Sunday, December 21, 2014

PLUIJM ATOA SIKU SABA (7) KUIBADILI YANGA


Kocha Hans Van Der Pluijm akiwa na Boniface Mkwasa katika moja ya mechi za Yanga Uwanja wa Taifa.

BAADA ya kupewa mkataba wa mwaka moja na nusu kukinoa kikosi cha Yanga kocha Hans van der Pluijm ameomba siku saba kuibadili timu hiyo.

Pluijm alisema atahakikisha anatoa mbinu zake zote alizokuwa nazo za ukocha ili aweze kuipa mafanikio timu hiyo msimu huu ikiwemo kutwaa ubingwa wa Tanzania bara.
Pluijm aliyetua Yanga kwa mara ya pili akichukua nafasi ya Mbrazil Marcio Maximo alisema kwa kuanza atatumia siku saba kwa ajili ya kubadilisha mfumo na kasi ya wachezaji ili waweze kushinda mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa Desemba 28.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Najisikia furaha sana kuwa kocha wa Yanga kwa mara ya pili ni heshima kubwa waliyonipa kwasababu hii ni timu yenye uwezo mkubwa wa kuajiri kocha kutoka bara lolote lakini imeamua kunirudisha mimi kulitambua hilo nimedhamiria kutoa kila nilicho nacho kiufundi kwa ajili ya kuijenga Yanga mpya, alisema Pluijm.
Pluijm alisema anaamini kazi yake haitakuwa ngumu kutokana na ubora wa wachezaji wanaounda kikosi hicho ambao wengi wao walikuwepo kabla hajaondoka nchini kujiunga na klabu ya Al Shaula ya Saudi Arabia hivyo amewataka kuwa na utulivu huku wakisubiri kuanza kuona kazi yake Desemba 26.
“Nimeiona Yanga ikicheza msimu huu ni kweli imeshuka kidogo lakini haitakuwa kazi kubwa kuirudisha katika kiwango chake ndiyo sababu nikatoa siku saba nikiamini haitakuwa kazi kuirudisha katika kiwango cha awali kutokana na mbinu zangu nitakazozitumia,” amesema Pluijm.
Pluijm alisema atakapofanikiwa kuirudisha timu hiyo kwenye kiwango chake kitu ambacho kitafuatia ni kupigania ubingwa wa kwani ameona hakuna tofauti kubwa ya pointi kati yao na timu inayoongoza ligi Mtibwa Sugar.
“Nimeona kuna tofauti ya pointi mbili kati ya Yanga na Mtibwa Sugar ni kitu kizuri kwangu kwasababu kazi yetu kubwa itakuwa kuhakikisha tunashinda kila mchezo wetu ili kukimbizana na wanaoongoza ligi Mtibwa Sugar.
Pluijm amewataka mashabiki wa Yanga kusahau machungu ya kufungwa na watani zao Simba Jumamosi iliyopita kwenye pamla Nani Mtani Jmebe 2 na kuendelea kuwapa sapoti wachezaji wao ili waweze kufanya vizuri katika ligi inayotarajia kuendelea Desemba 26 mwaka huu.  Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...