Shirika
la serikali la utangazaji nchini Afrika kusini-SABC limeshutumiwa vikali
na chama cha upinzani cha Economic Freedon Fighters-EFF kwa kutumia
kile chama hicho kinasema ni mbinu zinazofanana na zile za enzi za
ubaguzi wa rangi kwenye matangazo yake.
Lawama
hizo zinafuatia hatua ya SABC kukataa kupeperusha tangazo la chama hicho
cha kisiasa kama sehemu ya kampeni zake kabla ya uchaguzi mkuu wa Mei
7.
Julius
Malema, kiongozi wa chama hicho cha EFF ambaye zamani alikuwa kiongozi
wa vijana katika chama tawala cha African National Congress (ANC),
alisema kukataliwa kwa tangazo la chama chake cha kisiasa kunahujumu
mchakato wa uchaguzi ujao.
Chama cha EFF kitashiriki kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment