Saturday, March 16, 2013

HEBU ANGALIA WASANII TUNAOWAITA KIOO CHA JAMII


Kuna msemo unasema wasanii kioo cha jamii je ni kweli?hili ni kava linalobeba kazi za wasanii kwa hali kama hii bado tunadhubutu kusema wasanii ni kioo cha jamii? Mimi naona waitwe waharibifu wa jamii kwa halii hii. Hapa watoto wanajifunza nini kwa kweli?

MWANA FA AITAKA SERIKALI IRUDISHE MFUMO WA ANALOGIA

faaa

Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA ambaye March 13 mwaka huu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameiomba serikali kuwafikiria mara mbili mbili wasanii na kuachia mifumo yote miwili ya digitali na analojia kwakuwa mfumo wa digitali unawaumiza.

Akiongea na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini wanaumizwa na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi katika kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache tu wenye ving’amuzi.

“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.

Alisisitiza kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.

BAADA ya UKIMNYA KWA MDA MREFU HATIMAYE AGNESS MASOGANGE ATUPIA PICHA ZAKE INSTAGRAM.AMEPENDEZAJEE


CHECK OUT ALICHOKISEMA LULU KUHUSU MAREHEMU STEVEN CHARLES KANUMBA.

Leo kutoka akaunti ya Twitter ya  msanii wa filamu(Boongomovie) amefunguka na juu ya aliyekuwa mpenzi wake marehemu Steven Charles Kanumba ambae kifo cha mraehemu kilichosababisha yeye kuingia gerezani  sasa hiki ndicho alicho kiandika kupitia ukurasa wake huo wa mtandao wa kijamiaa Twitter 


BASI LA NDENJELA LAUNGUA MOTO LIKIWA SAFARINI MAENEO YA KIBAHA LEO HII


Basi la Ndenjela likiwa linatoka Dar kuelekea Mbeya limeteketea kwa moto Kibaha Kongowe asubuhi ya leo. Abiria wote wamenusurika janga hilo.MIZIGO IMTEKETEA KATIKA JANGA HILO

MASTAA WAANDAA MKESHA KUMUOMBEA KAJALA

Stori: Sifael Paul
ZIkiwa zimebaki siku 8 tu kabla ya hukumu ya staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja kusomwa Machi 25, mwaka huu, inasemekana kuwa baadhi ya mastaa wa filamu na muziki Bongo, wameandaa mkesha wa kumuombea ili hukumu hiyo iende vizuri na aachiwe  huru arudi uraiani.
Kajala anakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu kwa kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kushirikiana na mumewe, Faraji Agustino.
Kwa mujibu wa mwigizaji mmoja maarufu wa kiume, tayari ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na ujumbe kupitia mitandao ya kijamii umeanza kusambazwa kwa baadhi ya mastaa hao ambao kila mmoja anaonesha kuwa tayari kwa ishu hiyo ya kumuomba Mungu amsaidie Kajala.



Mwigizaji huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alidadavua kuwa wanachotafuta kwa sasa ni mahali au nyumba ya ibada kwa ajili ya kufunga na kumwombea Kajala kuanzia saa 2:00 usiku hadi asubuhi.
“Mwanzoni ilikuwa ni kuhamasishana tu kumkumbuka Kajala katika sala zetu za kila siku kama ilivyokuwa kwa Lulu (Elizabeth Michael), lakini sasa tumeona ni vema tukakutana kwa pamoja tumlilie Mungu ili hukumu yake imuendee vizuri,” alisema mwigizaji huyo na kuongeza:

“Yah! Kajala anatia huruma sana ndiyo maana kuna wasanii ambao ni watu wa karibu yake, wapo tayari kwa ajili ya mkesha wa maombi kama (Jacqueline) Wolper, Irene Uwoya, Patcho Mwamba, JB (Steven Jacob), Ray (Vincent Kigosi), Richie (Single Mtambalike), Dude (Kulwa Kikumba) na wengine wengi.”

Katika kesi hiyo iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Kajala amesota Segerea kwa takribani mwaka mmoja ambapo sasa hatma yake itajulikana tarehe tajwa hapo juu. 

CHUCHU HANS: NIMEANZA KUIGIZA TANGU NIKIWA MDOGO

Tangu akiwa mdogo alikuwa anaigiza na kufanya umiss wakati alipokuwa shuleni mkoani Tanga. Chuchu who has acted in many films including Lose Control, Hit Back and Tone la Damu. 

 Mshindi huyo wa taji la Miss Tanzania talent in 2005.Kiukweli mimi toka utotoni nilikuwa na kipaji cha u-miss na kuigiza  nimeanza tangia shule Tanga nilikuwa naigiza maigizo na nafanya fashion shows so naamini nilikuwa na talent that's y nilivyoingia miss Tanzania pia niliweza kutwaa taji la Miss Tanzania Talent Tanzania 2005" . Some of  her upcoming films include Mimba by Chekibud, Safari produced by Rich and her own film Raula.

US Hip Hop Rapper Lil Wayne is Recovering After Seizures.

The hip hop star tweets that he is “good” after suffering a reported seizure that led to claims he was in a coma and near death.
Grammy-winning hip hop star Lil Wayne has said he is recovering and has thanked fans for their concern after he suffered a reported seizure.
 One of the Celebrity news website claimed the star was in critical condition in Los Angeles after being admitted to hospital twice this week.
 In a message from his official Twitter account Lil Wayne said: “I’m good everybody. Thx for the prayers and love.”
 The 30-year-old rapper, who has a history of seizures, was first rushed to Cedars Sinai hospital on Tuesday after suffering multiple episodes, it said.
 He left the following day but was re-admitted hours later.
 His spokeswoman Sarah Cunningham said in an email that “Lil Wayne is recovering,” but did not specify what he was suffering from.
In October last year, the star, who won four Grammy awards in 2008 including best rap song and best rap album, reportedly suffered a number of seizures while on his private jet.

Wazimbabwe wanapiga kura ya maoni leo huku wanachama wa upinzani wakidaiwa kushambuliwa.

Wananchi wa Zimbabwe leo wanapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo itaweka kikomo cha muhula wa urais na kuongeza uhuru wa vyombo vya habari. 
Hata hivyo, wasiwasi umeongezeka baada ya wanachama kadhaa wa chama cha upinzani cha Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai kushambuliwa wakati wakifanya kampeni katika kitongoji cha Mbare kwenye mji mkuu Harare, hapo jana.
Msemaji wa chama hicho cha Movement for Democratic Change-MDC, Douglas Mwonzora, amewashutumu wafuasi wa Rais Robert Mugabe kuhusika na tukio hilo.
Katiba hiyo mpya itadhibiti mamlaka ya Rais Mugabe na kuweka misingi ya kufanyika kwa uchaguzi mwezi Julai, mwaka huu.
Uchaguzi huo utahitimisha makubaliano yaliyokumbwa na matatizo ya kugawana madaraka kati ya Rais Mugabe na Waziri Mkuu Tsvangirai.-DW.

MNYIKA::Tutaandamana kudai maji

MBUNGE wa Ubungo John Mnyika leo ataongoza maandamano ya amani kwenda Wizara ya Maji kupata majibu kuhusu matatizo ya maji, licha ya kuzuiwa na Jeshi la Polisi. 
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, ACP Charles Kenyela amekataza maandamano na mkutano huo kwa madai kuwa eneo la Manzese Bakhresa walilopanga kufanyia mkutano ni maegesho ya magari ya mizigo. 
Akizungumza kwa niaba ya Mnyika, mratibu wa maandamano hayo kutoka ofisi ya mbunge, Gaston Garubindi, alisema kuwa maandalizi yamekamilika na mbunge huyo ataongoza kama ilivyopangwa. 
Garubindi alisema kuwa Kenyela amewadanganya wananchi kwa kueleza kuwa Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe hakuwa na taarifa wakati ofisi ya mbunge ilimwandikia barua yenye kumbukumbu namba OMU/MJ/001/2013 na nakala nyingine kupelekwa kwa viongozi wengine wa wizara hiyo.

RAFIKI WA RAILA ODINGA AMPA TALAKA MKEWE KWA KUMSIFIA UHURU KENYATTA KUWA NI HANDSOME

Rafiki wa karibu wa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga Jumatatu hii anadaiwa kumpa talaka mke wake baada ya kumsifia Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta ni ‘handsome’ mbele yake.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Kenya, mwanasiasa huyo wa chama cha CORD anayetokea magharibi mwa Kenya, alikuwa akitazama taarifa ya habari akiwa na mke wake na ndipo alipoonekena Uhuru Kenyatta kwenye TV akizungumza na wawakilishi wa nchi mbalimbali nyumbani wake.
Baada ya kumuona mke huyo ambaye ana miaka 30 na kitu alisikika akisema kwa sauti ya chini kuwa anapenda muonekano wa Uhuru Kenyatta.
Hata kabla hajamaliza neno Kenyatta, inadaiwa kuwa mwanaume huyo aliye na ukaribu na Raila Odinga, alimpa kichapo cha haja na kumfukuza nyumbani usiku huo.

Simba hapatoshi leo,mkutano wa wanachama wake wapigwa stop.!

 WAKATI wanachama takribani 700 wanatarajia kufanya mkutano wa dharura leo Mnazi Mmoja, uongozi wa klabu hiyo umepiga stop kumkutano huo kwa madai kuwa wanachama hao hawana haki ya kuitisha mkutano wakati tayari uongozi ulishatoa tamko la kufanya mkutano huo wa dharura wakati wowote kuanzia sasa.

Uongozi huo wa Simba kupitia kwa ofisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga ulisema  kuwa mkutano utakaofanyika leo ni batili kwa kuwa hauna baraka za uongozi na kuwataka wanachama wa Simba kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho mwenyekiti wao Ismail Aden Rage akiwa India kwenye matibabu na anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki ijao.

Kauli hiyo ya uongozi imekuja ikiwa leo wanachama hao wakitarajia kufanya mkutano wao kwa mujibu wa katiba yao ibara ya 22 ambayo inatamka wazi wanachama wasiopungua 500 wana haki ya kuandaa mkutnao mkuu kama mwenyekiti hayupo tayari kuitisha mkutano ndani ya siku 30.

Hata hivyo jana Kamwaga alisema "Mwezi uliopita mwenyekiti alitangaza kuitisha mkutano wa dharura siku yoyote ajenda ingekuwa moja tu kujadili mwenendo wa klabu bahati mbaya alishikwa maradhi ikabidi aende India kutibiwa, kuna uwezekano mkubwa akarejea wiki ijayo.

"Uongozi umeridhia kufanyika kwa Mkutano wa wanachama. Kimsingi, kama uongozi umeridhia, hakuna mwanachama mwingine anayeweza kuitisha mkutano mkuu mwingine, hao wanaoitisha mkutano wana nguvu gani ya kisheria kufanya hivyo?  Walichaguliwa na nani kuwakilisha wanachama? Lini na wapi?" alihoji Kamwaga.

"Uongozi  unaweza kuitisha mkutano kwa vile wenyewe ndiyo wenye leja ya wanachama, Klabu ina database yake ya kompyuta inayotambua wanachama walio hai na wasio hai, hakuna mtu mwingine yeyote, aliye nje ya uongozi huu anayefahamu wanachama walio hai na wasio hai hao wanachama wanaoitana kufanya mkutano, wamehakikiwa na nani kubaini uhalali wao huo?"

Alisema wanachama wanaolazimisha kufanyika kwa mkutano wana ajenda  binafsi na si za maslahi ya klabu, Kama kweli wangekuwa na nia njema na klabu wangesubiri mkutano ambao utaitishwa punde na kwamba mkutano huo wa leo una lengo la kuleta vurugu na mifarakano ndani ya klabu yao.

" Michezo ni amani na furaha na michezo si vurugu,  uongozi wa Simba umetoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na ubatili wa mkutano huo, tunapenda kuwaomba wanachama wetu wasiopenda fujo na vurugu kwenye michezo kukaa mbali na mkutano huo kwa vile vyombo vya dola vitaufuatilia.

"Uongozi hautajiingiza katika kutoa dhamana au msaada wa namna yoyote kwa yeyote ambaye atachukuliwa hatua na vyombo vya dola kutokana na kujihusisha na mkutano huo."alisisitiza Kamwaga.
Hata hivyo pamoja na kauli hiyo ya Kamwaga wanachama wa Simba kupitia kwa mmoja wa waratibu wa mkutano huo Mohamed Wandi wamesisitiza kufanyika kwa mkutano huo ambao utakuwa na ajenda mbili moja ikiwa ni mwenendo wa timu yao katika mashindano pamoja na kutokuwa na imani na uongozi wa Rage.

Watu wanne wafikishwa mahakamani wakituhumiwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe..


Marehemu John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe..

*******


Watu wanne wamefikishwa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya wakituhumiwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe..
Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe aliaambia Mahakama hiyo Mbele ya Jaji Samweli Karua kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Mei 15,2011 katika Kijiji cha Mpandapanda kata ya Kiwira Wilayani Rungwe kinyume na kifungu cha 196(16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hakimu Mwakalinga ambaye ndiye mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo akiwa na Daudi Mwasipesya,Obote Mwanyimbili na Kelvin Maurus Myovela ambao wanatuhumiwa kumuua John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Awali baada ya kupandishwa kizimbani watuhumiwa kujibu kesi inayowakabili yenye namba 31/2012 walimkataa Wakili aliyejulikana kwa jina moja laMwakabubu aliyekuwa ameteuliwa kwa ajili ya kuwatetea kwa madai kuwa hawana imani naye kutokana na mwenendo wa kesi alizosimamia.
“Mtukufu Jaji kabla ya kesi yetu haijaanza kusikilizwa tunaomba kubadilishiwa Wakili kwa sababu huyu Mwakabubu hana uwezo na tumeona kesi ndogo tu anababaika na kesi yetu ni kubwa tunaona wazi kabisa kuwa hataweza kututetea” alisema Mwakalinga Mshitakiwa namba moja.
Kufuatia ombi hilo Jaji Karua alikubaliana nao ambapo alimteua Wakili mwingine ambaye ni Sambwee Shitambala ambaye walimkubali kabla hajawaongezea wakili mwingine ili asaidiane na Shitambala ambapo alimtaja Wakili Zakia Selemani.
Akisoma mashtaka yao Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 19, Mei 2011 majira ya jioni marehemu akiwa anatokea Mbeya mjini akirudinyumbani kwake Kiwira Wilayani Rungwe alifika Nyumbani akiwa na gari lenye namba za usajili T 127ACZ Nissan (Double cabin).
Namkambe aliongeza kuwa baada ya kufika nyumbani kwake alipiga honi ya gari kwa ajili ya kuomba kufunguliwa geti la mlango ambapo baada ya kusikia honi hiyo alitoka Mjomba wake ambaye baada ya kumfungulia aliambiwa ashushe Kuku aliyokuwa amewabeba nyuma ya gari yake.
Alisema kabla ya mjomba wa Marehemu hajaanza kushusha kuku kwenye gari alitokea mshitakiwa namba moja akiwa na siraha ambapo alimwamuru asifanye lolote ndipo akaanza kufyatua risasi akimwelekezea marehemu kisha kumuuana kutoweka kusiko julikana.
Akijibu tuhuma hizo Wakili wa Utetezi Shitambala na Zakia walikana washtakiwa hao kuhusika na matukio hayo pamoja na baadhi ya vielelezo vilivyotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha kuhusika kwa wateja wao.
Walisema mtuhumiwa wa kwanza hakuwepo Wilayani Rungwe siku ya tukio ambapo walisema atakuwa na mashahidi ambao watathibitisha kwamba hakuhusika ambao waliwataja kuwa ni pamoja na yeye mwenyewe, Askari Magereza wawili wa gereza la Tukuyu Wilayani Rungwe waliotajwa kwa jina moja moja la Hereda na Green.
Wengine ni Padeso Mwakipesile, Aneth Siandene Kalinga na Jumanne Mwakisole huku washtakiwa namba mbili, tatu na nne ambao hawatakuwa na mashahidi ambapo watasimama wao wenyewe kujitetea.
Namkambe aliiambai mahakama hiyo kuwa upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi zaidi ya 15 ambao aliwataja kuwa ni pamoja na Sofia Fungameza, Weston Gilbert,Magdalena Mgawe, Musa Jackson, Issa Mwaipopo, Teresia Ludovick na Williamu Mtanga.
Wengine ni askari Polisi Mwenye namba D2385 Sajent Michael wa Tukuyu, Inspekta Isaya Bwile wa Tukuyu, David Paul kutoka makao makuu ya Polisi Dar Es Salaam, Twaha kutoka kitengo cha Upelelezi makao makuu ya Polisi Dar Es Salaam, Haruna kutoka Polisi Tukuyu na WP3433 Agnes wa polisi Tukuyu.
Namkambe aliwataja mashahidi wengine katika kesi hiyo kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelezi (RCO) Mkoa wa Mbeya aliyehamishiwa makao makuu SSP Anacletus Malindisa, John Mayunga na Dk. D Z Matata kutoka ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali.
Jaji Karua aliahirisha kesi hiyo hadi hapo itakapopangwa tena kwa ajili ya kuendelea na kuwasilikiza mashahidi kutoka upande wa mashtaka baada ya kuambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na mashahidi wote wako tayari.
Na Venance Matinya, Mbeya.

BREAKING NEWZZZZZ .... Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maandamano ya Chadema Leo, Latoa Sababu Za Kupiga Marufuku Maandamano

 
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela
---
Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kanda ya Kinondoni limekataza maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika tarehe 16 Machi 2013 yaliyokuwa yameiratibiwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika yaliyolenga kufika katika Wizara ya Maji ili kufikisha ujumbe kwa Waziri wa Maji, Prof Maghembe kuhusu kero ya maji katika jimbo hilo ambayo haijatatuliwa wala kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo ACP, Charles Kenyela amesema endapo maandamano hayo yatafanyika:
   
 1. Upo wasiwasi wa kutokea kwa vurugu pale watakaposhindwa kufikia muafaka kuhusu hoja zao.

2. Amewasiliana na Ofisi ya Waziri husika na kufahamishwa kuwa haina  taarifa rasmi za ujio wa maandamano hayo.

 3. Barabara yatakakopita maandamano hayo ipo katika ujenzi na hivyo  maandamano hayo yatazuia shughuli za mkandarasi kukamilisha kazi yake kwa  wakati na kuisababishia Serikali hasara.

  4. Eeo ambamo maandamano hayo yanakusudiwa kutamatia ni dogo na hivyo  itasababisha usumbufu mkubwa
 
Credits: Lukaza Blog

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU KWA PAPA FRANCIS WA KWANZA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo Ijumaa 15 Machi, 2013 mchana amemtumia salamu za Pongezi Baba Mtakatifu Francis I kwa kuchaguliwa kwake kuwa Papa wa kanisa Katoliki Duniani na Vatican.
“Kuchaguliwa kwako ni ushuhuda tosha wa imani na heshima kubwa ambayo kanisa Katoliki inayo kwako, historia yako  na upendo wako wa kujali na kuwapenda wanyonge, unyenyekevu ni sababu tosha ya kuwapa wakatoliki, wasio wakatoliki na wasio wakristo pia kusherehekea uteuzi wako” Rais Kikwete amesema kwenye barua yake ya Pongezi kwa Papa Francis I.
Vatican na Tanzania imekua na uhusiano wa muda mrefu na hivyo Rais Kikwete amemhakikishia Papa Francis kuwa uhusiano huo utadumu na anatarajia utaimarika zaidi chini ya uongozi mpya wa Papa Francis I

“Mwisho”
Imetolewa na:
Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
IKULU
DAR ES SALAAM
15 March, 2013

Waziri Dkt. Mwakyembe abariki uzinduzi wa ‘Showroom’ mpya ya Magari ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (kulia) akiongozana na  Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani (kushoto) baada ya kuupokea Ujumbe kutoka nchini Ujerumani kunakotengenezwa magari aina ya Volks Wagon walipofika kushuhudia uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos wauzaji wa magari ya Volkswagon. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mh. Klaus Peter Brandes aliyeambata na ugeni huo.
  Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya  Kampuni ya Alliance Autos iliyopo Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa CFAO Motors Mama Maria Petro akipokea wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...