Tuesday, July 09, 2013

MBONA MAJANGAAA....!!! AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI

 

HATIMAYE  wale Wanawake wawili walionaswa  na  madawa ya  kulevya  Afrika  kusini wametambuliwa kuwa  ni  mabinti  wa  KITANZANIA ..
Mabinti  hao  wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.
Akizungumza na mwandishi wetu  jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.
Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE)  ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

CHELSEA WAANDAA DAU LA JUU ZAIDI KUMSAJILI ROONEY....!!!



Target: Chelsea are set to launch a bid for Wayne Rooney despite David Moyes saying he is not for saleAnasakwa vibaya sana: Chelsea wameamua kutuma ofa kwa David Moyes ingawa alitangaza kuwa hafanya biashara, lakini wakali hao wa darajani wanamhitaji jembe  Wayne Roonye

Will he stay or will he go? Rooney's future at Manchester United has been debated this summerAtabaki au ataondoka? Maisha ya baadaye ya Rooney katika klabu yake ya  Manchester United bado hayajulikani

New man in charge: David Moyes says he does not want to sell RooneyKocha mpya wa United: David Moyes amesema hamuuzi Rooney kwa sasa

Welcome back, Jose: Frank Lampard and John Terry will be pleased to see the return of Mourinho to Chelsea Karibu tena Jose: Malejendari, Frank Lampard na John Terry wamefurahi kuona ujio wa Mourinho katika klau yao ya Chelsea

WAKATI MZEE MANDELA AKIENDELEA KUPATA MATIBABU FAMILIA YAKE WAZIDI KUTIBUANA



Mandla Mandela aendelea kulikoroga
WAKATI mgogoro kati ya watoto wa Mandela na wajukuu ukizidi kutokota kuhusu uhalali wa uchifu wa Mandla Mandela, yeye amejibu mapigo akisema Mfalme Buyelekhaya Dalindyebo wa kabila la abaThembu ”hana akili timamu”.
Hiyo inatokana na madai yaliyotolewa na mfalme huyo kwamba Mandla hakuwa chifu sahihi wa ukoo wa Madiba. Alidai kwamba hakukuwa na cheti chochote halali kilichotiwa saini wakati mandla alipotawazwa kuwa chifu mwaka 2007 – sherehe ambazo zilisimamiwa na Mandela mwenyewe.
Gazeti la Mail & Guardian wiki iliyopita liliripoti kuwa uchifu wa Mandla ulilalamikiwa kabla ya Mandela kulazwa hospitalini, ikielezwa kama kweli anafaa kuendelea kuwa chofu ikizingatiwa kuwa mama na baba yake walimzaa bila kuoana.
Mgogoro unaoendelea hivi sasa kati ya Manla na shangazio yake, Makaziwe Mandela, na wanafamilia wengine unaonekana kama kichocheo kwa baadhi ya wanafamilia hiyo ambao wangetaka Mandla avuliwe uchifu.

WEMA SEPETU ANASAKWA NA POLISI BAADA YA KUMTUKANA MENEJA WA HOTELI WAKATI YUKO POMBE...!!!



Msanii wa filamu za Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu anasakwa na Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya fujo hotelini, kumtukana matusi ya nguoni na kumpiga makofi meneja wa hoteli hiyo, Godluck Kuyumbu. Songombingo hilo lilijiri saa tano usiku wa Jumatano iliyopita kwenye hoteli hiyo  iliyopo Kawe Beach, jijini Dar. 
Akizungumza na mwandishi wetu , meneja huyo alisema siku ya tukio majira ya saa nane mchana, Wema alifika kwenye mgahawa wa hoteli hiyo akiwa ameongozana na marafiki zake wapatao kumi.


Meneja huyo akaendelea kusema, ilipofika  saa tano usiku, Wema na marafiki zake  walionekana kuzidiwa na kilevi, wakaanza kufanya fujo kwa kupiga kelele, kitendo kilichowakera wateja waliokuwa katika mgahawa huo, wengi wakiwa ni Wazungu ambao waliondoka kutokana na fujo hizo. 


Aliongeza kuwa mmoja wa marafiki wa Wema ambaye ilidaiwa ni mpenzi wake, aliyejulikana kwa jina moja la D, alichukua glasi na kuipasua chini kwa makusudi huku meneja huyo akishuhudia.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Akutana na Waandishi Wa Habari Nakutoa maamuzi ya Kamati ya Ushauri (RCC) ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa mpya Mkwajuni Wilayani Chunya.


  
Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa Mbeya akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu wa mkoa Mbeya akiongea na waandishi wa habari.Picha na Habari na Mdau Joseph Mwaisango
--
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya hatimaye yatoa ufafanuzi na kupigilia Msumari maamuzi ya Kamati ya Ushauri (RCC) ya kupeleka Makao makuu ya Mkoa mpya Mkwajuni Wilayani Chunya.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 10, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

"NGUVU YA UMMA" INAVYOGHARIMU UHAI WA WAMISRI...!!!


 

Miili  ya wafuasi  wa Rais  aliyeondolewa madarakani nchini Misri ikiwa imehifadhiwa
 


 
MAAFISA wa Afya Misri wamesema takriban watu 42 wameuawa kwa kupigwa risasi mjini Cairo nje ya kambi ya kijeshi ambapo wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi walikua wamekusanyika na wanaamini anazuiliwa hapo. Watu wengine 300 wamejeruhiwa.

Kundi la Muslima Brotherhood limewataka raia wa Misri kuwapinga wale linawaita wanaopokonya raia uhuru na demokrasia.

Brotherhood imelaumu jeshi kwa kuwaua raia wake.
Katika kikao na waandishi wa habari, wafuasi hao walimlaani vikali mkuu wa jeshi Abdel Fattah Al-Sisi na kumtaja kama muuaji aliyewashambulia raia wenzake.

Haya yanajiri huku ghasia zikiendelea baada ya kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi.

NDEGE YA RAIS WA SOMALIA 'YASHIKA MOTO'

somali f9f1f
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mahamud
*******
NDEGE iliyokuwa inambeba rais wa Somalia, imelazimika kutua kwa dharura mjini Mogadishu baada ya moja ya mabawa yake kushika moto. (HM)
Msemaji wa Hassan Sheikh Mohamud, alisema kuwa haijulikani kwa nini injini ya ndege ilisita kufanya kazi.
 
Rais Hassan Sheikh Mohamud, alielezea kuwa rais hakujeruhiwa lakini wazima moto walifanya kila hali kuzima moto huo.
Bwana Mohamud alichaguliwa kama rais wa Somalia mwaka jana katika mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa, katika hatua za kumaliza vita vya miaka mingi.
Mwandishi wa BBC Mohamed Mwalimu, alisema kuwa magurugumu ya ndege yaliharibiwa vibaya baada ya tukio hilo.

Rais alikuwa anaelekea katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, wakati ndege hiyo ilipolazimika kurejea Mogadishu.
Moja ya ripoti zilizotolewa za mwanzo kuhusu tukio hilo, ilitoka kwa akaunti ya Twitter ya kundi la al-Shabab lakini haikusema kama imeshambulia ndege hiyo.

 
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika pamoja na wale wa Somalia, wanaounga mkono bwana Mohamud wamewaondoa wapiganaji wa al-Shabab kutoka mji mkuu Mogadishu, mwaka jana ingawa kundi hilo bado hufanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvizia.
Serikali mpya ni ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10 kutambuliwa na serikali ya Marekani na shirika la fedha duniani (IMF). 

Chanzo: bbcswahili

HILI NDILO GHETTO LA DIAMOND THE PLATNUMZ...!!!

Photo by diamondplatnumz
Photo by diamondplatnumz


Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...