Saturday, April 26, 2014

MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

IMG-20140426-WA0034_af1cd.jpg
IMG-20140426-WA0035_686a4.jpg
Umati wa watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea hivi sasa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, maonyesho haya yanajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo maonyesho. Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoaka mataifa mbalimbali (Picha na Awadhi Ibrahim)

G7 YAZIDI KUIBANA URUSI...!!!

Askari wa Ukraine
Viongozi wa nchi Saba tajiri kwa viwanda duniani G7 wamekubaliana kuongeza vikwazo zaidi kwa Urusi ambapo wamesema imezidi kuifanya Ukraine isitawalike.
Ikulu ya White House ya Marekani imesema wataanza kuweka vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo kuanzia siku ya jumatatu na wanatarajia kulenga biashara za binafsi na ambazo zina uhusiano na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Viongozi hao wa G7 wameelezea kuguswa kwa na jinsi Urusi ilivyoshindwa kuacha kuwasaidia wanaoipinga serikali.
Wametoa wito kwa Urusi kuacha mipango yake kijeshi ya siri kwenye mpaka na Ukraine.
Kwa upande mwingine viongozi hao wa nchi saba tajiri duniani wameisifu Ukraine kwa jinsi walivyojizuia kwa kupanda na wapiganaji waasi.
Serikali ya Ukraine imesema inahofia kuwa Urusi ina mipango ya kuivamia. Hata hivyo Urusi imesema nchi za magharibi zina mipango ya kuteka kuitawala nchi yao.

HAKUNA KATIBA BILA UKAWA...!!!

kingunge c2ea5
Na Hudugu Ng'amilo
MWANASIASA mkongwe na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge Ngombale – Mwiru, amesema makada wenzake wanaomshambulia aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, wanakitukana Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kumtukana au kumshambulia Jaji Warioba, au wajumbe wengine wa tume hiyo ni sawa na kukitukana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoongoza serikali.
Kingunge alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akichangia sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya Katiba, ambapo alisema wanaomshambulia Jaji Warioba wanaonyesha utovu wa adabu, kwa kuwa chama kina maadili na adabu katika kushughulikia masuala mbalimbali.
"Mimi sitakubali hata kidogo wajumbe watumie msimamo wa chama kumshambulia Warioba au wajumbe wengine wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, si halali kumshambulia Warioba au mjumbe yeyote yule binafsi.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRIL 26, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

WANASIASA WANNE WAZUIWA KUSAFIRI...!!!


Wanasiasa wakuu waliokuwa wamezuiliwa
Wanasiasa wanne wakuu walioachiliwa na serikali ya Sudan Kusini, wamepokonywa hati zao za usafiri walipokuwa wanajiandaa kuondoka nchini humo kusafiri hadi mjini Nairobi Kenya.
Mke wa marehemu John Garanga, Rebecca Garang, ambaye anashikilia cheo cha juu katika chama cha SPLM , ameambia mwandishi wa BBC Robert Kiptoo kuwa serikali haikutoa sababu ya kuwapokonya hati za usafiri wanasiasa hao.
Serikali ya Sudan Kusini iliwaachilia wanasiasa hao waliokamatwa kwa madai ya kuhusika na njama ya mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais Salva Kiir Disemba mwaka jana.
Waziri wa sheria alisema kuwa serikali ilifutilia mbali kesi dhidi ya wanasiasa hao wanne wakuu waliotuhumiwa kupanga njama ya mapinduzi ambayo yamesababisha vurugu za wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Wanne hao akiwemo aliyekuwa kiongozi wa chama cha SPLM, walikanusha madai ya kuhusika na njama ya mapinduzi, na pia wamekanusha uhusiano wowote na mapigano yanayoendelea nchini Sudan Kusini.

UPIZANI AFRIKA KUSINI WAKOSOA SHIRIKA LA SABC

Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha  Economic Freedom Fighters (EFF).
Shirika la serikali la utangazaji nchini Afrika kusini-SABC limeshutumiwa vikali na chama cha upinzani cha Economic Freedon Fighters-EFF kwa kutumia kile chama hicho kinasema ni mbinu zinazofanana na zile za enzi za ubaguzi wa rangi kwenye matangazo yake.
Lawama hizo zinafuatia hatua ya SABC kukataa kupeperusha tangazo la chama hicho cha kisiasa kama sehemu ya kampeni zake kabla ya uchaguzi mkuu wa Mei 7.
Julius Malema, kiongozi wa chama hicho cha EFF ambaye zamani alikuwa kiongozi wa vijana katika chama tawala cha African National Congress (ANC), alisema kukataliwa kwa tangazo la chama chake cha kisiasa kunahujumu mchakato wa uchaguzi ujao.
Chama cha EFF kitashiriki kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
CHANZO:VOA

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...