ameandika ujumbe wa kuwashutumu polisi kwenye mtandao wa kijamii baada ya kumfyatulia risasi na kumjeruhi vibaya mpenzi wake wa zamani .
Mauaji hayo ya polisi yanajiri wakati kunashuhudiwa ghadhabu kali kufuatia uamuzi wa hivi majuzi wa kutowafungulia mashtaka polisi wazungu waliohusika kwemye mauaji ya waamerika weusi.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

PLUIJM ATOA SIKU SABA (7) KUIBADILI YANGA


Kocha Hans Van Der Pluijm akiwa na Boniface Mkwasa katika moja ya mechi za Yanga Uwanja wa Taifa.

BAADA ya kupewa mkataba wa mwaka moja na nusu kukinoa kikosi cha Yanga kocha Hans van der Pluijm ameomba siku saba kuibadili timu hiyo.

Pluijm alisema atahakikisha anatoa mbinu zake zote alizokuwa nazo za ukocha ili aweze kuipa mafanikio timu hiyo msimu huu ikiwemo kutwaa ubingwa wa Tanzania bara.
Pluijm aliyetua Yanga kwa mara ya pili akichukua nafasi ya Mbrazil Marcio Maximo alisema kwa kuanza atatumia siku saba kwa ajili ya kubadilisha mfumo na kasi ya wachezaji ili waweze kushinda mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa Desemba 28.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

U.S.A YAITAKA KOREA KASKAZINI KUILIPA SONY

Wakuu wa kampuni ya filamu ya Sony Pictures.Marekani imeitaka Korea Kazkazini kuilipa kampuni hiyo kwa hasara iliopata baada ya madai ya kuhusika na uhalifu wa mtandao dhidi yake.
 
Marekani imezitaka China na nchi zingine kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini ilihusika na uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures.
Marekani inasema kuwa Korea Kaskazini ni lazima ikiri kuwa ilihusika na iilipe Kampuni ya Sony kutokana na hasara ambayo imepata
Korea Kaskazini imeyataja madai hayo ya Marekani kuwa ya uongo.
Wataalamu wanasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa Korea Kaskazini ilihusika.
Lakini mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa kampuni ya Sony Pictures nchini Marekani na wakuu wake nchini Japan watahitajika kuamua iwapo wataonyesha filamu ya uchesi yenye utata ya rais wa Korea Kazkazini Kim Jong-un. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

WAPIGA KURA WAHOFIA EBOLA LIBERIA


Uchaguzi wa kuwachagua maseneta nchini Liberia.

Idadi ndogo ya wapiga kura imeripotiwa kwenye kura ya kuwachagua maseneta nchini Liberia.
Kura hiyo ilikuwa imeahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola na huenda hofu ya ugojwa huo iliosababisha watu kukosa kufika kwa vituo vya kupigia kura.
Wapiga kura walishauriwa kusimama umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine walipokuwa wakipanga milolongo kupiga kura baada ya viwango vyao vya joto kuchukuliwa na maafisa wa afya.

Uchaguzi wafanyika nchini liberia licha ya idadi ndogo iliojitokeza kwa hofu ya kuambukizwa Ebola.
Kwenye taifa jirani la Guinea waandamanaji waliwazuia wafanyikazi wa shirika la madaktari wasio na mipaka MSF kuweka kituo cha ebola kusini mwa nchi hiyo.
Polisi wanasema kuwa mahema yalichomwa na wafanyikazi wakafukuzwa na megenge ya vijana.
Jamii kwenye sehemu zingine za magharibi mwa afrika zilipinga jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zikihofia kuwa huenda zikapata maambukizi kutoka kwa wafanyikazi wa kutoa huduma za afya. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC

MOHAMMED ALI ALAZWA HOSPITALINI

 Aliyekuwa bingwa wa ndondi duniani Mohammed Ali na Mwanawe leila Ali.Bondia huyo mkongwe amelazwa hospitalini akiugua maambukizi ya mapafu. 
 
Aliyekuwa bingwa wa ndondi ulimwenguni Mohammed Ali amelazwa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya mapafu.
Ali ambaye ana umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa wa Parkinson anadaiwa kuwa katika hali imara .
Msemaji wake amesema kuwa ugonjwa huo uligunduliwa mapema.
Mohammed Ali wakati wake alipokuwa bingwa wa ndoni duniani.
Hatahivyo hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo mkwongwe kuheshimiwa.
Ali alipataikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984,miaka mitatu baada ya kuustafu katika masumbwi.
Alionekana hadharani katika sherehe moja mnamo mwezi Septemba nyumbani kwake Louisville Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinaadamu za bondia huyo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

REAL MADRID NDIO CLUB BINGWA DUNIANI

Real Madrid washerehekea ushindi wao wa kombe la kilabu bingwa duniani baada ya kuinyuka kilabu ya marekani kusini San Lorenzo 2-0 katika fainali iliochezwa nchini Morrocco. 
 
Kilabu ya Real Madrid imeshinda taji lao la nne mwaka 2014 baada ya kuwashinda mabingwa wa Marekani Kusini kutoka Argentina San Lorenzo katika fainali la za kilabu bingwa duniani zilizochezwa nchini Morrocco.
Mabingwa hao wa kombe la kilabu bingwa barani ulaya,Copa Del Rey na mabingwa wa Super Cup barani Ulaya walianza kufunga kupitia kichwa cha Sergio Ramos.
Makosa ya mlinda lango wa Lorenzo yaliihakikisha ushindi Real madrid baada ya Gareth Bale kuongeza bao la pili.
Real madrid hawakutatizwa na mabingwa hao wa Marekani kusini na hivyobasi kuongeza rekodi yao ya ushindi katika mecho zote kufikia 22.
Ushindi huo pia ni wa kwanza wa kilabu hiyo Bernabeu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...