Thursday, November 14, 2013

MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 14, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
.

LIST MPYA YA MATAJIRI 50 AFRIKA, WATANZANIA WAKO WANNE

dangote
Mtandao wa Forbes maarufu kwa kutoa taarifa kama hizi, umetoa list mpya ya matajiri 50 kutoka Africa na kuhusisha vyanzo vya pesa zao, umri wao pamoja na kiasi cha pesa wanachomiliki.
List imeongozwa na Mnigeria Aliko Dangote (kwenye picha hapo juu) na mtanzania wa kwanza ameonekana kwenye namba 27 akiwa na utajiri wa dola bilioni moja. Cheki list yote hapa.
Watanzania hawa wanne ni Rostam Aziz kwenye namba 27, Reginald Mengi namba 34, Bakhresa namba 38 na Mohammed Dewji namba 38.

1
2
3
4
5

MZEE MIAKA 80 AJIUA KISA WIVU WA MAPENZI, MKEWE ADAIWA KUTEMBEA NA MWANAYE WA MIAKA 12


Mke wa marehemu, Asha Ali (50) anayetuhumiwa kutembea na mwanaye wa miaka 12.

Stori: Gladness Mallya na Chande Abdallah
AMA kweli duniani kuna mambo! Mzee Juma Kondo (80) mkazi wa Mkuranga mkoani Pwani amejiua kwa kunywa dawa ya macho hivi karibuni kutokana na wivu wa kimapenzi, Risasi Mchanganyiko limefukunyua.


Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo jirani na familia hiyo, mzee Juma na mkewe, Asha Ali (50) walikuwa na mgogoro wa muda mrefu uliotokana na mambo ya mapenzi.
Mzee huyo alikuwa akimtuhumu mkewe kutembea na mtoto wao wa mwisho ambaye ana umri wa miaka 12 (jina kapuni).
“Mpaka marehemu anachukua uamuzi wa kujiua, mgogoro mkubwa kati yao ulikuwa ni kumlalamikia mkewe kutembea na mtoto wao huyo anayesoma darasa la tano,” kimesema chanzo hicho.

Waandishi wetu walizungumza na mke wa marehemu, Asha ambaye alikiri mumewe kujiua kutokana na wivu huo wa mapenzi.
“Ndani ya ndoa yetu tulikuwa na mgogoro na mume wangu alikuwa akinituhumu kutembea na mwanangu kitu ambacho hakikuwa cha kweli, binafsi siwezi kulala na mwanangu kwa sababu mimi siyo kuku.

Mtoto wa mwisho wa marehemu mwenye umri wa miaka 12 anayesoma darasa la tano anayetuhumiwa kutembea na mama'ke.

MAELEZO MAPYA ALIYOYATOA MOHAMED MORSI JINSI ALIVYOPINDULIWA EGYPT.

Morsi 1 
Rais Mohamed Morsi aliepinduliwa madarakani nchini Misri July 2013 amesema alitekwa nyara na wanajeshi ambao ndio walimtoa kwenye madaraka ambapo kikundi cha wanasheria waliojitolea ambao hawako kwenye upande wa Morsi, wametangaza hii baada ya kukutana na Morsi gerezani.

Rais huyu aliepinduliwa anataka kulishtaki jeshi na anasema hakutakua na utulivu Misri mpaka hawa watu waliompindua watolewe na wale waliohusika na umwagaji damu za Wamisri  watakapowajibishwa.
morsi gerezani

FUTURE YOUNG TAIFA STARS YAICHAPA TAIFA STARS 1-0 ANGALIA ILIVYOKUWA


Mshambulia wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa (kulia) akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars, Kabanda katika mchezo kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Kiungo wa Taifa Stars, Athuma Idd "Chuji" akichuana na mchezaji wa Future Young Taifa Stars,Paul Nonga.

ALIYEMUUA GWIJI LA SHERIA YA KATIBA DAKTA MVUNGI AKAMATWA DAR

kova1 e15c3
Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova.

Na Damas Makangale, Moblog
Siku moja baada ya nguli ya sheria za katiba nchini, Dakta Sengodo Mvungi kuaga dunia nchini Afrika Kusini, Jeshi la Polis Kanda Maalum Ds, linamshikilia mtuhumiwa mmoja John Ikondia Mayunga (56) kwa kosa la kushiriki kikamilifu kwenye mauaji ya mwanasheria huyo na mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda Maalum Dsm, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Suleiman Kova amesema mtuhumiwa huyo ni mkazi wa kiwalani walipata taarifa kwa raia wema kwamba alishiriki kikamilifu kwenye tukio hilo lilosababisha kifo cha Dakta Sengodo Elibariki Mvungi.

"mnamo tarehe 12/11/2013 Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema kwamba kuna mtu ambaye amehusika na tukio la mauaji ya Dakta Mvungi na kwamba kipindi hicho mnamo saa 12 jioni mtuhumiwa alikuwa maeneo ya mtaa wa Twiga Jangwani akiwa anaangalia Televisheni," amesema Kamishina Kova. Marehemu Dakta. Sengodo Mvungi.

CCM YATOA POLE MSIBA WA DR.SENGONDO MVUNGI


 KINANA_MKUTANO_WA_SHIRIKISHO_LA_CCM_VYUO_VIKUU_MORO_PIX_NO_2_529d1.jpg
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana amesikitishwa na taarifa ya kifo Cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea Jana katika Hospitali ya Millpark nchini Afrika ya Kusini.

Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu anawapa pole wanafamilia, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na Uongozi wa Chama Cha NCCR-Mageuzi. Hakika Taifa limepoteza Mtaalamu wa Sheria, Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi ambacho mawazo yake yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa hili.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.

Imetolewa na:
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
13/11/2013
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr Sedondo Mvungi ambacho kimetokea katika hospitali ya Millpark nchini Afrika kusini.

Uongozi wa UVCCM Taifa unatoa pole kwa familia na ndugu wa marehemu, pia UVCCM inatoa pole kwa uongozi wa NCCR- Mageuzi na kwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Warioba pamoja na Vijana nchini kote ambao wamenufaika na Utaalamu na mafunzo. 
Kama vijana tulihitaji sana mchango wa mawazo, hekima na utaalamu kutoka kwake, hakika tumepoteza kiongozi shupavu, muadilifu na mzalendo ambae ni mfano wa kuigwa kwa Vijana wa Taifa hili.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...