Monday, November 03, 2014

WARIOBA AWASUTA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KWA NYERERE, VURUGU ZAIBUKA...!!!

   Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba alihutubia katika mdahalo huo.

 Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba jana alivamiwa na kikundi cha watu wachache waliohudhuria mdahalo wa Katiba wakati akihoji vitendo vya baadhi ya watu kutumia vibaya jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Jaji Warioba, ambaye alikuwa msemaji mkuu kwenye mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alikuwa akihitimisha hotuba yakle aliyoianza saa 9:15 alasiri, kwa kuhoji kuhusu watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Nyerere kupitisha hoja zao katika misingi isiyokubalika.
 Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba akijaribu kijiokoa mara baada ya vurugu kuzuka

Vurugu hizo zilidumu kwa takriban dakika 45 ndani ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wasaidizi wa waziri huyo mkuu wa zamani, walimtoa ukumbini dakika 30 baada ya sakata hilo kuanza, hali iliyowapa nafasi vijana hao walionekana kujiandaa kufanya vurugu, kumsogelea na kumpiga.
Baadhi ya watu walionekana kumzonga Jaji Warioba ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ni pamoja na aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda. 
Baada ya tukio hilo, polisi waliokuwa na silaha na wakiwa wamevalia nguo za kiraia walimtoa Jaji Warioba ukumbini. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 03, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ANGALIA PICHA ZA JAJI WARIOBA AKIJIOKOA KATIKA VURUGU ZILIZOZUKA KWENYE MDAHALO WA KUJADILI KATIBA

Jaji Joseph Warioba akitoa mada. 
Mtoa mada katika mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa, Jaji Joseph Warioba akitoa mada kabla ya mkutano huo kuvunjika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Saam leo.
Baadhi ya vijana walioingia na mabango ndani ya ukumbi wa mkutano wakiwa na mabango yaliyokuwa yakisomeka ‘Katiba inayopendekezwa tumeipokea tunaiunga mkono’.
Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani. 
Jaji Joseph Warioba akiangalia usalama wake kabla ya kuondolewa mlinzi wake katika ukumbi wa Ubungo Plaza ambapo mdahalo wa kuijadili Katiba inayopendekezwa ulikuwa ukifanyika kabla ya kuvunjika. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HII KALI: MWANAMKE AISHI KINYUMBA NA WANAUME WAWILI KWA MIAKA NANE BILA KUTAMBUANA...!!!

 Juliana Josia(22)kushoto anaedaiwa kuishi na wanaume wanaume wawili kwa zaidi ya miaka 8 bila kutambuana akiwa na Mume wake halisi Rogers ofisini kwa mtendaji

 Juliana Josia(22)kushoto akiwa na barozi Dinde 

Bwana Rogers akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa kwenda kituo cha polisi

Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juliana Josia(22)amezua utata hivi karibuni baada ya kugunduliwa akishi na wanaume wawili kwa muda wa miaka minane bila wanaume hao wawili  kujitambua. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WARIOBA ADHALILISHWA KATIKA MDAHARO WA KATIBA...!!!


Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu

Katika mazingira ya kutatanisha, jana Jumapili Novemba 02, mwaka huu vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni za hapa nchini  ulivurugika kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Vijana hao ambao haijajulikana walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka salama nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo jijini Dar Es Salaam, lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu vingine. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MSIMAMO WA VODACOM PREMIER LEAGUE (VPL) KWA SASA

 
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE MASHALI, KAONEKA WASHINDA KWA K,O

Bondia Shabani Kaoneka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ramadhan Alfani wakati wa mpambano wao Kaoneka alishinda kwa K,O ya Raundi ya kwanza 
Shabani Kaoneka akinuliwa kuwa mshindi. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAANDAMANO ZAIDI YAFANYWA BURKINA FASO

Jeshi la Burkina Faso limefyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji nje ya kituo cha utangazaji cha taifa katika mji mkuu, Ouagadougou.
Ripoti zinasema kuwa risasi zilifyatuliwa punde baada ya kiongozi wa upinzani, Sara Sereme, kuwasili pamoja na wafuasi wake.
Wanajeshi waliwatawanya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika katika medani kuu mjini Ouagadougou.
Vyama vya upinzani vinataka iwekwe serikali ya muda ya raia hadi uchaguzi wa rais utapofanywa.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa mjini humo, Mohamed ibn Chambas, ameonya kuwa Burkina Faso inaweza kuwekewa vikwazo iwapo jeshi litaendelea kuongoza nchi. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...