Monday, November 03, 2014

WARIOBA AWASUTA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KWA NYERERE, VURUGU ZAIBUKA...!!!

   Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba alihutubia katika mdahalo huo.

 Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba jana alivamiwa na kikundi cha watu wachache waliohudhuria mdahalo wa Katiba wakati akihoji vitendo vya baadhi ya watu kutumia vibaya jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Jaji Warioba, ambaye alikuwa msemaji mkuu kwenye mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alikuwa akihitimisha hotuba yakle aliyoianza saa 9:15 alasiri, kwa kuhoji kuhusu watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Nyerere kupitisha hoja zao katika misingi isiyokubalika.
 Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba akijaribu kijiokoa mara baada ya vurugu kuzuka

Vurugu hizo zilidumu kwa takriban dakika 45 ndani ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wasaidizi wa waziri huyo mkuu wa zamani, walimtoa ukumbini dakika 30 baada ya sakata hilo kuanza, hali iliyowapa nafasi vijana hao walionekana kujiandaa kufanya vurugu, kumsogelea na kumpiga.
Baadhi ya watu walionekana kumzonga Jaji Warioba ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ni pamoja na aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda. 
Baada ya tukio hilo, polisi waliokuwa na silaha na wakiwa wamevalia nguo za kiraia walimtoa Jaji Warioba ukumbini. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Makonda na Amon Mpanju, ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, nao waliokolewa na polisi kutokana na vijana walioonekana kumuunga mkono Jaji Warioba kuwatuhumu kuhusika kwenye vurugu. Makonda aliambulia kipigo na kulazimika kujificha katika moja ya ofisi zilizopo hotelini hapo.
Mbali na Jaji Warioba, wajumbe wenzake wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambao ni Humphrey Polepole, Profesa Paramagamba Kabudi, Profesa Mwesiga Baregu, Awadhi Said na Ester Mkuchu nao walitolewa kwenye ukumbi huo na kupelekwa katika chumba maalum hotelini hapo.
Akitolea mfano watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Nyerere kiasi cha kuwashangaza hata wale waliowahi kuishi naye kwa karibu, Jaji Warioba alihoji iwapo Mwalimu Nyerere angekuwa hai angekubali mambo haya yapite.
Baadhi ya mambo aliyodai kuwa hata Mwalimu Nyerere asingeweza kuyapinga ni miiko ya uongozi, viongozi kupokea zawadi na kuzimiliki.
“Watu walimuandikia barua Mwalimu Nyerere kumshawishi kuwa fedha zake zitakuwa salama kama ataziweka nje ya nchi, siyo kama alikataa tu, alitangaza jambo hilo katika vyombo vya habari,” alisema.
Huku akizungumza kwa mtindo wa kuuliza swali Jaji Warioba alisema: “Nauliza, hivi, Mwalimu Nyerere angekataa miiko ya uongozi isiingizwe katika katiba? Angekubali watu wawe na akaunti nje ya nchi? Watu wapate zawadi wakae nazo? Labda huyo si Mwalimu.”
Jaji Warioba, ambaye alianza kushangiliwa kwa nguvu baada ya kuzungumza mambo hayo, alisema: “Kwa sisi tunaomjua vizuri Mwalimu, tunajua kuwa ndio yuleyule ambaye alilipitia Azimio la Arusha lililokuwa msingi wa utu na kutoona hata sehemu moja yenye makosa ya kurekebisha.”
Mifano hiyo iligeuka ‘mwiba mchungu’ kwa baadhi ya waliohudhuria mdahalo huo ambao walionekana kujiandaa kutokana na kwenda ukumbini hapo na mabango yanayoonyesha kukubali Katiba Inayopendekezwa.
Baada ya mneno hayo, watu hao walisimama na kunyanyua mabango yaliyokuwa yamebeba ujumbe mbalimbali, ukiwemo “Katiba Inayopendekezwa tumeipokea na tumeikubali”.
Kitendo hicho kiliwakera baadhi ya washiriki kwenye mdahalo huo ambao walisimama na kuanza kuwakamata waliokuwa wamebeba mabango hayo na kuanza kuyachana.
Licha ya Jaji Warioba na mshehereshaji wa mdahalo huo, Said Kubenea kuwataka washiriki kutulia, vurugu zilizidi na kudumu kwa dakika 45 huku viti vikirushwa kutoka upande mmoja kwenda mwingine na kusababisha watu kukimbia hovyo.
Wakati washiriki wakikimbilia nje, walikutana na polisi ambao walipiga mabomu ya machozi ya kuwafanya baadhi yao kurejea ndani ya hoteli hiyo.
Baada ya hali kutulia Joseph Butiku, ambaye ni mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alirudi ukumbini na kueleza kuhuzunishwa na kilichotokea na kufafanua kuwa kutokana na hali ya kiusalama ni vyema mkutano huo ukaahirishwa.
Akizungumza kwa masikitiko, Butiku alisema: “Hata enzi za Nyerere aliwahi kupita katika wakati mgumu. Lakini haikuwahi kufikia hatua ya watu kupigana ngumi na mateke na kurushiana viti kama tuliyoshuhudia hapa. Kutokana na aibu iliyotokea leo, kwa nia njema ya kuzuia lisije tokea jingine zaidi, tunaahirisha mdahalo huu kwa ajili ya kwenda kujipanga vizuri zaidi.”
Butiku alisema anawafahamu baadhi ya watu walioandaa vurugu hizo na kusisitiza kuwa watu wa aina hiyo hawataruhusiwa kushiriki kwenye midahalo hiyo ambayo itaendelea kuwepo katika maeneo mengi ya nchi ili kutoa fursa kwa wananchi kujadili namna ya kupata katiba iliyo bora.
Mpaka gazeti hili linaondoka hotelini hapo, Makonda alikuwa hajatoka eneo ambako inadaiwa alijificha huku Jaji Warioba akiondolewa chini ya ulinzi mkali.
Alipotoka eneo la nje ya hoteli hiyo, Jaji Warioba alikumbana na umati mkubwa wa watu ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu na kumuita kuwa ndio rais ajaye wa Tanzania. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Kabla ya vurugu
Shangwe, vifijo na nderemo zilitawala kutoka kwa zaidi ya watu wengi waliohudhuria mdahalo huo wakati Jaji Warioba na wenzake walipokuwa wakiingia ukumbini saa 9:00 alasiri.
Kabla ya Jaji Warioba kuanza kuzungumza katika mdahalo huo ambao pia ulihudhuriwa na makada wa CCM na Chadema, Butiku alisema: “Hayawi hawayi, sasa yamekuwa. Tume imeshamiliza kazi na Bunge nalo lmeshamaliza kazi yake. Lengo ni moja tu, ni maendeleo yetu sote.”
Aliongeza: “Sasa tujadili kwa utulivu kwani hatusimamiwi na makundi na badala yake tunaijadli Katiba kwa sheria, hakuna kutishana, kuogopa mtu wala kusimamiwa na chama na hata shinikizo,”
“Miaka ijayo tusije tukawa kwenye kundi la wajinga na kushindwa kujua tulikuwa tunajadili nini ili tuepuke maswali kutoka kwa wajukuu zetu na watoto pia.’’
Warioba
Kabla ya Jaji Warioba kuanza kuzungumza, mshehereshaji wa mdahalo huo Hamza Kassongo alimuomba atoe jibu kama ni kweli Katiba Inayopendekezwa imebeba asilimia 80 ya maudhui ya rasimu ya Pili ya Katiba.
Jaji Warioba alianza kwa kuifafanua Sheria ya Kura ya Maoni kuwa inamtaka wiki mbili baada ya rais kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa kuitangaza katika gazeti la Serikali na kuiagiza Tume ya Uchaguzi (NEC) kuanza kusimamia mchakato huo.
Pia alieleza kuwa kazi ya kutoa elimu kwa wananchi itakayofanywa na NEC na asasi za kiraia kwa mujibu wa sheria hiyo inatakiwa kufanyika kwa siku 60, baada ya hapo itafanyika kampeni kwa muda wa mwezi mmoja.
“Sheria inasema Kamati ya Kampeni ndiyo itafanya kampeni. Kamati hizo zinakuwa mbili ambazo ni Kamati ya Kitaifa na ya Jimbo. Kamati moja ni ya kuungaa mkono Katiba Inayopendekezwa na ya pili ni ya kupinga, zote lazima zisajiliwe na NEC. Baada ya kampeni NEC itasimamia upigaji kura, kuhesabu na kutangaza matokeo,” alisema.
Jaji Warioba alikosoa utaratibu wa kufanya maboresho daftari la kudumu la wapigakura na kuonyesha wasiwasi wake kama kura ya maoni itaweza kufanyika kama sheria inavyosema kutokana na kamati kutoundwa na muda wa NEC kuwa mdogo.
Katiba Inayopendekezwa
Akigusia Katiba Inayopendekezwa, Jaji Warioba alisema kuna baadhi ya mambo ya muhimu yaliyokuwa katika rasimu ya Katiba yameondolewa
“Katiba Inayopendekezwa haijasambazwa ipasavyo. Tunatakiwa kutotazama wingi au uchache wa ibara, tutazame Katiba ina mabadiliko gani,” alisema.
Aliyataja mabadiliko ambayo hayapo katika Katiba ya sasa lakini yalikuwepo kwenye Rasimu kuwa ni tunu na maadili na kusisitiza kuwa mambo hayo yalikuwa mapya.
Pia aligusia kuondolewa kwa madaraka ya wananchi katika Katiba Inayopendekezwa, mawaziri kutokuwa wabunge, madaraka ya rais kutopunguzwa, mgombea binafsi kuwekewa masharti mengi, haki mbalimbali kutodaiwa mahakamani, idadi ya wabunge kuongezwa pamoja na muundo wa muungano kuwa unazidisha kero baada ya kuzipunguza. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Mabango, wasemavyo washiriki
Baadhi ya vijana waliobeba mabango ya kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa walilalamikia vurugu walizofanyiwa ukumbini.
“Wamechana mabango yetu… walichokifanya ni kuzuia uhuru wetu wa kutoa mawazo yetu,” alisema mmoja ya vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la John Ndumbaro.
“Warioba anapingana na Katiba Inayopendekezwa, lakini sisi tunaipenda na ndiyo maana tumekuja na ujumbe wa kuielewa, kuipenda na kuikubali.”
Asilimia kubwa ya mabango yalikuwa yanafanana yakiwa na ujumbe wa Katiba Inayopendekezwa tumeielewa, tunaipenda na tunaikubali.
Alipoulizwa iwapo kundi lao ni miongoni mwa wafuasi wanaodhaniwa kutumwa na CCM kuvuruga mdahalo, Ndumbaro alisema nchi inawagusa watu wote na kwamba hawakuwa wafuasi wa chama chochote bali walienda kutetea nchi.
Naye Wagese Wilson alisema kilichotokea pale ulikuwa ni uhuni ambao anaamini ulipangwa na kikundi anachodhani ni cha wana-CCM.
“Kimsingi hizi vurugu ziliandaliwa kwa sababu ulinzi ulikuwepo nje muda wote. Kwa nini baada ya purukushani kutokea zimepita takriban dakika 40 bila polisi kuingia na kumlinda mtu mkubwa kama Warioba?” alihoji.
Mmoja ya washiriki waliokuwa jirani kabisa wakati Warioba akitolewa nje ya ukumbi, William Ndiyekeiya alisema alisikitisha kuona kiongozi mkubwa kama Warioba akikosa ulinzi wa kutosha hasa katika mdahalo wa kitaifa.
“Yule mtu wa CCM alikuwa nyuma ya Warioba huku amemng’ang’ania na askari wa FFU (kikosi cha kutuliza ghasia) aliyekuwa ameingia hakuonyesha hali yoyote ya kutaka kuwatenganisha.
Mlinzi wa Jaji Joseph Warioba (kushoto) akimkinga kwa mikono ili asipate madhara baada ya mdahalo wa kujadili Katiba inayopendekezwa kuvamiwa na kundi la vijana na kusababisha uvunjifu wa amani.
“Hili ni tatizo la serikali la kushindwa kuleta ulinzi mapema…dakika 45 baada ya vurugu ndiyo wanaleta askari ndani! Lazima watambue kuwa Watanzania wa sasa siyo sawa na wale wa mwaka 1977 au 1982,” alisema Ndiyekieya.
Mpango wa Vurugu ulipangwa
Mmoja wa Wanafunzi wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WMDI) ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa ajili ya usalama wake, alisema kuwa juzi usiku kulikuwa na ujumbe mfupi uliokuwa ukisambazwa ukitaka kujiandaa na mdahalo.
“Nilipokea ujumbe uliokuwa unatutaka leo muda wa saa 6:30 kuja Ubungo Plaza na nauli zingetolewa… baadaye kidogo ujumbe huo ulieleza kwamba hatukutakiwa kwenda na nguo za kijani wala njano kwa sababu kulikuwa na shughuli maalumu,” kilisema chanzo hicho.
Alipouliza mtu aliyekuwa anawasiliana naye, mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu, alijulishwa kuwa aliyetuma ujumbe alikuwa ni mmoja wa viongozi wa chama kimoja chenye tawi chuoni hapo.
“Pale Chuo hakuna matawi ya vyama vingine…na zitazame meseji zote hizi tulizokuwa tunachati akijaribu kutuelekeza namna ya kuandaa ‘kazi hiyo maalumu’,” alisema.
“Hata baada ya kuingia ukumbini nilianza kuwaona wanafunzi wenzangu kidogokidogo ambao walienda kujirundika upande mmoja na baadaye kuanza kuonyesha mabango,” aliongeza huku akimuonyesha mwandishi wetu meseji hizo. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na Mwananchi

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...