Monday, May 13, 2013

SIKILIZA NA DOWNLOAD LYRICS YA WIMBO WA ULIOTUMIKA KWENYE TAMTHILIA YA MARA CLARA


https://fbcdn-sphotos-h-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn2/972140_184345635053283_871561002_n.jpg



WHO yasema coronavirus yaambukiza.


Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema inaelekea sana kuwa aina mpya ya virusi vinavouwa, vya coronavirus, vinaweza kuambukizwa baina ya watu walio karibu sana.

Coronavirus
Virusi hivyo ni sawa na vile vya homa ya SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome) na vinamfanya mgonjwa kuwa na shida sana ya kuvuta pumzi.

Nchini Ufaransa mwanamume mwengine hivi sasa ni mahtuti baada ya kuambukizwa na mgonjwa wa mwanzo nchini humo, ambaye walilazwa chumba kimoja hospitali.

Hadi sasa watu 34 wanajulikana kupata ugonjwa huo duniani tangu mwaka wa 2012, 18 kati yao walikufa Saudi Arabia.
WHO inasema ni muhimu kujulisha watu kuhusu virusi hivyo kwa sababu kuna wasi-wasi mkubwa kuwa vinaweza kusambaa.
Chanzo ni BBC Swahili.

MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE KUTANGZWA WIKI HII


Matokeo mapya ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 yanatarajia kutangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi siku yeyote wiki hii. 

Kutangazwa upya kwa matokeo hayo kunafuatia uamuzi uliochukuliwa na serikali hivi karibuni kufuta wa matokeo hayo ili yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. 

Habari ambazo NIPASHE imezipata jana na kuthibitishwa na 
viongozi wandamizi wa wizara hiyo, kazi ya kufanya marekebisho ya matokeo hayo imeshakamilika na yatatangazwa wiki hii. 
“Kazi ya kuandaa matokeo imekwishakamilika sababu ni kazi inayofanywa na watu watatu kwa kutumia kompyuta,” alisema ofisa mmoja ambaye alisema taarifa rasmi zitatolewa na Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.

AFANDE SELE AMSHUKURU MH. ZITTO KABWE KWA KUGHARAMIA VIDEO YAKE, HIKI NDO ALICHOKISEMA


Mapema asubuhi hii Mfalme wa Rhymes Afande Sele ametoa ya moyoni na kuelezea lengo lake la kutunga wimbo wa DINI TUMELETEWA kumrudisha Muafrika kwenye Uafrika na msingi wake wa UMOJA, USHIRIKIANO na UPENDO. Pia hakuwa nyuma kutoa shukrani zake kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe kwa kumuwezesha kugharamia Video ya wimbo wake huo mpya ambao unafanya vizuri sana kwa sasa.


Nanukuu "Lengo la hii kazi yangu mpya DINI TUMELETEWA ni kumrudisha mwafrika kwenye uafrika wake ambao msingi wake ni UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO. Ambao kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia ukitoweka. Tumeona mapigano/mauaji ya itikadi za kidini wenyewe kwa wenyewe, pia kuelezea uhuru wa kuabudu kwa imani yoyote bila kuvunja sheria za Taifa letu. Kwa mtu yoyote makini mwenye mapenzi mema kwa Taifa letu na AFRIKA hawezi kupingana na hilo, kwa kutambua hilo MH; ZITTO ZUBERI KABWE(ZZK) kajitolea kugharamia gharama zote kwa ajili ya kufanikisha vidio bora kabisa ya wimbo huu, hii ni kazi yetu wote mimi na wewe, tunasema asante sana kwa Mh; Zitto. AMANI NA UPENDO KWANZA"

KIFAA CHA CHANJO YA UKIMWI CHAGUNDULIKA


'Ugunduzi huu ni ukombozi katika kuharakisha kupatikana kwa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi' Dk Seif Rashid 
Dar es Salaam. Wanasayansi nchini Marekani wamebaini kifaa kipya kitakachoharakisha upatikanaji wa chanjo ya virusi vya Ukimwi (VVU).
Taarifa kwa Mwananchi Jumapili iliyotolewa Alhamisi wiki hii na Taasisi ya Tafiti Kukabiliana na Magonjwa ya Mzio na Kuambukiza (NIAID) ya nchini Marekani ilieleza kuwa mfumo wa kifaa hicho siyo tu utasaidia kurahisisha chanjo kukabiliana na VVU, bali hata kwa magonjwa mengine yanayosababishwa na virusi kama mafua na yale yanayosababisha uvimbe wa ini.
“Ni mfumo wa hali ya juu wenye uwezo wa haraka wa kuchambua chembechembe kinga zenye uwezo wa kuangamiza aina mbalimbali za VVU zinazopatikana duniani,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliyoambatanisha majina ya wanasayansi nguli wa NIAID ambao wamethibitisha kifaa hicho chenye mfumo mpya katika teknolojia ya kuchambua VVU, umeweka wazi kuwa matatizo waliyokuwa wakipata wanasayansi katika kudhibiti virusi sasa imepata ufumbuzi.
Uzuri wa kifaa hicho unaelezwa kwamba ni kuweza kuchambua na kutofautisha chembe kinga za aina mbalimbali, hata kujua idadi na uwezo wake katika kushambulia adui katika mwili wa binadamu.

MSICHANA WA MIAKA 16 APIGWA RISASI BAADA YA KUKUTWA AKIVUNJA AMRI YA SITA NDANI YA GARI NA MWANAUME JIJINI DAR ES SAALAM



JESHI la polisi limekumbwa na kashfa nyingine baada ya askari wake kudaiwa kumpiga risasi msichana wa miaka 16 baada ya kumkuta akivunja amri ya sita ndani ya gari.
Msichana huyo..
(Jina tunalihifadhi) alikumbana na mkasa huo Jumatano usiku eneo la Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, ambapo alipigwa risasi sehemu ya makalio wakati akijaribu kuwakimbia polisi kwa kutumia gari la mpenzi wake.
Mpenzi huyo (jina linahifadhiwa), alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi ya ubakaji.

Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana katika wodi ya Hospitali ya Temeke alikolazwa, msichana huyo alisema siku ya tukio alikutana na kijana huyo majira ya saa 8:00 usiku katika baa moja inayoitwa Kindau na kukubaliana kwenda kushiriki tendo la ndoa kwa malipo ya Sh 20,000.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 13.05.2013

DSC 0128 4113f

DSC 0133 5b992

DSC 0134 c44ac

DHAMANA YA LWAKATARE LEO


Jopo la mawakili wanaomtetea Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare leo linaanza harakati za kumtoa mahabusu kwa dhamana.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kumfutia Lwakatare mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakimkabili yeye na mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura, ambayo hayana dhamana na kubaki na shtaka moja la kula njama ambalo linadhaminika.

Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2013, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatajwa leo, lakini mawakili wa Lwakatare wamejipanga kumwombea dhamana Lwakatare.

Mmoja wa mawakili wa Lwakatare, Peter Kibatala aliliambia Mwananchi jana kuwa kwa kuwa kosa lililobaki linadhaminika, basi jambo moja watakalolifanya leo ni kuwasilisha maombi ya dhamana.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...