Sunday, December 21, 2014

MOHAMMED ALI ALAZWA HOSPITALINI

 Aliyekuwa bingwa wa ndondi duniani Mohammed Ali na Mwanawe leila Ali.Bondia huyo mkongwe amelazwa hospitalini akiugua maambukizi ya mapafu. 
 
Aliyekuwa bingwa wa ndondi ulimwenguni Mohammed Ali amelazwa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya mapafu.
Ali ambaye ana umri wa miaka 72 na ambaye ana ugua ugonjwa wa Parkinson anadaiwa kuwa katika hali imara .
Msemaji wake amesema kuwa ugonjwa huo uligunduliwa mapema.
Mohammed Ali wakati wake alipokuwa bingwa wa ndoni duniani.
Hatahivyo hakutoa maelezo zaidi na kutaka haki ya faragha ya familia ya bondia huyo mkwongwe kuheshimiwa.
Ali alipataikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka 1984,miaka mitatu baada ya kuustafu katika masumbwi.
Alionekana hadharani katika sherehe moja mnamo mwezi Septemba nyumbani kwake Louisville Marekani wakati wa kutoa tuzo za kibinaadamu za bondia huyo. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...