Thursday, May 15, 2014

IJUE HISTORIA YA KAMPUNI YA MABASI YA SCANDINAVIA EXPRESS ILIYOLETA HESHIMA KWA TAIFA...!!!


Kampuni ya mabasi ya Scandinavia Express ni kampuni pekee ya kitanzania iliyowahi kutokea kwa kuwa na huduma za uhakika na za viwango vya hali ya juu kabisa kulinganisha na huduma zinazotolewa na kampuni za sasa. Kampuni hii ilijijengea jina kubwa na sifa nzuri ndani na nje ya nchi kwa huduma bora walizokuwa wakizitoa kwa abiria wake na pia kuliletea sifa taifa la Tanzania kwa kujulikana kuwa na mabasi ambayo ni quality na high class.

Kampuni ya Scandinavia ilianzishwa zaiidi ya miaka thelathini na tano (35) iliyopita ikiwa na mabasi machache tu aina ya LEYLAND  na ilipofika mwaka 1982 kwa mara ya kwanza Scandinavia walinunua basi lao la kwanza la kisasa kutoka kampuni ya SCANIA TANZANIA COACHES aina ya SCANIA ambalo kutokana na ubora  wake na uzuri wake kwa kipindi hicho waliamua kulitumia kwa safari yao mpya waliyoianzisha ya Dar es salaam hadi Iringa.
BASI LA KWANZA LA KISASA KUNUNULIWA NA SCANDINAVIA 1982
Kadiri mahitaji ya usafiri yalivyokuwa yakiongezeka ndipo michirizi ya rangi ya BLUU,KIJIVU na NYEKUNDU ikaanza kuonekana katika mabasi mengi zaidi yaliyokuwa yakisafirisha abiria karibia kila kona ya Tanzania.
Ilipofika mwaka 2001 kampuni ya Scandinavia walianzisha safari yao ya kwanza kabisa kutoka nje ya nchi kwa safari ya Dare es salaam hadi Nairobi nchini Kenya,ambapo mafanikio ya ruti hiyo yalipelekea kuzaliwa kwa ruti nyingine kati ya Nairobi hadi Mombasa na Mombasa hadi Dar es salaam. Katika mwaka wa 2002 kampuni ya Scandinavia walipanua wigo wa huduma zao kwa kuanza ruti mpya ndani ya Afrika mashariki kwa safari za Dare es salaam hadi Kampala nchini Uganda.
Ilipofika mwaka 2003 kampuni ya Scandinavia ilipanua wigo zaidi kwa kuanza kwenda katika mji mkuu wa nchi ya Zambia Lusaka. Wakati huo wote kampuni ya Scandinavia ilikuwa chini ya mkurugenzi na mwanzilishi wake MR.MUHAMED ABDULLAH. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Kampuni ya Scandinavia ilianza kutumia mabasi ya kisasa mwaka 1982 na kuanzia hapo walikuwa wakiongeza mabasi kadili ya mahitaji ya kampuni na abiria pia na kufikia jumla ya mbasi 100 ambayo yalikuwa yakitoa huduma za usafiri ndani na nje ya nchi na mengi ya mabasi hayo yalikuwa ni ya kisasa yaliyonunuliwa kutoka kiwanda cha SCANIA na MARCOPOLO kilichopo nchini BRAZILI.
KWA HISTORIA HII FUPI YA KAMPUNI YA SCANDINAVIA WAMILIKI WA MABASI WANATAKIWA AJIFUNZE KUWA NA HUDUMA BORA NA ZA VIWANGO VYA HALI YA KUMFANYA ABIRIA ASINUNG'UNIKE .
TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA MABASI YA KAMPUNI YA SCANDINAVIA HAPA CHINI!


Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
















Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz














Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

























Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Chanzo: Tanzania Bound Buses Blog

3 comments:

Anonymous said...

No one can provide such service. We all miss this quality service.

Anonymous said...

Kampuni iliyokuwa inajali wateja wake kwa kila njia

Anonymous said...

Serikali ingewatazama wawekezaji wazawa kama hawa

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...